Hakuna kitu kibaya kama kukumbatia umasikini... na hakuna kitu kizuri kama kuempoer your people to be self sustainable
Si vyema si HAKI kutajrika kwa gharama ya kuwaibia jasho lao wale unaowatumikia katika utumishi wa umma.Ni lini Lowasa aliiacha kuwa Mtumishi wa Umma akenda mitaani kutafuta Mtaji kama Mze Mengi au Bhakhresa na kutajirika ...ni lini?.
Hivi unajua Taifa nalo pia uitaji kufanya tafiti ya jinsi gani ..siasa zime sababisha Watawala kuwaibia Wananchi na wao watawala kutajilika kwa kutumia Mali za Umma na kuwaingiza Waarabu na Wahindi katika keki ya kuwaibia Umma kama sehemu yao ya kuchuma kwa migongo ambayo leo hii unawaita maskini wakati wameibiwa rasilimali zao hivyo kuwafukarisha maisha yao kuoenekana maskini.
Hiv ukiwa Sweden ukaangalia maisha ya Wasweden utasema ni maskini wote au Matajiri wote...je ustawi wa Taifa unaangaliwa kwa idadi ya Matajiri au kwa idadi ya ubora wa maisha ya kila raia katika Taifa husika.
Mwalimu angekuwa hai sijui angesema nini kwa kauli kama hiyo ya dhihaka na matusi kwa Watanzania.Yani ndio ile una mwibia mtu na kumpiga juu.
Kuna kamsemo Watanzania wanako siku hizi, wanasema POLICE wetu uwa wanasema wewe iba, lakini katika wizi huo usimwage damu za watu, wezi wamwaga damu inasemekana POLICE wetu uwa hawana masihara nao..sasa kauli za namna hii ni sawa na kauli za kupitiliza na kujisahau ambako ni extreme.
Kuwaempower watu si kosa ni jambo jema unaweza kuwa empower Watanzania sekta nyingi nyingi kwa jinsi Taifa linategemea eneo hilo kuzalisha tija na kuleta faida kwa watu na Taifa.Inaweza kuwa ni kuempower watu sekta ya kilimo, labda kahawa, pamba, mpunga n.k. Inaweza kuwa ni kuwa empower watu eneo la Madini, dhahabu, almasi na Tanzanite, inaweza kuwa ni ubunifu wa mawazo mapya kwa vijana wanaomaliza shule na vyuo vyetu Tanzania..n.k.