Lowassa awajibu wanaomtuhumu kutovaa sare za CHADEMA, Asema ahukumiwe kwa matendo yake

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,787
1.jpg

Aliyekuwa mgombea wa Urais 2015 kwa tiketi ya CHADEMA na waziri mkuu mstaafu Mzee Edward Lowassa amesema si kweli kuwa havai sare za CHADEMA, na pia asihukumiwe kwa kuvaa au kutokuvaa sare hizo bali kwa matendo yake.

Waziri Mkuu huyu mstaafu tokea ajiunge na chama cha kikuu cha upinzani Tanzania amekuwa akituhumiwa na wanachama na wengine nje ya chama kwa kutokuvaa kabisa sare za chama maarufu kama gwanda.

Hata hapa JamiiForums kuna mada inayomtuhumu Lowassa kutokuvaa sare, zaidi soma => Kwanini Lowassa havai vazi rasmi la CHADEMA maarufu kama gwanda?

WanaJF mnasemaje kuhusu kauli ya Mzee Lowassa?
 
Kauli nzuri ,sio yule upande wa pili kazi yake ni mipasho tu SIJARIBIWI

swissme
Mkuu naona umekalia kiti cha Joseverest.

Sasa hapo kauli nzuri inatoka wapi? Swali kakwepa. Hana tofauti na ''Vita ya madawa ya kulevya haijawahi kumuacha mtu salama''
 
Kuvaa gwanda ndio uanachama kamili ? sidhani lakini mbona wengi wao wanavaa magwanda na wamekuwa wapiga dili wazuri tu, atujadili content ya kitabu kwa kuangalia jalada la kitabu.
 
we answer concrete questions only not questions of this nature.
Mzee hivi unajua kuwa neno concrete manaake ni zege?
Aliyekuwa mgombea wa Urais 2015 kwa tiketi ya CHADEMA na waziri mkuu mstaafu Mzee Edward Lowassa amesema si kweli kuwa havai sare za CHADEMA, na pia asihukumiwe kwa kuvaa au kutokuvaa sare hizo bali kwa matendo yake.

Waziri Mkuu huyu mstaafu tokea ajiunge na chama cha kikuu cha upinzani Tanzania amekuwa akituhumiwa na wanachama na wengine nje ya chama kwa kutokuvaa kabisa sare za chama maarufu kama gwanda.

Hata hapa JamiiForums kuna mada inayomtuhumu Lowassa kutokuvaa sare, zaidi soma => Kwanini Lowassa havai vazi rasmi la CHADEMA maarufu kama gwanda?

WanaJF mnasemaje kuhusu kauli ya Mzee Lowassa?
 
Ni kweli hana ulazima wa kuvaa gwanda. Lakini hebu tupate mfano huu mdogo, shehe hawi shehe kwa kuvaa kanzu tu na wala kanzi haiongezi wala kupunguza ushee wake. Lakini pata picha shehe yuko msikitini anaswalishwa huku kavaa jeans na tshirt, hata kama ana mahubiri mazuri vipi na ni mnyoofu vipi haya mavazi hayatowaingia watu akilini. Ni kipi kinachomfanya special kiasi hawezi kuvaa hizo sare kama wenzake. Viongozi wa cdm kusoma hamjui ila hata picha hamuoni? Kwa kweli nikiikumbuka ile cdm yetu ya amsha amsha nashindwa kujua imekuwaje kwa kujichanga na huyo Lowassa kiasi kukipotezea chama mvuto kiasi hiki.
 
Yale yale ya mashabiki wa CHADEMA enzi zile kuhoji Nyerere na sare za CCM!!!!
 
Alikua anahojiwa na azam tv na Charles,amesema amevaa sana gwanda wakati yupo jeshini na alipoenda vitani kagera.kwa hiyo imetosha kuvaa gwanda hatavaa tena.
 
Back
Top Bottom