Lowassa autathimini mwaka mmoja baada ya uchaguzi

edo.gif

Aliyekuwa mgombea urais kupitia CHADEMA, Edward Lowassa amechambua mwaka mmoja wa uongozi wa Rais John Magufuli tangu aingie madarakani akisema kuna mafanikio machache katika baadhi ya maeneo, lakini maisha ya wananchi yamezidi kuwa magumu.

Lowassa ambaye katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, 2015 aliungwa mkono na vyama vya upinzani vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), alisema hayo jana katika andishi lake kwa vyombo vya habari.

Mwanasiasa huyo aliyewahi kuwa waziri mkuu katika Serikali ya Awamu ya Nne kabla ya kujiuzulu mwaka 2008, amesema katika andishi hilo kwamba, “kile ambacho tulikisema wakati ule kwa nini tunataka mabadiliko, hivi sasa kila mtu anakiona.

“Kwamba pamoja na mafanikio machache katika baadhi ya maeneo, lakini maisha yamezidi kuwa magumu, ajira imeendelea kuwa bomu linalosubiri kulipuka, elimu bure iliyoahidiwa siyo inayotekelezwa, utumishi wa umma umekuwa kaa la moto.”

Chanzo: Mwananchi
 
Mzee wa mvua za Thailand kaona aingie front mwenyewe baada ya wafuasi wake kuendelea kupotezwa na utendaji safi wa awamu hii!
 
View attachment 424349

Aliyekuwa mgombea urais kupitia CHADEMA, Edward Lowassa amechambua mwaka mmoja wa uongozi wa Rais John Magufuli tangu aingie madarakani akisema kuna mafanikio machache katika baadhi ya maeneo, lakini maisha ya wananchi yamezidi kuwa magumu.

Lowassa ambaye katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, 2015 aliungwa mkono na vyama vya upinzani vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), alisema hayo jana katika andishi lake kwa vyombo vya habari.

Mwanasiasa huyo aliyewahi kuwa waziri mkuu katika Serikali ya Awamu ya Nne kabla ya kujiuzulu mwaka 2008, amesema katika andishi hilo kwamba, “kile ambacho tulikisema wakati ule kwa nini tunataka mabadiliko, hivi sasa kila mtu anakiona.

“Kwamba pamoja na mafanikio machache katika baadhi ya maeneo, lakini maisha yamezidi kuwa magumu, ajira imeendelea kuwa bomu linalosubiri kulipuka, elimu bure iliyoahidiwa siyo inayotekelezwa, utumishi wa umma umekuwa kaa la moto.”

Chanzo: Mwananchi
Namwonea huruma lowassa bora atulie tu.
 
Mlidhani mtapewa material na Mzee Lowassa kuhusu aliyo ya ongea hususani ajira na elimu ili mdese maana haikuwa kipao mbele chenu mlidandia mbele ya safari ndio maana mnapata taabu kuyatekeleza kwa ufanisi.
 
Mzee unisamehe mimi kura yangu niliiharibu kwa sababu sikuona anaetosha kuwa rais,nilipendelea nchi ibaki SINGLE kwanza kabla ya haija-date rais mwingine!
 
Namwonea huruma lowassa bora atulie tu.
Huna sifa za kumuonea huruma Lowassa, yeye ndio anatakiwa kukuonea huruma wewe! Hivi nyinyi mbweha wa kijani huwa mnafikiria kwa kutumia viungo vyenu vya kukalia au kichwa? Huna hata senti moja mfukoni halafu eti "namuonea huruma Lowassa"!
 
  • Thanks
Reactions: Pai
Ila CHADEMA watu wa ajabu sana, Duniani kuna vituko leo hii Luwasa ni CHADEMA damu damu na wao wanashangilia.

Mwenyekiti CCM JF
 
EL: Ni mwanasiasa mwenye elimu ya masters kwenye nyanja sanaa. Aliwahi kugombea nafasi ya kuteuliwa kugombea urais 2005 akiwa na rafiki yake Kikwete katika chama chao CCM, ila akashindwa kuteuliwa. Rafiki yake Kikwete alimteua kua PM, nafasi ambayo, kwa kiswahili chake mwenyewe, aliachia ngazi kwa kashfa ya rushwa ya richmond. Aliomba tena nafasi ya kupeperusha bendera ya chama chake CCM kwenye kinyang'anyiro cha urais 2015, ila hakuteuliwa. Aliamua kukimbilia upinzani ili kuweza kugombea urais, fursa ambayo alitunukiwa na CDM katika mazingira tata na sababisha badhi ya viongozi wa kuu kama Dr. Slaa kutimka. Katika uchaguzi, ambao ulikua na ushindani mkubwa, alibwagwa na rais wa sasa JPM. Katika maneno muhimu aliyo wahi yasema kabla na kwakati wa kampeni ni kuwa "huwezi yazuia mafuriko kwa mikono, akishindwa urais ataenda kwao kuchunga, kama upinzani ukishindwa autashinda tena labda baada ya miaka 50 ijayo, waandishi wa habari wanamuonea, mapesa anayo toa kusaidia anapewa na marafiki zake, akishinda kipaumbele chake ni elimu elimu elimu" na kukiri kuwa hayo si maneno yake bali "ni ya PM mmoja wa UK.". Kwa kifupi huyo ndo EL.
 
Ila CHADEMA watu wa ajabu sana, Duniani kuna vituko leo hii Luwasa ni CHADEMA damu damu na wao wanashangilia.

Mwenyekiti CCM JF
Hata CCM ni wa ajabu pia, juzi juzi mnabana pua kukataa misaada ya nchi za magharibi kwa madai ya kumudu kujitegemea halafu leo mnaomba msaada kujengewa msikiti na uwanja wa mpira na nchi nyingine ya Afrika.
 
View attachment 424349

Aliyekuwa mgombea urais kupitia CHADEMA, Edward Lowassa amechambua mwaka mmoja wa uongozi wa Rais John Magufuli tangu aingie madarakani akisema kuna mafanikio machache katika baadhi ya maeneo, lakini maisha ya wananchi yamezidi kuwa magumu.

Lowassa ambaye katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, 2015 aliungwa mkono na vyama vya upinzani vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), alisema hayo jana katika andishi lake kwa vyombo vya habari.

Mwanasiasa huyo aliyewahi kuwa waziri mkuu katika Serikali ya Awamu ya Nne kabla ya kujiuzulu mwaka 2008, amesema katika andishi hilo kwamba, “kile ambacho tulikisema wakati ule kwa nini tunataka mabadiliko, hivi sasa kila mtu anakiona.

“Kwamba pamoja na mafanikio machache katika baadhi ya maeneo, lakini maisha yamezidi kuwa magumu, ajira imeendelea kuwa bomu linalosubiri kulipuka, elimu bure iliyoahidiwa siyo inayotekelezwa, utumishi wa umma umekuwa kaa la moto.”

Chanzo: Mwananchi

mnafiki mamvi huyu, alitakiwa aseme ndani ya mwaka mmoja: atcl imenunua ndege 2 na shirika kuanza kufanya kazi, elimu bure mpaka kidato cha 4 imeanza, ujenzi wa reli kwa standard gauge umeanza, mfumuko wa bei umeshuka kutoka 7% mpaka 4.x%, Tanzania ni moja ya nchi ambayo uchumi wake unakuwa kwa kasi na lengo la kufikia 7.2%, serikali inashugulikia mafisadi ndani ya utumishi wa umma na utashi wa kisiasa wa serikali kukabiliana na mafisadi unaonekana dhahili na mengine mengi.
 
Back
Top Bottom