Lowassa apewe CHADEMA aiongoze kuelekea 2020

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,999
NILIPOANDIKA pendekezo hili wakati wa kampeni bila ya shaka watu walifikiria natupa dongo la kisiasa tu kama sehemu ya Operesheni ya kukataa mabadiliko feki.

Nina uhakika wapo waliodhani kuwa nilitoa pendekezo la Lowassa kuiongoza Chadema wakati ule kama ngumi ya tumbo kwa uongozi wa Chadema hasa kwa vile nilishaonesha upinzani wangu dhidi ya kumpokea Lowassa na kumpatia mikoba ya kugombea urais kwa kupitia chama hicho. Sikuwa ninatania.

Siku za karibu na mara baada ya uchaguzi wa 2015 kumetokea baadhi ya viongozi wa Chadema, wanachama na mashabiki wa Chadema kuwa mafanikio kiduchu yaliyotokea wakati wa uchaguzi ni matokeo ya ujio wa Lowassa Chadema.

Imani hii imeanza kuaminika kiasi kwamba Lowassa anaanza kubebeshwa sifa zote kuwa kwa siku chache alizoweza kukaa Chadema na kuzunguka nchi nzima aliweza kuijenga Chadema kushinda wale waliokuwepo ndani ya chama hicho na kuenyeka kwa muda mrefu.

Simulizi hili jipya lina lengo la kuendeleza kile kile kilichotokea wakati ule wa uchaguzi – kuhalalisha ujio wa Edward Lowassa – Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa zamani wa Monduli – Chadema baada ya jina lake kukatwa katika chama kilichomlea – cha Mapinduzi. Kwamba, Watanzania watambue na kukubali kuwa Lowassa alikuwa ni mtaji mkubwa kwa Chadema.

Na ushahidi pekee wanaoutoa ni kutuonesha tu kuwa idadi ya wabunge wa kuchaguliwa imeongezeka kidogo na wabunge wa upinzani wameongezeka kuliko Bunge la 2010.

Kwamba, hata kushindwa kwao kufikia theluthi moja ya wabunge wote kwa kukosa majimbo machache ni ishara ya mafanikio ya ujio wa Lowassa. Kwamba, wakiwa na Lowassa wameweza kuchukua kwa mara ya kwanza uongozi wa Halmashauri za Jiji la Dar na kuweza kutoa mameya kitu ambacho hakikuwahi kudhaniwa kwa muda.

Kwamba, wameweza kuchukua halmashauri za miji ya Iringa, Moshi, Mbeya, Tanga, na Arusha na kuongoza mitaa mingi. Hili linaweza kuwa kweli kabisa. Lakini pia halielezei jinsi gani walipoteza pia Jiji la Mwanza, na mji wa Musoma na kuelekea kufutika kabisa katika kanda ya ziwa.

Lowassa ni kweli aliweza kuwa mtaji na kama hii ni imani ya viongozi hawa na kuwa ndio ushahidi wa kazi yake kubwa basi hakuna njia nyingine ya kumzawadia au kuonesha kuwa wanaamini kweli isipokuwa kumpa uongozi wa chama.

Kama Mbowe na timu yake yote walivyofanya kazi kwa miaka yote hii hawakuweza kuliteka Jiji la Dar, na hawakuweza kuongeza idadi ya wabunge kwa kiasi hicho ni wazi Lowassa ni mtaji mkubwa zaidi.

Na ukweli kuwa wanahusisha wabunge wachache waliowapata kuwa ni matokeo ya Lowassa na kazi yake kubwa basi hakuna namna isipokuwa kuonesha imani hiyo kwa vitendo.

Kama Mbowe na uongozi wote wa Chadema wanaamini kwa dhati kabisa kuwa bila ya ujio wa Lowassa wangepoteza viti vingi zaidi vya ubunge na wasingeweza kupata mavuno manono waliyoyapata basi Lowassa ni kiongozi sahihi kabisa wa kuivusha Chadema kutoka ilipo sasa kuelekea kwenye mafanikio zaidi.

Vinginevyo ni lazima tujiulize ni kiongozi gani mwingine ndani ya Chadema mwenye ujiko, uwezo, uzoefu na maono ya kuliinua taifa anayeweza kushindana na Lowassa?

Kama Mbowe mwenyewe aliona Lowassa ni mtu anayefaa kubeba bendera ya mabadiliko yeye hafai kuiongozi tena Chadema. Kama Lissu, Mnyika, Msigwa na wengine wote ambao walisimama nyuma ya Lowassa na kutubu makosa yao wenyewe na kumvisha kilemba cha ushujaa ni kitu gani zaidi wanahitaji kufanya isipokuwa kupiga magoti mbele yake na kujiweka chini ya uongozi wake?

Hii ndio njia pekee ya kuenzi mchango mkubwa ambao unadaiwa ulitolewa na Lowassa na ndiyo njia sahihi – yaani kumpa uongozi wa Chama ili akisuke na kukipanga vizuri zaidi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Serikali za Mitaa na ule wa wabunge 2019 na 2020 kwa mfuatano huo.

Mbowe asipofanya hivyo na viongozi wengine wasiposhinikiza hili litokee wananchi ni lazima watafikia hitimisho moja tu la kuchefua- vyote hivi ni njia za kuhalalisha kitu ambacho walijua siyo halali; namna ya kuficha kosa kubwa kabisa la kisiasa lililofanywa na viongozi hawa.

Chanzo:
Raia Mwema

Wito;

Maoni ya ziada yanatakiwa hasa katika kipindi hiki cha mpito kwa siasa za upinzani.Toa Hoja na sio kelele.
 
Je kama Lowassa hataki hiyo nafasi ya mwenyekiti wa CHADEMA Taifa afungwe kamba na kulazimishwa kuongoza CHADEMA? Lowassa ni Presidential Material na level yake si kuongoza wanachama wa chama fulani tu bali watanzania wote.
 
Mkuu hii itakuwa safi ukizingatia kuwa mambo yote yanaanzia kwenye chama.Presidential Matereal je akiwa mshindwa kwa maisha yote itakuwaje?
 
Andiko zuri sana chama cha chadema kimeuzwa. Mabadiliko ni lowassa na Lowassa ni mabadiliko. Shame on you vibaraka wa wapiga dili.
 
Sina la kusema.Ila Lowasa angefanikiwa kuongoza nchini Novemba 2015 nadhani sasa hivi tungekuwa tuna****
 
Ni mpaka ujue thamani ya hii habari, hivi hivi huwezi kuelewa ni kwanini iliandikwa. Mhariri angeombwa ushahidi asingetoa maana hana, lakini alijua anaiandika kwa maslahi gani. Na alijua anaiandika wakati gani. Na kikubwa alijua itapuuzwa kama ilivyopuuzwa.

Hoja iliyoletwa ina mantiki hata kama aliyeiandika na aliyeileta wamefanya hivyo 'kinazi'. Lakini ili mwandishi aweze kutendea haki mawazo aliyokuwa nayo wakati anaandika ilikuwa ni muhimu kwanza apitie mipango mikakati ya Chadema baada ya uchaguzi mkuu; ile ya muda mfupi, wa kati na mrefu. Vinginevyo, mawazo yake yatabaki kuwa haya maana yoyote!
 
NILIPOANDIKA pendekezo hili wakati wa kampeni bila ya shaka watu walifikiria natupa dongo la kisiasa tu kama sehemu ya Operesheni ya kukataa mabadiliko feki.

Nina uhakika wapo waliodhani kuwa nilitoa pendekezo la Lowassa kuiongoza Chadema wakati ule kama ngumi ya tumbo kwa uongozi wa Chadema hasa kwa vile nilishaonesha upinzani wangu dhidi ya kumpokea Lowassa na kumpatia mikoba ya kugombea urais kwa kupitia chama hicho. Sikuwa ninatania.

Siku za karibu na mara baada ya uchaguzi wa 2015 kumetokea baadhi ya viongozi wa Chadema, wanachama na mashabiki wa Chadema kuwa mafanikio kiduchu yaliyotokea wakati wa uchaguzi ni matokeo ya ujio wa Lowassa Chadema.

Imani hii imeanza kuaminika kiasi kwamba Lowassa anaanza kubebeshwa sifa zote kuwa kwa siku chache alizoweza kukaa Chadema na kuzunguka nchi nzima aliweza kuijenga Chadema kushinda wale waliokuwepo ndani ya chama hicho na kuenyeka kwa muda mrefu.

Simulizi hili jipya lina lengo la kuendeleza kile kile kilichotokea wakati ule wa uchaguzi – kuhalalisha ujio wa Edward Lowassa – Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa zamani wa Monduli – Chadema baada ya jina lake kukatwa katika chama kilichomlea – cha Mapinduzi. Kwamba, Watanzania watambue na kukubali kuwa Lowassa alikuwa ni mtaji mkubwa kwa Chadema.

Na ushahidi pekee wanaoutoa ni kutuonesha tu kuwa idadi ya wabunge wa kuchaguliwa imeongezeka kidogo na wabunge wa upinzani wameongezeka kuliko Bunge la 2010.

Kwamba, hata kushindwa kwao kufikia theluthi moja ya wabunge wote kwa kukosa majimbo machache ni ishara ya mafanikio ya ujio wa Lowassa. Kwamba, wakiwa na Lowassa wameweza kuchukua kwa mara ya kwanza uongozi wa Halmashauri za Jiji la Dar na kuweza kutoa mameya kitu ambacho hakikuwahi kudhaniwa kwa muda.

Kwamba, wameweza kuchukua halmashauri za miji ya Iringa, Moshi, Mbeya, Tanga, na Arusha na kuongoza mitaa mingi. Hili linaweza kuwa kweli kabisa. Lakini pia halielezei jinsi gani walipoteza pia Jiji la Mwanza, na mji wa Musoma na kuelekea kufutika kabisa katika kanda ya ziwa.

Lowassa ni kweli aliweza kuwa mtaji na kama hii ni imani ya viongozi hawa na kuwa ndio ushahidi wa kazi yake kubwa basi hakuna njia nyingine ya kumzawadia au kuonesha kuwa wanaamini kweli isipokuwa kumpa uongozi wa chama.

Kama Mbowe na timu yake yote walivyofanya kazi kwa miaka yote hii hawakuweza kuliteka Jiji la Dar, na hawakuweza kuongeza idadi ya wabunge kwa kiasi hicho ni wazi Lowassa ni mtaji mkubwa zaidi.

Na ukweli kuwa wanahusisha wabunge wachache waliowapata kuwa ni matokeo ya Lowassa na kazi yake kubwa basi hakuna namna isipokuwa kuonesha imani hiyo kwa vitendo.

Kama Mbowe na uongozi wote wa Chadema wanaamini kwa dhati kabisa kuwa bila ya ujio wa Lowassa wangepoteza viti vingi zaidi vya ubunge na wasingeweza kupata mavuno manono waliyoyapata basi Lowassa ni kiongozi sahihi kabisa wa kuivusha Chadema kutoka ilipo sasa kuelekea kwenye mafanikio zaidi.

Vinginevyo ni lazima tujiulize ni kiongozi gani mwingine ndani ya Chadema mwenye ujiko, uwezo, uzoefu na maono ya kuliinua taifa anayeweza kushindana na Lowassa?

Kama Mbowe mwenyewe aliona Lowassa ni mtu anayefaa kubeba bendera ya mabadiliko yeye hafai kuiongozi tena Chadema. Kama Lissu, Mnyika, Msigwa na wengine wote ambao walisimama nyuma ya Lowassa na kutubu makosa yao wenyewe na kumvisha kilemba cha ushujaa ni kitu gani zaidi wanahitaji kufanya isipokuwa kupiga magoti mbele yake na kujiweka chini ya uongozi wake?

Hii ndio njia pekee ya kuenzi mchango mkubwa ambao unadaiwa ulitolewa na Lowassa na ndiyo njia sahihi – yaani kumpa uongozi wa Chama ili akisuke na kukipanga vizuri zaidi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Serikali za Mitaa na ule wa wabunge 2019 na 2020 kwa mfuatano huo.

Mbowe asipofanya hivyo na viongozi wengine wasiposhinikiza hili litokee wananchi ni lazima watafikia hitimisho moja tu la kuchefua- vyote hivi ni njia za kuhalalisha kitu ambacho walijua siyo halali; namna ya kuficha kosa kubwa kabisa la kisiasa lililofanywa na viongozi hawa.

Chanzo:
Raia Mwema

Wito;

Maoni ya ziada yanatakiwa hasa katika kipindi hiki cha mpito kwa siasa za upinzani.Toa Hoja na sio kelele.
Mimi nakuona wewe ni CCM ama adui wa CDM. Huyu jamaa haifai CDM. Bora arudi alikotoka kama kweli upinzani wanataka kuwa serious kwa hapo walipofika ni kujizatiti na hoja za msingi si kusubiri makosa madogo madogo ya serikali ama kusubiri matokeo. Katibu kishapatioana anatakiwa aanze mizunguko nchi nzima maana hizo kelele zao za kila kukicha Bunge live hawatafika kokote. Usisahau magufuli kishatenga rushwa kijanja ya million 50 kila kijiji na hii lazima itapita bungeni maana ccm wapo wengi. Ndiyo maana nilisema mwaka jana Mbowe kama angekua mjanja angemwambia Eddo kuwa urais agombee 2020 ila asaidie waingize wabunge wengi bungeni. Japo ninahamasika na yanayofanywa na serikali lakini baadhi ya mipango ya serikali hii bila Bunge kali sioni kama mwisho mzuri. Rais na mawaziri wanafanya wanavyotaka baadhi ya mambo sababu Wanaque upinzani Kuna wqpiga zumari kama ccm. Katika kujadili maslahi ya Taifa tutumie akili zetu bila kuburuzwa na wanasiasa
 
Umetoa mchango mmzuri

Kaka hizi post zingine zimepitwa na wakati, vijalada vya kipuuzi ambavyo havina tofauti na mwanahalisi. Unakishabikia sababu wewe ni CCM sawa na wale wana CDM wanaposhabikia upuuzi wa mwanahalisi japo wanajua linaandika udaku. Siku zote Tabloid hazina wanahabari mahususi wenye weledi hasa katika nchi kama zetu ambazo hata Kubenea anaweza kuwa managing editor wakati hata shule hakwenda kwa kukiri mwenyewe. Unadhani kama managing editor ana elimu ya hapa na pale je waandishi wake wataweza vipi kuleta investigative material i hali wanajua wana editor kihiyo? Hayo manajarida yanafaa kuweka picha za uchi hapa Uk wanaita page 3. Kama kweli una hoja za msingi jikite katika magazeti kama The Guardian na mengineyo ambayo yanajulikana world wide.
 
Back
Top Bottom