Lowassa autathimini mwaka mmoja baada ya uchaguzi

Lowassa autathimini mwaka mmoja baada ya uchaguzi

Kweli namba inasomeka hatujui tuanzie wapi tumalizie wapi! Potelea mbali chaguo letu wenyewe tumelipenda wenyewe wacha tuisome namba....................................ting ting, xxxxxxxx mbele kwa mbele mpaka tufunguke
 
Kura Yangu nilikupa sijawai kujutia wala kuwaza kwanini nilikupa.
Ila wale waliompa jamaa wanajuta mpka kesho.
mimi nilimpa kura magufuli... na wala sijawahi jutia uamuzi wangu.

japo namheshimu mzee lowasa. ila sijawahi fikiri kama angeweza kuwa president mzuri.
 
Mkuu uko sahihi. Hii inakwenda pia na kutegemea ushindi kwenye hizi mahakama zinazosemekana kuwa ziko huru.

Utegemezi wa kushinda katika mahakama hizo katika hali ilivyo ni "umajinuni mwingine".

Mwendo ilikuwa kuwekeza katika kupata katiba mpya -- ile ya Mzee Warioba.

Hivi kweli watu mlitegemea Lowassa ashinde mbele ya tume ya uchaguzi iliyoundwa na mwenyekiti wa CCM?

Huo ni umajinuni.
 
Earthmover you got it wrong 100% for ENL. Go back to your Education records
 
Dah....wale mawaziri 500, maRC 4000 na maDC 70000 walionunua suti wakiona uzi huu wanazidi kupagawa [emoji13] [emoji13] [emoji13]
 
Kuna watu wanazidi kuchukiwa day by day. Wao wanadhani ni wabingwa wa figisu figisu. Hata mnadiriki kuiba umeya. Ili tu apate cada wenu. Chama cha.macada, serikali ya macada na kazi za makada. Bila shaka hata shule inaweza kuwa ya makada iwapo mtu kama Ndalichako anaweza kuingizwa gengeni. Lol
 
Lowassa autathimini mwaka mmoja baada ya uchaguzi.

Tarehe Kama ya leo mwaka Jana, ilikuwa siku muhimu sana kwa watanzania na Mimi binafsi.Niliwaongoza watanzania kupiga kura nikiwa mgombea wa upinzani.

Naamini nilileta sura na msisimko mpya katika siasa za Tanzania.Nilishirikiana na wenzangu kuionesha nchi yetu Demokrasia maana yake ni nini.

Napogeuka nyuma kuingalia siku ile, nasikia faraja kubwa sana hasa kwa jinsi watanzania walivyotuunga mkono na kuonyesha matumaini makubwa kwetu.Ujasiri na ushapavu wa hali ya juu aliyouonesha Mke wangu Regina wakati wa kampeni,ulinipa nguvu kubwa.

Chini ya Mwenyekiti wetu Freeman Mbowe,tuliendesha kampeni za kiungwana kama tulivyoahidi.Upepo ule ulivuma kwa kasi mpaka visiwani ambako Maalim Seif aliporwa dhahiri ushindi.

Kwa mujibu wa Tume isiyo huru ya uchaguzi, tulishindwa uchaguzi ule.Hatutaki kuendelea kuyalilia maziwa yaliyokwisha mwagika ambayo hayazoleki, lakini kile ambacho tulikisema wakati ule kwanini tunataka mabadiliko, hivi sasa kila mtu anakiona.

Pamoja na mafanikio machache katika baadhi ya maeneo lakini maisha yamezidi kuwa magumu, ajira imeendelea kuwa bomu linalosubiri kulipuka, Elimu bure iliyoahidiwa siyo inayotekelezwa,utumishi wa umma umekuwa kaa la moto,.Nasononeka sana nikiona viongozi wanavyoshindana kuwasweka ndani madiwani na viongozi wengine wa kuchaguliwa hasa wa UKAWA.


Nawashukuru sana wananchi kwa imani kubwa waliyoionesha kwangu na UKAWA kwa ujumla. Kumalizika kwa uchaguzi ndiyo mwanzo wa uchaguzi mwengine, kwa hiyo mapambano ndiyo kwanza yameanza. Kasi, nguvu, ari na hamasa niliyonayo ni kubwa zaidi kuliko wakati mwengine wowote.

Edward Lowassa

Waziri mkuu mstaafu na Mjumbe kamati Kuu CHADEMA.

Note ÷Tarehe kama ya leo mwaka jana...Watanzania tulifanya mtihani wa hesabu (uchaguzi)...na sasa tunaendelea kuisoma namba....wale wa kanga na pilau za uchaguzi kimyaaa
Waziri uliyefukuzwa kwa kashfa ya wizi na si mstaafu ww!
 
Kuna watu wanazidi kuchukiwa day by day. Wao wanadhani ni wabingwa wa figisu figisu. Hata mnadiriki kuiba umeya. Ili tu apate cada wenu. Chama cha.macada, serikali ya macada na kazi za makada. Bila shaka hata shule inaweza kuwa ya makada iwapo mtu kama Ndalichako anaweza kuingizwa gengeni. Lol
Urrasa,Kimalio,Makundi,Lema,Shoo,Mungi na .......
 
Hivi kweli watu mlitegemea Lowassa ashinde mbele ya tume ya uchaguzi iliyoundwa na mwenyekiti wa CCM?

Huo ni umajinuni.
Hakuna marefu yakakosa incha, na hakuna penye mwanzo pakakosa mwisho.haya nayo yabubabe ,wiki wa kura,lkn pia maonevu yatakwisha.
 
Back
Top Bottom