Lowassa: Elimu ya bure inawezekana!

Lowassa: Elimu ya bure inawezekana!

Joined
Dec 11, 2010
Posts
3,321
Reaction score
6,331
Akiongea kupitia kituo cha channel 10 kwenye taarifa ya habari ya saa 1 leo 18 Nov,2012 Mheshimiwa Lowassa amesema serikali inaweza kugharamia elimu ya msingi na sekondari kwa wananchi wake kuwa bure, na elimu ya sekondari ikafanywa kuwa ya lazima na ya kiwango (quality). Ili kuwafanya vijana kushindana kikamilifu kwenye soko la ajira.

Kauli hii ni muendelezo wa wana CCM kuendelea kukubali sera kadhaa kwenye ilani ya CHADEMA ya mwaka 2010, juzi Kinana alisema serikali iondoe kodi kwenye vifaa vya ujenzi ili wananchi wawezi kujenge nyumba bora kwa ajili ya makazi.
 
Mwanangu Mtoi umeleta hoja nzuri ingawa nasita kukubaliana na Lowassa. Nani atawaruhusu tegemezi na ombaomba kutoa elimu ya bure wakati bajeti yao inategemea wafadhili. Laiti angesema kuwa kama tutasimamia raslimali zetu na kodi vilivyo hili la kutoa elimu bure lingewezekana ningemwelewa. Lowassa anaongea kama mgombea wa urais wa Marekani Mitt Romney. Ni pendekezo zuri ingawa sijui kama alionyesha jinsi ya kulifanikisha.
 
Na ili kulifanikisha hili lazma turudi kwenye nationalization of schools, kusiwepo na private schools ili usawa uwepo...baada ya hapo wahamie kwenye afya, nayo iwe bure!!
 
Na ili kulifanikisha hili lazma turudi kwenye nationalization of schools, kusiwepo na private schools ili usawa uwepo...baada ya hapo wahamie kwenye afya, nayo iwe bure!!

Nationalisation of private schools again? Ili tuwaachie wanasiasa nafasi ya kuziharibu shule nzuri kama Feza na Maria Golleti ziwe kama shule za kata au Jabal Hila??? No way!
 
Na kasema kwa nchi changa kama ya kwetu muhimu kuwa na intersectoral articulation kwa maana ya elimu,kilimo,miundombinu,viwanda kuwepo na direct link baina ya sekta na sekta..lowasa hata akikosa urais lazima tukubali kuwa ana vision na dira.
 
Hiyo ndiyo dhamira ya ccm kwa sasa na hili litawezekana pamoja na kuwasaidia wananchi katika ujenzi wa nyumba bora za kisasa chama changu pongezi kwa kuwajali watanzania
 
Mwanangu Mtoi umeleta hoja nzuri ingawa nasita kukubaliana na Lowassa. Nani atawaruhusu tegemezi na ombaomba kutoa elimu ya bure wakati bajeti yao inategemea wafadhili. Laiti angesema kuwa kama tutasimamia raslimali zetu na kodi vilivyo hili la kutoa elimu bure lingewezekana ningemwelewa. Lowassa anaongea kama mgombea wa urais wa Marekani Mitt Romney. Ni pendekezo zuri ingawa sijui kama alionyesha jinsi ya kulifanikisha.

Mkuu wangu Father of All
Naamini Lowasa ni sawa na kata inayoingia kwenye mtungi, si unakumbuka ule msemo "siri ya mtungi aijuaye kata", anajua kuwa serikali ni tegemezi sana hasa kwenye bajeti lakini nachelea kusema huenda ana kifuniko cha siri moyoni na anajua kuwa waliyo kuwa wanapinga yanawezekana.

Nakubaliana na wewe kuwa hajaonyesha njia kuwa itawezekana vipi (Romnesia) lakini naamini anajua kuwa kama wenzake wa ccm wakiwa naka uzalendo kidogo na huruma kwa taifa hili, wanauwezo wa kutoa elimu bure kuanzia msingi hadi sekondari na hata kuwapatia wastaafu wa nchi kiasi cha shilingi elfu 30 kwa mwezi kwa kuanzia ili angalau kuwapunguzia machungu ya kulipa bili za umeme za na maji au kununua mafuta ya taa kwa ajili ya vibatari vyao na kandili zao.

Inawezekana! Waliyopinga miaka 3 iliyopita leo wanakiri hadharani kuwa inawezekana. Hizi ni alama za wanafiki kwenye imani yangu.
 
Last edited by a moderator:
Na ili kulifanikisha hili lazma turudi kwenye nationalization of schools, kusiwepo na private schools ili usawa uwepo...baada ya hapo wahamie kwenye afya, nayo iwe bure!!

watahitaji complex ways ku handle wizi wa shule binafsi na za hovyo ambazo zitajaza wanafunzi bila kiwango ili walipiwe na serikali.Pia watahitajai kuweka viwango kwa wale watakaopenda kwenda kusoma shule zitakazoongeza huduma ktk nyanja mbalimbali za elimu na hivyo kuwa na bei za juu.Hawa ndio wakaofanya private zibaki milele.

COmplication hapa itakuwa ni rushwa ktk CCM na uwezo mdogo wa kufikiri beyond the box kwa mambo halali.
 
Lowassa akae kimya. Si aliwahi kutuambia kuwa ndege ya uchumi imeanza kupaa! ipi ya inflation 19%.

Baada ya kutuhumiwa kutaka kumuondoa Mwenyekiti wa CCM Dodoma sasa anataka kubadilisha mada kwa kuongelea mambo aliyoshindwa kuyafanya akiwa PM.Mpuuzi na mnafiki mkubwa sana.

Mtoi, ilani ya Chadema 2010 ina mambo mengi sana ya msingi. Tatizo ni kuwa wao wenyewe hawaamini kuwa yaliyomo ni kweli. Kwa msingi huo hutasikia katika mikutano mtu akiongelea au kufanya reference ya ilani hiyo.

Wengine wanatangaza Urais na wengine kujipanga katika ukuu wa mikoa na Uwaziri. Nani ataelezea Ilani.

Si unakumbuka hoja ya katiba ilivyoporwa!!! Chadema wametulia. In fact ile ilikuwa ni sehemu muhimu sana ya ahadi zao katika uchaguzi 2010 na iliwapatia umaarufu kwasababu kila mmoja aliona ni jambo sahihi.Wameikabidhi kwa Mwenyekiti wa CCM, na wala hatusikii nini msimamo wao kuhusu mambo muhimu ya kitaifa.
 
si sera ya chadema rejea 95 na 2000 cuf hao. mbona nyerere aliweza?
 
MKUU Mtoi!

Heshima kwako!

Ki ukweli WANA-MAGAMBA wanaucheza MDUMANGE wa CHADEMA kwa kasi kubwa sana. Tatizo hawa jamaa ni vilaza wa kutupwa. Yaani hata mtu kama ni Prof. Anapoingia MAGAMBANI hata akili yake yote inapotea kabisa.

Haya yote walisema hayawezekani wakati ule wa uchaguzi. Leo hii kila MWANA-MAGOME anaimba musiki wa ELIMU BURE, ambayo ilikuwa sera ya CHAMA KUBWA "CHADEMA".

Si hata unasikia Waziri wao wa Ujenzi anavyo aminisha Wadanganyika kwamba CCM imejenga barabara mpya sijui zenye urefu wa zaidi ya KM 11,000 wakati ukweli hawajajenga barabara bali wamekarabati barabara za zamani.
 
La msingi kwa level ya primary kuwepo na nationalization za shule zote na oleve bt frm alevel waruhusu private,then wakimaliza six wote wapitie jkt before kwenda chuo.
 
Sio kweli Mwanasiasa yeyote anaangalia kitu wanachotaka wananchi ndicho wanakisema. Akishapata atabadili maneno.

Lowassa ndiye aliyeasisi maisha bora kwa kila mtanzania. Baada kupata akageuka ati maisha bora haywezi kuja kwa kukaa vijiweni. Swali kuwa je alipoahidi haya hakujua kama kuna watu wanakaa vijiweni. Ingawaje kauli ilitolewa na JK lakini Lowassa ndiye aliyekuwa master mind wake. Kama angalijua hili haliwezekani anagalimshauri vinginevyo.
 
Huu ni unafiki wa kisiasa baada ya kuona wenzie wametibua mipangopa yake kule Dodoma, kama kweli alikuwa akifahamu hayo alitakiwa kuyasema 2010 wakati chama chake CCM kilipokuwa kikidai kuwa hilo haliwezekani. Lakini kwa kuwa alikuwa akinyanyuliwa mkono juu na JK alibana kimya. je ni watanzania wangapi hadi leo wameendelea kuteseka kwa kukosa elimu hiyo chini ya uongozi wa chama chake CCM katika hii miaka miwili?
 
Nilifikiri wamesham write off by now? kumbe bado yupo kwenye mbio?
OKA

KATOKA KICHWANI TU gamba kashindikana DHAIFU kaishia kulalama tu,makundi ,rushwa,magamba MBABE wa siasa maji taka yumo tu na mafisadi wenzie.hawatoki yakhe hao.
 
Mkuu wangu Father of All
Naamini Lowasa ni sawa na kata inayoingia kwenye mtungi, si unakumbuka ule msemo "siri ya mtungi aijuaye kata", anajua kuwa serikali ni tegemezi sana hasa kwenye bajeti lakini nachelea kusema huenda ana kifuniko cha siri moyoni na anajua kuwa waliyo kuwa wanapinga yanawezekana.

Nakubaliana na wewe kuwa hajaonyesha njia kuwa itawezekana vipi (Romnesia) lakini naamini anajua kuwa kama wenzake wa ccm wakiwa naka uzalendo kidogo na huruma kwa taifa hili, wanauwezo wa kutoa elimu bure kuanzia msingi hadi sekondari na hata kuwapatia wastaafu wa nchi kiasi cha shilingi elfu 30 kwa mwezi kwa kuanzia ili angalau kuwapunguzia machungu ya kulipa bili za umeme za na maji au kununua mafuta ya taa kwa ajili ya vibatari vyao na kandili zao.

Inawezekana! Waliyopinga miaka 3 iliyopita leo wanakiri hadharani kuwa inawezekana. Hizi ni alama za wanafiki kwenye imani yangu.
Mtoi,
I hate to say this, kwenye watu wanaoongelewa kuuwania uraisi, huyu bwana EL, licha ya wizi wake na ulevi wake wa madaraka akiwa nayo, ndio pekee ameonyesha kuwa na mawazo yenye meno ambayo nchi yetu inahitaji. Tatizo ni vigumu kumuamini kutokana na historia yake mbovu anapopewa madaraka. Tufanyeje sasa Watanzania?
 
Mwanangu Mtoi umeleta hoja nzuri ingawa nasita kukubaliana na Lowassa. Nani atawaruhusu tegemezi na ombaomba kutoa elimu ya bure wakati bajeti yao inategemea wafadhili. Laiti angesema kuwa kama tutasimamia raslimali zetu na kodi vilivyo hili la kutoa elimu bure lingewezekana ningemwelewa. Lowassa anaongea kama mgombea wa urais wa Marekani Mitt Romney. Ni pendekezo zuri ingawa sijui kama alionyesha jinsi ya kulifanikisha.

Ni rahisi sana kufanikisha.Tufilisi mafisadi wote.Halafu tuzibe mianya yote ya wizi wa nyara na fedha za serikali,ikiwa pamoja na madini.Pia tuzuie matumizi mabaya ya fedha za serikali ikiwa pamoja na kodi mbalimbali.Pesa iko kibao tu,wala hatuhitaji wezi wa nchi za magharibi.
 
Back
Top Bottom