Lowassa autathimini mwaka mmoja baada ya uchaguzi

Lowassa autathimini mwaka mmoja baada ya uchaguzi

Namuomba mh. aje kutusalimia kanisani kwetu. Au ndo mpaka karibu na Oct 2020?
 
Huyu Mzee atulie kimya, alitapeli fikra za watu eti ''Mkishapiga kura nendeni nyumbani, kura zangu nitazilinda mwenyewe na haitoibwa hata moja''.

Baada ya uchaguzi ''Nimeshinda kwa zaidi ya 62% lakini kura zangu zimeibwa''....Kuna mambo mengine yanatia hasira sana.
Kani alisema wongo
 
Hawa watu sijui hawana kazi za kufanya????? Uchao habari za Lowassa tu!! Hamjui ndio imetokaaaaaa? Hana nafasi tena! He is politically finished! period!
 
Lowassa autathimini mwaka mmoja baada ya uchaguzi.

Tarehe Kama ya leo mwaka Jana, ilikuwa siku muhimu sana kwa watanzania na Mimi binafsi.Niliwaongoza watanzania kupiga kura nikiwa mgombea wa upinzani.

Naamini nilileta sura na msisimko mpya katika siasa za Tanzania.Nilishirikiana na wenzangu kuionesha nchi yetu Demokrasia maana yake ni nini.

Napogeuka nyuma kuingalia siku ile, nasikia faraja kubwa sana hasa kwa jinsi watanzania walivyotuunga mkono na kuonyesha matumaini makubwa kwetu.Ujasiri na ushapavu wa hali ya juu aliyouonesha Mke wangu Regina wakati wa kampeni,ulinipa nguvu kubwa.

Chini ya Mwenyekiti wetu Freeman Mbowe,tuliendesha kampeni za kiungwana kama tulivyoahidi.Upepo ule ulivuma kwa kasi mpaka visiwani ambako Maalim Seif aliporwa dhahiri ushindi.

Kwa mujibu wa Tume isiyo huru ya uchaguzi, tulishindwa uchaguzi ule.Hatutaki kuendelea kuyalilia maziwa yaliyokwisha mwagika ambayo hayazoleki, lakini kile ambacho tulikisema wakati ule kwanini tunataka mabadiliko,hivi sasa kila mtu anakiona.

Pamoja na mafanikio machache katika baadhi ya maeneo lakini maisha yamezidi kuwa magumu, ajira imeendelea kuwa bomu linalosubiri kulipuka,Elimu bure iliyoahidiwa siyo inayotekelezwa,utumishi wa umma umekuwa kaa la moto,.Nasononeka sana nikiona viongozi wanavyoshindana kuwasweka ndani madiwani na viongozi wengine wa kuchaguliwa hasa wa UKAWA.


Nawashukuru sana wananchi kwa imani kubwa waliyoionesha kwangu na UKAWA kwa ujumla.Kumalizika kwa uchaguzi ndiyo mwanzo wa uchaguzi mwengine, kwahiyo mapambano ndiyo kwanza yameanza.Kasi,nguvu, ari na hamasa niliyonayo ni kubwa zaidi kuliko wakati mwengine wowote.

Edward Lowassa
Waziri mkuu mstaafu na Mjumbe kamati Kuu CHADEMA.
Note ÷Tarehe kama ya leo mwaka jana...Watanzania tulifanya mtihani wa hesabu (uchaguzi)...na sasa tunaendelea kuisoma namba....wale wa kanga na pilau za uchaguzi kimyaaa
Siamini kama Lowassa kuandika haya!!! MTU aliwahi kuwa Waziri Mkuu??? Anamlaumu nani sasa! Hayo si angeyafanya huko nyuma?? Kama ni yeye kweli basi aache unafiki!! Urais haupatikani kwa mbinu hizo!!
 
Hongera kwa kuwa mgombea wa urais lakini nadhani ni muda wa kumuacha Rais Magufuli afanye kazi ili kesho tuje tumuulize nini alichotufanyia kila jambo na wakati wake . Kama alivyosema Lowassa uchaguzi umekwisha anajiandaa kwa uchaguzi mwingine. Magufuli ndio Rais wa sasa acha atende kwa wakati wake tutamkumbuka kwa atakayotenda hivyo tumpe muda akiondoka atakuja mwingine nae atatenda kwa wakati wake .
 
MWINYI: nchi inaendeshwa kama gari bovu
Hali ilipofikia ni mbaya zaidi maana Marais karibia wote wastaafu wanamkosoa hadharani huyu mfalme.....ni kitu kikubwa sana kutokea! JPM akubali kushauriwa na kupewa mawazo mbadala nchi yetu sote! Pekeyake hatafika popote! Mgawanyiko ndani ya chama si kitu kizuri! Watendaji wataomba kupumzika hasa KM wa chama atatoka.......chama kikigawanyika na kisipokuwa na imani na mwenyekiti wao ni hatari! Akiona anazidiwa nguvu ataanza kutumia mabavu na dola kutawala kwa nguvu au ataamua kususa na kuamua kupumzika! La msingi akubaliane na wenzake na akubali ushauri nchi sio yake pekeyake na hawezi kurekebisha kila kitu.....aende taratibu! .....usalama wake pia maana hakuna alie amani hata kwa wanaomzuguka!!
 
Lowassa ndo basi tena, CCM ni maarufu kuliko wewe. Jifariji tu.
 
Back
Top Bottom