Lowassa atahadharisha magadi soda Engaruka

Lowassa atahadharisha magadi soda Engaruka

OgwaluMapesa

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2008
Posts
10,942
Reaction score
437
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, amesema hatakubali kuona kiasi kikubwa cha magadi soda kilichogundulika katika Kijiji cha Engeruka Juu, kinageuzwa na baadhi ya watu kuwa balaa kwa wakazi wa eneo hilo badala ya kuwa neema kwao.

Badala yake amewataka wanakijiji hao kujipanga vizuri ili kujiendesha kibiashara kwa manufaa yao na taifa kwa jumla.

Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli (CCM), alifanya ziara ya kikazi ya siku moja kuzungumza na wakazi wa kijiji hicho kuhusu miradi ya magadi soda, umeme, barabara na maji.

Alisema hivi karibuni kumekuwa na ugomvi mara kwa mara katika rasilimali ya ardhi, lakini kwa eneo la Engaruka hakuna tatizo hilo.

Aliwaonya wakazi hao kuacha kushawishiwa na watu wachache kuuza maeneo yao kwa tamaa ya fedha za sasa, lakini hapo baadaye wakajikuta hawana kitu na kubaki kuwa maskini.

Akizungumzia mradi wa magadi soda, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NDC, Mlingi Mkucha, alisema utafiti waliokuwa wamefanya umebaini kuwapo kwa mita za ujazo trilioni 4 na milioni 700 za magadi soda katika eneo hilo, hali ambayo inaifanya Tanzania kuwa nchi ya tatu kwa kuwa na akiba kubwa ya magadi soda baada ya Marekani na Uturuki.

Chanzo: Nipashe
 
Mzee wa kuthubutu, mwenye uwezo wa kuvunja mikataba ya kilaghai bila kujali nini wasioitakia mema nchi yetu watasema.
 
Dah,bora maana na soda zitashuka bei,maana hili joto la Dar na Azam cola hazishikiki lol.Najua sasa soda zitashuka mpaka sh500 kwa mil350.
Ahsante Mungu,Ahsante kua mtanzania.
 
Yaani rasilimali zote zilizokuwepo Tanzania ameamua kuzungumzia magadi tu!! Na huyu ndiye anayetaka kuwa Rais wa Tanzania!!!

Kazungumzia magadi kwa sababu alikuwa kwenye eneo la uzalishaji wa magadi ya soda....
 
Yaani rasilimali zote zilizokuwepo Tanzania ameamua kuzungumzia magadi tu!! Na huyu ndiye anayetaka kuwa Rais wa Tanzania!!!

Jaribu kuelewa kwanza kabla ya kulaumu!
Mh. Lowasa ni Mbunge wa eneo Hilo lililogunduliwa magadi kwa hivi sasa hivyo anaongelea Madini ambayo yamegunduliwa ktk eneo lake hivi karibuni.
TUMPE nchi nzima ili asimamie na kutoa kauli kwa nchi nzima!
 
Mkuu umenena! Bila shaka hakuelewa sasa ameelewa
 
Uvccm Monduli, nimsikiavyo Lowasa, yeye mwenyewe atakuwa wakwanza kuwarusha hao wanakijiji. kwani uadilifu wake una mashaka makubwa.
 
Last edited by a moderator:
hivi magadi na Tanzanite kipi kipo juu huyu babu ni juha
 
Huyu ni mgombea wa Urais hii siyo siri. Inabidi kuongea kama mgombea wa Urais na siyo kama Mbunge kwamba atazilinda rasilimali zote za Tanzania yakiwemo hayo magadi. Kutoa kauli kama mgombea wa Urais ndio kuanza kujiuza/kujitangaza kwa Watanzania.

Jaribu kuelewa kwanza kabla ya kulaumu!
Mh. Lowasa ni Mbunge wa eneo Hilo lililogunduliwa magadi kwa hivi sasa hivyo anaongelea Madini ambayo yamegunduliwa ktk eneo lake hivi karibuni.
TUMPE nchi nzima ili asimamie na kutoa kauli kwa nchi nzima!
 
Yaani rasilimali zote zilizokuwepo Tanzania ameamua kuzungumzia magadi tu!! Na huyu ndiye anayetaka kuwa Rais wa Tanzania!!!

ungekuwa mwanasiasa ungezungumzia makaa ya Mawe Engaruka na magadi mchuchuma
we ni devision 5
 
Yaani rasilimali zote zilizokuwepo Tanzania ameamua kuzungumzia magadi tu!! Na huyu ndiye anayetaka kuwa Rais wa Tanzania!!!

Embu jaribu kuwa fair angalau kwa siku moja kwa mwaka na jaribu kusoma habari na kuielewa!
Bw.Lowasa ni Mbunge wa jimbo la Monduli na hayo Magadi Soda yako kwenye kijiji cha Engaruka ndani ya Jimbo la Monduli sasa ulitaka aongelee kuhusu Buzwagi au North Mara? na angefanya hivyo pia mngesema kwa nini anaongelea Majimbo ya watu wakati la kwake limemshinda halafu isitoshe Bw.Lowasa hajawahi kutamka kwamba anataka kuwa Raisi wa TZ ni ninyi tu ndio mnachechetuka!
 
Back
Top Bottom