Lowassa azikoroga serikali ya JK, CCM

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,013
Lowassa azikoroga serikali ya JK, CCM
• Pinda, Mukama, Nape watoa kauli za mshtuko

na Mwandishi wetu
Tanzania Daima

MWENENDO wa siku za hivi karibuni wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, unaonekana kuleta mshtuko na wasiwasi miongoni mwa viongozi wakuu wa serikali ya Rais Jakaya Kikwete na wale wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Daima Jumapili limebaini.

Hali hii ya mambo ndani ya CCM na miongoni mwa viongozi wa juu wa serikali katika hali ya uwazi na kificho imekuwa ikidhihirishwa na kauli zao zenye mwelekeo wa ukali, kukamia, dhihaka na pengine jeuri dhidi ya Lowassa.

Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima Jumapili umebaini kwamba, hali ya mshtuko miongoni mwa vigogo wa CCM na wale wa serikali kuhusu mwenendo wa Lowassa haukuanzishwa na Pinda bungeni juzi, bali ulianza siku chache tu baada ya kubainika kwamba alisafiri hadi Lagos, Nigeria na kuhudhuria sherehe za kuzaliwa za mmoja wa viongozi maarufu wa Kikristo duniani, Nabii, T.B. Joshua.

Mshtuko huo, kwa mujibu wa wadadisi wa mambo, ulibainishwa na habari iliyokuwa imeandikwa katika gazeti la UHURU linalomilikiwa na CCM zaidi ya wiki moja iliyopita, ambalo pasipo kutaja jina liliripoti kuhusu ziara hiyo ya Lowassa, nchini Nigeria na kuitaja kuwa moja ya mikakati ya mwanasiasa huyo kujaribu kukwepa kitanzi cha kuvuliwa gamba.

Hitimisho la mshtuko huo ni kauli iliyotolewa bungeni mjini Dodoma juzi na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakati akihitimisha mjadala wa hotuba ya makadirio na matumizi ya ofisi yake.

Pinda ambaye alikuwa akijibu hoja zilizotolewa na wabunge mbalimbali waliochangia mjadala wa bajeti ya ofisi yake kwa mwaka 2011 na 2012, alionekana akichukua mwelekeo tofauti wakati alipokuwa akitoa maelezo yaliyoonyesha dhahiri kulenga kauli iliyotolewa wiki iliyopita na Lowassa.

Habari ambazo Tanzania Daima Jumapili imezipata kutoka vyanzo vya kuaminika ndani ya serikali na kutoka kwa viongozi wa juu wa CCM zinaeleza kwamba, hali ya mambo ilikuwa ni tofauti miongoni mwa viongozi wa juu wa dola na wale wa chama tawala, tangu Lowassa alipozungumza bungeni kwa mara ya kwanza, katika kipindi cha zaidi ya miaka mitatu, Alhamisi ya wiki iliyopita.

Kikubwa kinachoonyesha kuwagusa viongozi wengi katika kauli hiyo ya Lowassa ni wito wake wa kuwataka viongozi wakabiliane na kile alichokiita ugonjwa ulioanza kuingia miongoni mwao wa kuogopa kutoa maamuzi.
Lowassa aliyekuwa akichangia hotuba ya Waziri Mkuu alieleza kusikitishwa na tabia hiyo hata kufikia hatua ya kuwaasa viongozi kutambua kwamba, kutoa maamuzi ni jambo jema na la muhimu kuliko kutotoa kabisa maamuzi.

Baadhi ya viongozi wa serikali na wale wa CCM waliozungumza na gazeti hili, mbali ya kukubaliana na maoni ya Lowassa ambaye ni Mbunge wa Monduli kwa tiketi ya CCM, walitafsiri maelezo ya mwanasiasa huyo kuwa shutuma dhidi ya viongozi waliopo madarakani hivi sasa.

Kada mmoja wa juu wa CCM aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa jina, alilieleza gazeti hili kwamba, mmoja wa viongozi walioonyesha kukerwa na kauli hiyo ya Lowassa ni Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama.

Mukama alikaririwa na chanzo hicho cha habari akieleza kukerwa na hatua ya baadhi ya wabunge wa CCM kuonekana wakishangilia kwa kupiga makofi wakati wote wa dakika 12 ambazo Lowassa alizitumia kuchangia bajeti hiyo ya waziri mkuu.

Wakati kada huyo akilieleza Tanzania Daima Jumapili mtazamo huo wa Mukama, maelezo aliyoyatoa kigogo huyo wa CCM katika Chuo Kikuu cha Mzumbe, Morogoro siku moja tu baada ya Lowassa kutoa maoni hayo, yanaweza kuthibitisha hisia za kiongozi huyo.

Mukama aliyekuwa akizungumza na makada wa CCM wa chuo kikuu hicho, alionyesha kukerwa na kikaragosi kilichochorwa katika gazeti moja linalochapishwa kwa Kiswahili la kila siku (siyo Tanzania Daima) ambalo lilimuonyesha kiongozi wa CCM akishindwa kuchukua maamuzi magumu ya kutoa barua kwa vigogo wa chama hicho wanaotajwa kukabiliwa na tuhuma za ufisadi.

Akizungumzia suala hilo, Mukama alisema msimamo wa CCM wa kuendelea na azima yake ya kujivua gamba ulikuwa upo pale pale na kwamba yeye na viongozi wenzake wa sekretarieti walikuwa hawana hofu yoyote ya kutekeleza maazimio yaliyofikiwa katika vikao halali vya chama chao.

Siku chache tu baada ya Mukama kutoa matamshi hayo, Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, aliibuka kupitia katika mtandao wa intaneti na pasipo kumung’unya maneno kama alivyofanya Mukama akajibu kwa sehemu hoja za Lowassa bungeni.

Katika matamshi yake, Nape alipingana na Lowassa kuhusu kuwapo kwa hofu miongoni mwa viongozi kutoa maamuzi na akatoa baadhi ya mifano kuwa kielelezo cha namna viongozi wa serikali na wale wa CCM walivyoweza kutoa maamuzi mazito.

Nape alisema maamuzi kama yale ya kulivunja Baraza la Mawaziri baada ya Lowassa kujiuzulu na ule wa CCM wa kujivua gamba ambao miongoni mwa walengwa wake ni Lowassa mwenyewe kuwa ni mifano ya namna viongozi wa CCM na serikali yake walivyo na uwezo wa kutoa maamuzi magumu.

Kiongozi mmoja wa juu wa serikali aliye karibu na Lowassa amelieleza Tanzania Daima Jumapili kwamba, hata kabla ya Pinda kujitokeza bungeni na kumjibu, Mbunge huyo wa Monduli alikuwa ameshadokezwa kuhusu matamshi yake ndani ya Bunge yalivyoibua minong’ono hasi ndani ya CCM.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo, mara baada ya Lowassa kupata taarifa hizo aliwasiliana na Ofisi ya Hansard ya Bunge na akachukua nakala ya hotuba yake na kuituma kwa Mukama kupitia kwa mmoja wa wasaidizi wake.

“Ninaweza kukuthibitishia kwamba, Lowassa amelazimika kuituma nakala ya hansard ya hotuba yake kwa Mukama, ili aisome baada ya kusikia kwamba ndani ya chama (CCM) yameibuka maneno mengi kwamba alitoa kauli zenye mwelekeo wa kukikebehi chama chake na viongozi wake wa juu,” alieleza kiongozi huyo.

Tanzania Daima Jumapili ilipowasiliana na Lowassa kwa simu jana kuhusu kuwapo kwa mvutano huo ndani ya CCM na kwamba hali hiyo ilimlazimu kuwasiliana na Mukama, hakuwa tayari kukubali au kukataa zaidi ya kusema; “Nashangaa yanatoka wapi maneno hayo? I have no comment (sina la kueleza).”

Wakati hayo yakitokea, uamuzi wa juzi wa Pinda kusoma orodha ndefu ya kile alichokiita maamuzi mazito ambayo yamepata kufanywa na Serikali ya Awamu ya Nne hata kusema ndiyo iliyofanya mengi kuliko serikali zote kabla, ni ushahidi wa namna viongozi serikali walivyoshtushwa na wasivyokubaliana na maoni ya Lowassa.

Ingawa Pinda katika orodha yake, kwa kujua au kutojua alijikuta akirejea kuyataja maamuzi magumu ambayo ndiyo hayo hayo yaliyotajwa na Lowassa wakati akichangia bajeti yake, hakueleza lolote kuhusu pendekezo la mtangulizi wake la kuitaka serikali ijipange sasa kujenga upya Reli ya Kati na bandari za Mtwara, Tanga na Dar es Salaam.

Akizungumzia hotuba hiyo ya Pinda waziri mmoja aliyezungumza na Tanzania Daima Jumapili jana, alisema kitendo cha Pinda kushindwa kueleza lolote kuhusu hoja ya msingi ya Lowassa ya kujenga upya bandari hizo tatu na Reli ya Kati ni kielelezo kwamba si tu kwamba serikali ilikuwa haina majibu bali ilikuwa imekerwa na hoja za Lowassa.

“Sikutegemea kumwona Pinda akinaswa katika mtego ule ule alionaswa Nape wa kudhani kwamba maamuzi mazito aliyozungumzia Lowassa yalikuwa ni yale ya kisiasa. Ni jambo lisiloingia akilini hata kidogo, Lowassa anazungumzia maamuzi ya kujenga upya miundombinu wao wanazungumzia siasa,” alisema waziri huyo.

Mbali ya hilo, waziri huyo alisema kitendo cha Pinda kulitumia tukio la kuvunjwa kwa Baraza la Mawaziri mwaka 2008 kuwa ni moja ya mifano ya maamuzi magumu kilikuwa ni kulidanganya Bunge kwa kupindisha ukweli na kumdhihaki Lowassa na hoja yake.
“Hivi ni nani hajui kwamba aliyesababisha Baraza la Mawaziri livunjike na siyo livunjwe alikuwa ni Lowassa aliyejiuzulu uwaziri mkuu na siyo serikali? Pinda halijui hilo au alitaka kulipotosha Bunge na Watanzania?” alihoji waziri huyo ambaye aliomba jina lake lisitajwe.

Hii sinema itaendelea hivi hivi hadi 2015, ukikaribia uchaguzi ccm wanabadilisha dvd wanaingia kwenye uchaguzi wakiwa pamoja na mapacha watatu.
 
Lowasa ana matatizo yake... Lakini anaona mbali...for me he is my option ...at least for now.....
 
Haaaa haaaa! Eti "kuvunja Baraza la Mawaziri" nao ulikuwa ni "uamuzi mgumu" wakati Baraza lilivunjika lenyewe!Pinda bwana, kaaazi kweli kweli!
 
Cheap politics

Very cheap indeed! Tanzania Daima imekuwa ikiendelea kujidhalilisha by the day.
Ukweli ni kwamba hakuna news kwa hotuba ya Lowassa pale bungeni. It was a populist approach which was intended to discredit his rivals with a view to gaining a political mileage. This move has boomeranged and it made matters worse for him. He is tainted beyond repair and no amount of manouvres can get him off the hook! He has lost a moral authority to speak anything for this country.
 
Ni Rais Mwinyi tu wakati huo aliyewahi kulivunja baraza la mawaziri waziri mkuu akiwa Joseph Sinde Warioba. Lilipoundwa upya John Cigwiyemisi Malecela akateuliwa kuwa waziri mkuu. Hii ya Lowasa wala Kikwete hakulivunja baraza, bali Waziri mkuu aliyekuwepo alijiuzuru, kwa hiyo kwa mujibu wa katiba na baraza linakuwa halipo. Hata ukifuatilia vyombo vya habari jinsi vilivyoripoti tukio hilo hautapata kichwa cha habari kisemacho "JK avunja baraza la mawaziri" bali utapata vichwa vya habari kama vile "JK akubali kujiuzuru kwa Lowasa" n.k.

Waziri mkuu anapojiuzuru huwezi kusema raisi kavunja baraza, maana waziri anajiuzuru kwa hiari wakati raisi anapovunja baraza maana yake ni kwamba mawaziri wote wanafutwa kazi kwa lazima. Hapa pinda kachemka!!!!
 
Pinda ni kama Puppet on a string! wanamchezesha wanavyotaka maskini! hawezi amua jambo lolote lile, na ile Mibunge ya CCM huwa inampigia makofi kila anapopiga propaganda pale bungeni, naona na spika kaamua kumnusuru na dhahma ya wabunge makini wa CHADEMA na NCCR kwa kumlinda eti asijibu maswali ya papo kwa papo!
 
Haaaa haaaa! Eti "kuvunja Baraza la Mawaziri" nao ulikuwa ni "uamuzi mgumu" wakati Baraza lilivunjika lenyewe!Pinda bwana, kaaazi kweli kweli!

Yaani! ni usanii mtupu! Haoni hata aibu kusema uongo ndani ya Bunge "tukufu"
 
Ni Rais Mwinyi tu wakati huo aliyewahi kulivunja baraza la mawaziri waziri mkuu akiwa Joseph Sinde Warioba. Lilipoundwa upya John Cigwiyemisi Malecela akateuliwa kuwa waziri mkuu. Hii ya Lowasa wala Kikwete hakulivunja baraza, bali Waziri mkuu aliyekuwepo alijiuzuru, kwa hiyo kwa mujibu wa katiba na baraza linakuwa halipo. Hata ukifuatilia vyombo vya habari jinsi vilivyoripoti tukio hilo hautapata kichwa cha habari kisemacho "JK avunja baraza la mawaziri" bali utapata vichwa vya habari kama vile "JK akubali kujiuzuru kwa Lowasa" n.k.

Waziri mkuu anapojiuzuru huwezi kusema raisi kavunja baraza, maana waziri anajiuzuru kwa hiari wakati raisi anapovunja baraza maana yake ni kwamba mawaziri wote wanafutwa kazi kwa lazima. Hapa pinda kachemka!!!!

Hili ni kweli kabisa na Watanzania wengi tukadhani ataunda Baraza la Mawaziri lenye sura mpya nyingi lakini akafanya usanii na kuwateua tena watu wale wale nadhani kuna mmoja au wawili ambao waliachwa lakini sikumbuki vizuri na Watanzania wengi walibaki kusikitika kwa kuvunja baraza la mawaziri na kisha kuteua tena watu wale wale.
 
Pinda ni kama Puppet on a string! wanamchezesha wanavyotaka maskini! hawezi amua jambo lolote lile, na ile Mibunge ya CCM huwa inampigia makofi kila anapopiga propaganda pale bungeni, naona na spika kaamua kumnusuru na dhahma ya wabunge makini wa CHADEMA na NCCR kwa kumlinda eti asijibu maswali ya papo kwa papo!

Nakubaliana nawe mkuu. pinda is so cheap kwa kweli. sometimes kuwa too good a person kunakufanya kutokuwa kiongozi mzuri. no wonder serikali haiwezi kutoa mamuuzi magumu. raisi kwa hulka yake hawezi kutoa maamuzi. pm wake nae hawezi kutoa maamuzi. so mnwisho wa siku hakuna wa kuamua chochote! terrible state
 
Back
Top Bottom