LOWASSA: Arusha pagumu!

LOWASSA: Arusha pagumu!

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Waziri Mkuu Mjiuzulu na Mbunge wa Monduli,Edward Ngoyai Lowassa,amesema kuwa Jiji la Arusha ni gumu sana kisiasa hasa upande wa CCM. Lowassa aliyasema hayo jana hapa Arusha alipokuwa akizindua kampeni yake ya kichama ya kuwasaidia madereva wa pikipiki maarufu kama boda boda. Lowassa,dhahiri kabisa,alishangazwa na mapokezi hafifu ya kichama aliyoyapata huku akiarifiwa kuwa ziara hiyo haikubalikiwa na chama kiwilaya,kimkoa na hata kitaifa.

'Vijana wa Arusha wana bashasha kubwa. Ni wasikivu na waelewa.Lakini hawatabiriki kimaamuzi hasa ujapo wakati wa uchaguzi;wao na CHADEMA na CHADEMA na wao. Hapa pagumu sana.Arusha ni 'stronghold' ya CHADEMA' alisema Lowassa akionesha ukweli wa anachokisema.

'Nitakuwa makini na nivifanyavyo hapa Arusha kichama na kibinafsi' aliongeza Lowassa.

Chanzo: Mimi niliyekuwepo Arusha na sasa najiandaa kurejea Dar.
VUTA-NKUVUTE aka Mzee Tupatupa wa Lumumba Dar (sasa Arusha)
 
Last edited by a moderator:
Nasubiri thread yako kuhusu swala la filamu ya Maudodo
 
CCM wajiulize wamefanya nini hadi watu wa Arusha wakahamia CHADEMA, naona wanatafuta shuka kumekucha.
 
Hapa arusha tumeizika ccm kitambo sana.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
mimi sioni UGUMU wa kujivunia kwa Arusha kama Mwenyekiti wa Jiji anatoka CCM.Hii inaonyesha madiwani wengi ni wa ccm.X
 
Tupa Tupa sijasoma kabisa mawazo yako ya kujiridhisha kuhusiana na hii clip inayoitwa ya Bukoba boy, heri mh. Lowassa ameliona hilo na kwa taarifa Arusha akina mama ndo hawaipendi kabisa CCM. Nahitaji coment zako za kichunguzi kuhusu hii clip nafikiri unaweza dodosa hata muktaza wake katika utengenezaji.
 
safi ndio mambo ya M4C hata kenya soon ukweli utajulikana tu,tatizo la CCM ni mafundi sana wa kuiba kura,2010 tume ya uchaguzi inasema kura za urais zimepotea hivi inaingia akilini kweli?DAWA NI KWA VIJANA WENGI KU OMBA NAFASI ZA WAJUMBE WA MABARAZA YA KATIBA MWISHO TAREHE 20.03,2013
 
Ccm ni ng'onda, inanuka rushwa, wizi, ufisadi, ujasusi, mauaji, udanganyifu, ngono, udhalilishaji, .........
 
Arusha ni pagumu kweli kweli.....sio uongo alichosema Lowasa.......

Vijana wa Arusha wana bashasha kubwa. Ni wasikivu na waelewa.Lakini hawatabiriki kimaamuzi hasa ujapo wakati wa uchaguzi;wao na CHADEMA na CHADEMA na wao. Hapa pagumu sana.Arusha ni 'stronghold' ya CHADEMA' alisema Lowassa akionesha ukweli wa anachokisema.
 
2015 mbunge wa Arusha mjini atatoka CCM!Hutaki unaacha
 
VUTA-NKUVUTE ulichosema au kukiripoti ni sahihi sana, na katika kukabiliana na hali hii CDM waliibuibuka na usemi kula CCM kulala CDM. Hapo ndipo walipotoa kibali cha kuchukua chochote toka CCM wakiona ni haki yao maana hao ni mafisadi hivyo wanawarudishia indirect lakini kwenye kula hawawapi!!

Utamaduni huo umekubalika na ndiyo unawatesa wanaCCM.
 
Last edited by a moderator:
Arusha ni pagumu kweli kweli.....sio uongo alichosema Lowasa.......

Preta najilaumu sana sijui nilikuwa wapi nikapate toyoya kampeni kwa ajili ya CDM!
 
Last edited by a moderator:
ni kweli ni pagumu heri yake aliyeugundua ukweli na kuunena/ kuliko kujifanya kipofu
 
Waziri Mkuu Mjiuzulu- FISADI na Mbunge wa Monduli,Edward Ngoyai Lowassa,amesema kuwa Jiji la Arusha ni gumu sana kisiasa hasa upande wa CCM. Lowassa aliyasema hayo jana hapa Arusha alipokuwa akizindua kampeni yake ya kichama ya kuwasaidia madereva wa pikipiki maarufu kama boda boda. Lowassa,dhahiri kabisa,alishangazwa na mapokezi hafifu ya kichama aliyoyapata huku akiarifiwa kuwa ziara hiyo haikubalikiwa na chama kiwilaya,kimkoa na hata kitaifa.

'Vijana wa Arusha wana bashasha kubwa. Ni wasikivu na waelewa.Lakini hawatabiriki kimaamuzi hasa ujapo wakati wa uchaguzi;wao na CHADEMA na CHADEMA na wao. Hapa pagumu sana.Arusha ni 'stronghold' ya CHADEMA' alisema Lowassa akionesha ukweli wa anachokisema.

'Nitakuwa makini na nivifanyavyo hapa Arusha kichama na kibinafsi' aliongeza Lowassa.

Chanzo: Mimi niliyekuwepo Arusha na sasa najiandaa kurejea Dar.
VUTA-NKUVUTE aka Mzee Tupatupa wa Lumumba Dar (sasa Arusha)

Huyu angeenda kufuga ng'ombe na kutumbua pesa za ufisadi kabla hatujamtafuna...ni kati ya niwatamanio siku kikinuka bongo!
 
Mkuu nami nashangazwa na ukimya wa Mkuu VUTA-NKUVUTE na Mzee Mwanakijiji juu ya kinachojiri sasa kwa Lwakatare.Hawa ni watu makini kiintelijensia. Mnasubiriwa Wakuu...LOL

Mie nimehoji na kuomba mtazamo wa Wana JF juu ya ukimya usio wa Kawaida wa vijana wa Lumumba hasa Ritz na @Nnape Nauye kutosema chochote juu ya sakata la sinema ya Lwakatare. Inamaanisha nini?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom