Rais Magufuli anavyomponza Mzee Lowassa ndani ya Chadema

Rais Magufuli anavyomponza Mzee Lowassa ndani ya Chadema

Albert Einstein

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2017
Posts
394
Reaction score
583
Jinsi Magufuli Anavyomponza Lowasa Ndani ya Chadema

Bavicha iliyokuwa ikiongozwa na Patrobas Katambi iliwahi kutangaza kufanya maandamano ya kwenda Dodoma kuizuia CCM isifanye mkutano wake mkuu. Wakati vijana hao wakiendelea na maandalizi ya mkakati wao, Lowasa aliibukia Arusha na kutoa tamko kuwa Chadema inapaswa kuhama kutoka ktk siasa za uanaharakati na kuanza kufanya siasa za kujiandaa kushika dola, ktk kikao hicho na waandishi wa habari Lowasa alizungumzia mpango wa BAVICHA na kutaka kufanya maandamano jijini Dodoma na kuwasihi waachane na mpango huo. Baada ya siku moja Mwenyekiti wa Chadema alitangaza kuzuia mpango wa BAVICHA na ukawa umeishia hapo, leo hii Patrobas Katambi ni DC wa Dodoma baada ya kuhamia CCM.

Lowasa alianza kwa kutembelea Ikulu na kufanya mazungumzo na Mh Rais Magufuli, baada ya mazungumzo aliongea na vyombo vya habari na kumpongeza sana Mh Rais Magufuli na serikali yake kwa jinsi inavyojitahidi kushughulika na matatizo ya wananchi pamoja na kasi nzuri ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, kauli ya mwisho ya Lowassa aliwaomba watanzania wakiona mtu anafanya mambo mazuri kama hayo wampe moyo na siyo kumkatisha tamaa. Baada ya kauli hiyo. Baada ya hiyo kila mtu anajua kilichofuata, japo yalikuwa ni mawazo yake binafsi lakini wengi walitegemea Lowasa aongee msimamo wa chama au msimamo wa viongozi wa chama.

Katika tukio la pili ni uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Monduli, katika harakati za vyama siasa kusimamisha wagombea, viongozi wenye ushawishi ndani ya chama walionyesha wazi nia na dhamiri ya kumtumia Fredy Lowasa kulikomboa jimbo hilo, wengi waliamini kwa ushawishi wa Fredy Lowasa na historia ya kiutendaji ya Mzee Lowasa ktk jimbo hilo, Fredy alitegemewa kuleta ushindani mkubwa. Baada ya kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa na Chadema kugombea nafasi hiyo Fredy Lowasa alitangaza kujitoa masaa machache kabla ya kamati kuu kukaa kupitisha majina ya wagombea.

Baada ya hili kutokea niliandika hapa nikasema kuwa, maamuzi ya Fredy Lowasa kujitoa siyo ya bahati mbaya, haya ni maamuzi yanayoelezea hatma na mtazamo wa baadae wa Lowasa ktk siasa. Japo ni haki yake kujitoa, lakini mpaka kufikia uamuzi wa kuchukua fomu, kuijaza na kuirejesha harafu baadae utangaze kujitoa ktk kipindi ambacho wenzako wengi wanakutegemea siyo rahisi kiasi hicho lazima kuna maelekezo yenye nguvu na heshima kifamilia yamekufanya ugeuze mawazo.

Katika uzinduzi wa Maktaba ya Kisasa pale chuo kikuu cha Dar es Salaam, viongozi wa upinzani mbalimbali walioalikwa ktk hafla hiyo hawakuhudhuria isipokuwa Lowasa pekee, Lowasa anazidi kuonyesha utofauti mkubwa sana baina ya kile anachokiamini na kile ambacho chama chake kinaelekeza kila mtu kiongozi wa chama na wanachama wakiamini. Chadema wanaelekezana viongozi wake na wanachama wake kumuona Magufuli kama adui yao mkubwa, lakini Lowasa anapita njia ya tofauti sana dhidi ya misimamo ya chama chao na viongozi wake

Kuna nadharia nyingi katika hili, ila baadhi ya nadharia ni kwamba
i) Huenda Lowasa amekomaa sana kisiasa, na hapendi kuchanganya itikadi na shughuli za maendeleo
ii) Huenda Lowasa hapendi kupangiwa nini cha kuwaza na nini cha kufanya, nasema hivyo kwa sababu mara kadhaa ameonekana kwenda kinyume na msimamo wa baadhi ya viongozi wa chama na hata mtazamo wa wanachama.
iii) Huenda Lowasa amestaafu siasa za ushindani, zile za kiharakati na kupinga chochote na sasa ameamua kuishi maisha yake kama kiongozi mstaafu wa serikali na siyo kama adui wa serikali aliyoitumikia tangu enzi.
iv) Huenda Lowasa anandaa mazingira mazuri ya kuhamia CCM siku za usoni hususani katika kampeni za uchaguzi mkuu wa 2020, kwa wanasiasa lolote linawezekana.

Mwisho niseme kuwa, Dr Wilbroad Slaa aliwahi kuhoji kuwa, Lowasa ni Asset au ni Liability? Kipindi kile wengi hawakumjibu iwapo Lowasa ni Asset au Liability kwa upinzani, badala yake waliishia kumtukana na kumuita msaliti. Siku za hivi karibuni tumeona wengi wakijaribu kurejelea kauli ya Dr Slaa kama majuto japo tayari wamechelewa.

Lakini mpaka leo binafsi ninaweza kusema kuwa Lowasa ni 'Asset' , cha msingi wapinzani wanatakiwa wajiulize kuwa hiyo 'asset' inamilikiwa na nani? Je fikra za hiyo Asset ziko tayari kupelekeshwa na kupangiwa nani wa kuonana nae na nani wa kumchukia? Lowasa ni

Wakipata jibu ndipo wataelewa kuwa upinzani wa Tanzania bado haujaanza kuheshimu na kujijengwa ktk misingi dhabiti, bado upinzani unaishi ktk matukio na matamko ya kukwepa uhalisia huku mtu mmoja au wawili wakiwa na nguvu kuliko wanachama wote.

Upinzani unaoweza kutamka kuwa wapo radhi kuungana na shetani ilimradi waingie Ikulu ni upinzani usiojua misingi yake na kama unaijua misingi ya uanzishwaji wake basi ni upinzani usioheshimu misingi ya uanzishwaji wake, na kama upinzani wa aina hiyo unayo misingi ambayo imeujenga basi ni misingi dhaifu sana ambayo nyumba inaweza kubomoka muda wowote hata ktk mawimbi ya upepo wa kawaida kabisa.

Kwahiyo ni wazi kwamba, upinzani lazima uanze kubadilika, uwe na misimamo ktk mambo yanayogusa misingi ya uanzishwaji wake na viongozi wake wawe na misimamo kuhusiana na masuala mbalimbali ya kitaifa waliyowahi kuyasimamia huko nyuma na sasa waonekana wakiyasimamia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom