Lowassa for CHADEMA, mpokeeni

Lowassa for CHADEMA, mpokeeni

The dirt paka

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2011
Posts
371
Reaction score
69
Hey!
CHADEMA ninyi ni wanaharakati na waalimu wazuri nawashauri jambo moja gumu,
pamoja na kuchafuliwa kisiasa babu yetu Lowasa fanyeni mpango mumpe offa ya kadi, atawasaidia sana maana pamoja na mchango wake huko kijiwe cha CCM wamememnyima heshima yake kwaualimu wenu mumfundishe uzalendo na jinsi yakutumikia taifa na kuirejesha heshima yake kisha mumpe wajibu na majukumu. Maana kazi kubwa ya wanaharakati ni kuleta mabadiliko katika mambo mbalimbali. Go ahead CHADEM WAR FRONT, CCM WILL FOLLOW!
 
Wahenga walinena samaki mkunje..............................
 
he has already gone bad!! Ni kama chakula, hakifai tena kuliwa -kimeoza!
 
Angali mbichi,Lowassa umeshakauka(amekuwa kaukau)

Acheni zenu we apply alternatives, wamewezakuwaongoza maelf ya Watz katka maandamano sembuse lowasa!, samaki mkavu wanamloweka katika maji ya uvuguvugu akishalainika tu mnapika akiiva analiwa wamoto hamjui?
 
La kuvunda halina ubani.
Sikio la kufa halisikii dawa.
Lowassa for chadema??
Noooooooooooooooooooooooooooooooooooo.
 
itakuwa haina tofauti sasa, watu wale wale kila siku, tunataka watu wapya bana na si wale wale kwa sura mpya!
 
LOWASA karibu,kwa kipindi kifupi ulichokaa madarakani walau ulionyesha kuwajali watz,ulisimamia shule zikajengwa,mradi wa maji victoria mpaka kahama,mradi wa maji wachina dar bomba zilitandazwa lakini ulivyoondoka mpaka leo bomba zile hazijtumika.eti source ya maji haitoshelezi.barabara kama ya shekilango ilijengwa etc.karibu tuwaletee watz maendeleo!yaliyopita si ndwele!tunajua tatizo lilikuwa ni uwaziri mkuu
 
Ni mtendaji mzuri sana tena mjue ni safi akipewa uenyekiti CHADEMA.
 
Jamii yote inatambua kuwa Lowassa ni fisadi, endapo atapokelewa CHADEMA, lazima chama kinuke ufisadi.

Chukua mfano huu: nyumba safi ilyopigwa deki na kupuliziwa perfume inayonukia vizuri kisha aingie yule mnyama aitwaye Fungo, itakuwaje? Bila shaka nyumba lazima ichemke na kuchukua harufu yake!

Chonde chonde CHADEMA msithubutu kumpokea huyo jamaa.
 
Mwambie akamsaidie Mchungaji Mtikila kesi ya mgombea binafsi wakinda afanye maandalizi yake ya kugombea 2015 kama private candidate
 
mhmmm mhmm musiki wa Lowasa unaimbwa na wasio fiki zaidi
 
Lowassa Karibu CDM, ila kabla ya kuja nenda kaoge kwanza mbele ya umma kwa kutueleza bila kuacha kitu kuhusu kashfa zinazokukabili, hasa ushiriki wa swahiba wako JK. Huenda utasafishika mbele ya jamii, kabla ya hapo ukija utakichafua na chama kama ulivyofanya ccm.
 
LOWASA karibu,kwa kipindi kifupi ulichokaa madarakani walau ulionyesha
kuwajali watz,ulisimamia shule zikajengwa,mradi wa maji victoria mpaka kahama,mradi wa maji wachina dar
bomba zilitandazwa lakini ulivyoondoka mpaka leo bomba zile hazijtumika.eti source ya maji haitoshelezi.
barabara kama ya shekilango ilijengwa etc.karibu tuwaletee watz maendeleo!yaliyopita si ndwele!tunajua tatizo
lilikuwa ni uwaziri mkuu

Mmewasiliana naye akawatuma mmuombee au ni ushauri wenu tu, hata hivyo sidhani kama ni
wazo baya ingawa anapaswa kutubu kwanza kwa Watz kwa ufisadi wote alioufanya uliolitea
matatizo taifa hili ili apokelewe kama mtu mpya aliyezaliwa mara ya pili. Otherwise itakuwa ni
sawa na vichekesho vya pwagu na pwaguzi
 
Mwacheni mzee wa watu waziri mkuu mstaafu kwa kujiuzulu apumzike mara baada ya kumaliza kipindi hichi cha ubunge na kula maraha na vijisenti vyake.

Achana kabisa na siasa.
 
Nani kakwambia EL anaondoka CCM? jidanganye ndugu!!! HATOKI MTU FOR YOUR INFORMATION.
 
Chumvi ikiharibika itatiwa nini hata ikolee! Hasha itatupwa chini na kukanyagwa kanyagwa na wapita njia! He is not CHADEMA prototype though!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom