Lowassa apewe CHADEMA aiongoze kuelekea 2020

Lowassa apewe CHADEMA aiongoze kuelekea 2020

Na sie tunataka Mchaga mbowe amuachie Kiti mmasai Lowasa........Mbowe aache kumbania Lowasa
mwenyekiti wa WAHA alisema yeye mwenyewe atakabidhi chama kwa atakayegombea Urais ambay ni Mama Mghwira
 
Lowassa again! Karibu tutasahau ni nani Mwenyekiti wa ccm taifa maana hatajwi tens katika ujenzi wa chama labda issue za ununuzi wa UDA na makontena tuu zinapojitokeza.
Na hakuna wa kuzitoa hadharani zaidi ya ukawa/lowasa maana sasa jiji ni letu na watakoma
 
Na Lula wa Ndali Mwananzela

NILIPOANDIKA pendekezo hili wakati wa kampeni bila ya shaka watu walifikiria natupa dongo la kisiasa tu kama sehemu ya Operesheni ya kukataa mabadiliko feki. Nina uhakika wapo waliodhani kuwa nilitoa pendekezo la Lowassa kuiongoza Chadema wakati ule kama ngumi ya tumbo kwa uongozi wa Chadema hasa kwa vile nilishaonesha upinzani wangu dhidi ya kumpokea Lowassa na kumpatia mikoba ya kugombea urais kwa kupitia chama hicho.

Sikuwa ninatania. Siku za karibu na mara baada ya uchaguzi wa 2015 kumetokea baadhi ya viongozi wa Chadema, wanachama na mashabiki wa Chadema kuwa mafanikio kiduchu yaliyotokea wakati wa uchaguzi ni matokeo ya ujio wa Lowassa Chadema. Imani hii imeanza kuaminika kiasi kwamba Lowassa anaanza kubebeshwa sifa zote kuwa kwa siku chache alizoweza kukaa Chadema na kuzunguka nchi nzima aliweza kuijenga Chadema kushinda wale waliokuwepo ndani ya chama hicho na kuenyeka kwa muda mrefu. Simulizi hili jipya lina lengo la kuendeleza kile kile kilichotokea wakati ule wa uchaguzi – kuhalalisha ujio wa Edward Lowassa – Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa zamani wa Monduli – Chadema baada ya jina lake kukatwa katika chama kilichomlea – cha Mapinduzi.

Kwamba, Watanzania watambue na kukubali kuwa Lowassa alikuwa ni mtaji mkubwa kwa Chadema. Na ushahidi pekee wanaoutoa ni kutuonesha tu kuwa idadi ya wabunge wa kuchaguliwa imeongezeka kidogo na wabunge wa upinzani wameongezeka kuliko Bunge la 2010. Kwamba, hata kushindwa kwao kufikia theluthi moja ya wabunge wote kwa kukosa majimbo machache ni ishara ya mafanikio ya ujio wa Lowassa. Kwamba, wakiwa na Lowassa wameweza kuchukua kwa mara ya kwanza uongozi wa Halmashauri za Jiji la Dar na kuweza kutoa mameya kitu ambacho hakikuwahi kudhaniwa kwa muda. Kwamba, wameweza kuchukua halmashauri za miji ya Iringa, Moshi, Mbeya, Tanga, na Arusha na kuongoza mitaa mingi.

Hili linaweza kuwa kweli kabisa. Lakini pia halielezei jinsi gani walipoteza pia Jiji la Mwanza, na mji wa Musoma na kuelekea kufutika kabisa katika kanda ya ziwa. Lowassa ni kweli aliweza kuwa mtaji na kama hii ni imani ya viongozi hawa na kuwa ndio ushahidi wa kazi yake kubwa basi hakuna njia nyingine ya kumzawadia au kuonesha kuwa wanaamini kweli isipokuwa kumpa uongozi wa chama.

Kama Mbowe na timu yake yote walivyofanya kazi kwa miaka yote hii hawakuweza kuliteka Jiji la Dar, na hawakuweza kuongeza idadi ya wabunge kwa kiasi hicho ni wazi Lowassa ni mtaji mkubwa zaidi. Na ukweli kuwa wanahusisha wabunge wachache waliowapata kuwa ni matokeo ya Lowassa na kazi yake kubwa basi hakuna namna isipokuwa kuonesha imani hiyo kwa vitendo. Kama Mbowe na uongozi wote wa Chadema wanaamini kwa dhati kabisa kuwa bila ya ujio wa Lowassa wangepoteza viti vingi zaidi vya ubunge na wasingeweza kupata mavuno manono waliyoyapata basi Lowassa ni kiongozi sahihi kabisa wa kuivusha Chadema kutoka ilipo sasa kuelekea kwenye mafanikio zaidi.

Vinginevyo ni lazima tujiulize ni kiongozi gani mwingine ndani ya Chadema mwenye ujiko, uwezo, uzoefu na maono ya kuliinua taifa anayeweza kushindana na Lowassa? Kama Mbowe mwenyewe aliona Lowassa ni mtu anayefaa kubeba bendera ya mabadiliko yeye hafai kuiongozi tena Chadema. Kama Lissu, Mnyika, Msigwa na wengine wote ambao walisimama nyuma ya Lowassa na kutubu makosa yao wenyewe na kumvisha kilemba cha ushujaa ni kitu gani zaidi wanahitaji kufanya isipokuwa kupiga magoti mbele yake na kujiweka chini ya uongozi wake?

Hii ndio njia pekee ya kuenzi mchango mkubwa ambao unadaiwa ulitolewa na Lowassa na ndiyo njia sahihi – yaani kumpa uongozi wa Chama ili akisuke na kukipanga vizuri zaidi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Serikali za Mitaa na ule wa wabunge 2019 na 2020 kwa mfuatano huo. Mbowe asipofanya hivyo na viongozi wengine wasiposhinikiza hili litokee wananchi ni lazima watafikia hitimisho moja tu la kuchefua- vyote hivi ni njia za kuhalalisha kitu ambacho walijua siyo halali; namna ya kuficha kosa kubwa kabisa la kisiasa lililofanywa na viongozi hawa.

Chanzo: Raia Mwema
Namheshimu sana mwandishi huyu nguli lakini ana haki ya kulisema lile analoliona linafaa kwa upande wake, na mimi pia nina haki hiyo hiyo. Sema usemalo lakini huwezi kupinga hata ukweli unaoonekana dhahiri. Huwezi kusema Chadema walipata ushindi kiduchu ukafumbia macho mawaziri zaidi ya sita walioangushwa katika uchaguzi. Huwezi ukasema ni ushindi kiduchu kwa UKAWA kuongoza halimashauri mbili kati ya tatu katika jiji la Dar es Salaam. Huwezi ukasema kwa uhakika kuwa ni ushindi kiduchu kwa UKAWA kuongoza majiji yote katika nchi hii ukiondoa Mwanza (Dar es Salaam, Tanga, Arusha na Mbeya) lakini ukiondoa majiji pia wanaongoza: Moshi, Iringa, Musoma na miji mingine. UKAWA wanaongoza Dar es Salkaam na Dar es Salaam ndiyo Tanzania, asilimia 80 ya mapato katika nchi hii yanatoka Dar es Salaam. Chama kinaongoza Ilala na ilala ndiyo Dar es Salaam yenyewe wewe unasema ni ushindi kiduchu. UKAWA wanaongoza halimashauri zote kubwa na kwa wajanja ukiondoa Mwanza halafu mtu anasema ati huo ni ushindi kiduchu sasa wangeshinda Namanyere na Namtumbo kumbe angesemaje.
 
Mwenyekiti wa WAHA wote. ...MWAMI NA NURU YA CHAMA alisema kuwa atayegombea Urais yeye atamwachia U Kiongozi mkuu wa chama...yaani U NURU..Mbona MWAMI anakuwa NKURUNZINZA
Mbowe from 2005 mpaka to infinity........hata JK atauacha uenyekiti wa ccm yy bado yupo tu.......hata hivyo MBOWE hamuwezi Lowasa...amuachie chama....asipomuachia 2020 CCM watashinda tena, na ACT itakuwa chama kikuu cha upinzani
 
Na hakuna wa kuzitoa hadharani zaidi ya ukawa/lowasa maana sasa jiji ni letu na watakoma
Na ndo maana tunasema Mbowe out Lowassa in.....kwenye nafasi ya uenyekiti
 
Mgwhira ni MKT wa ACT wazalendo....taratibu, kanuni, na sheria za chama anahakikisha zinatekelezwa, yeye huitisha vikao vya chama kuhakikisha sera, na ideology za chama zinatekelezwa. Zitto ni kiongozi mkuu wa chama, ana kazi ya kuuza sera na ideology za chama zikubalike, na kushawishi umma ukubali sera hizo......hawa wote wana mamlaka, moja ya kichama, mwingine nchi iiende vipi endapo watatwaa madaraka.

Lowasa hana cheo chochote CDM, lakini kwa muda mfupi amemshinda Mbowe, kwa kuleta wabunge wengi, na kutwaa halmashauri za majiji....ndo maana tunasema kwenye nafasi ya uenyekiti....Lowasa in and looser Mbowe out
Duuu kwa hiyo ka i ya zzk ya kuuza sera kwa watanzania amefanikiwa kwa 100% maana watanzania wamewakubali na kuwazawadia mbunge mmoja kama taa ya gari moshi?
 
yaani chama cha wenye akili kubwa kinakuwa na mbunge mmoja tu...heko mama mghwira

Duuu kwa hiyo ka i ya zzk ya kuuza sera kwa watanzania amefanikiwa kwa 100% maana watanzania wamewakubali na kuwazawadia mbunge mmoja kama taa ya gari moshi?
 
hahahaha. .....kweli nyie mnaota...malengo ya CHADEMA sio kuwa wapinzani.

mwambieni kiongozi wa WAHA aachie chama
Na ili tusiwe wapinzani milele...tunamtaka Lowasa kwenye uenyekiti.......shida ipo wapi?
 
Ukifika wakati wa kugombea uenyekiti wa chama anaweza kugombea, ila sidhani kama kamanda mkuu atakuwa tayari kuachia yale madaraka.
 
Mbowe from 2005 mpaka to infinity........hata JK atauacha uenyekiti wa ccm yy bado yupo tu.......hata hivyo MBOWE hamuwezi Lowasa...amuachie chama....asipomuachia 2020 CCM watashinda tena, na ACT itakuwa chama kikuu cha upinzani
ACT kuwa chama kikuu cha upinzani kwa kuongeza diwani mwingine Chigoma? Acha utani kwenye masuala mazito.
Kwanza huo ubunge sijui utapatikana wapi maana Mwami sijui ataomba kubadilishana na nani jimbo tena. Labda abadillishane na Lusinde ili akagombee Mtera
 
ACT kuwa chama kikuu cha upinzani kwa kuongeza diwani mwingine Chigoma? Acha utani kwenye masuala mazito.
Kwanza huo ubunge sijui utapatikana wapi maana Mwami sijui ataomba kubadilishana na nani jimbo tena. Labda abadillishane na Lusinde ili akagombee Mtera
Teeeeeh teeeeeeh teeeeeh mbavu zangu mieeee
 
naona dalili za edo kuwa mwenyekiti wa cdm, ila pia naona kama edo anaofc yake, hiv jamaa huwa anafika hata ufipa??

jamaa wanamyenyekea balaaa, ila ukweli ni huu japo ni mchungu, hata kama atagombea mara 100000 urais atausikia kama alivyo usikia maalim, ni maneno magum ila ndo ukweli...
 
Back
Top Bottom