Zitto amuanika Waziri wa Ujenzi, John Magufuli kwa upotevu wa Tsh 252 Bilioni

MPANDA Jr

JF-Expert Member
Nov 27, 2011
1,295
157
Ndugai amekuwa mtetezi wa ufisadi bungeni. Ni baada ya kamanda Zitto Kabwe kumuanika Waziri wa Ujenzi Bwana Magufuli kwa upotevu wa Tsh 252 Bilioni. Baada ya Zito kutoa hoja ya kutoa shilingi ya mshahara wa Magufuli, Ndugai akakurupuka kufunika hoja, eti kisa Zito ni Mwenyekit wa PAC. Safari bado ngumu.
"Mwaka 2011 tulipohoji kifungu chenye Fedha tshs 252bn kwenye Wizara ya Ujenzi, Naibu Waziri Harrison Mwakyembe alijibu "hizi Ni Fedha za miradi maalumu ya barabara ambapo tukipata misaada ya wafadhili hizi ndio michango yetu Kwa miradi". Bunge likapitisha. Hazina ikatoa pesa zote kwenda Wizara ya Ujenzi.

Mwaka huu tumehoji, hizi Fedha zilitumika namna gani? Waziri John Magufuli akasema "tulilipa Madeni".

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali anasema kwenye taarifa yake "ilitengenezwa miradi hewa ya barabara yenye namba ya mradi hewa. Pia hakuna uthibitisho kuwa Madeni yalilipwa kwani hakuna nyaraka za kuonyesha malipo". Tumehoji kutaka majibu, tumepigwa chenga.

Kweli? Tshs 252 bilioni hazina maelezo? Tutahakikisha Uwajibikaji katika hili"

Agosti 24, 2013 - Mwananchi
Tuhuma nzito: Magufuli, Mwakyembe, Lukuvi kufikishwa kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge

Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imesema itawafikisha kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge, Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe akiwatuhumu kwa kulidanganya Bunge.

Hatua hiyo ilitangazwa jana na Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe baada ya kumhoji Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi Herbert Mrango kuhusu hati ya mashaka waliyoipata kutoka kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), mwaka wa fedha 2011/2012.

Kamati hiyo ilieleza kuwa kwenye Bajeti ya mwaka huo kiasi cha Sh348,075,000,000 fedha za ndani zilizokuwa zimetengwa chini ya fungu lililotajwa kuwa ni la mradi maalumu (Special Road Construction Project) hazikutumiwa kwa malengo yaliyoelezwa bungeni.

“Ni vizuri leo uiambie kamati fedha hizi ziliombwa kwa kitu gani na zilitumika kwa jambo gani. Tunajua kwamba fedha hizi zilipunguzwa kiasi cha Sh95 bilioni na kupelekwa Wizara ya Uchukuzi, zilibakia Sh252.975bilioni katika kifungu hicho lakini kuna bilioni 100 zimetumika visivyo,” alisema Zitto, ambaye pia ni Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini (Chadema).

Alisema katika majumuisho ya Bajeti ya wizara hiyo, Dk Magufuli na Dk Mwakyembe wakati huo akiwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Lukuvi walitoa maelezo yasiyo ya kweli bungeni kuhusu fedha.

Alikariri maneno yaliyorekodiwa kwenye Hansard ya Bunge yaliyosemwa na viongozi hao watatu.

“Tunaomba fedha Sh252 bilioni kwa ajili ya kuanzia kazi za ujenzi wa barabara,” Zitto alisema akikariri maneno ya Dk Magufuli wakati anawasilisha bajeti.

“Fedha hizi zitachangia miradi ya wafadhili,” haya yalikuwa maneno ya Dk Mwakyembe wakati akifanya majumuisho.

“Hizi ni fedha kwa ajili ya counterpart fund,” alimkariri Lukuvi wakati akichangia hotuba ya wizara hiyo.

Zitto alisema CAG alihoji mwaka huu kuhusu matumizi ya fedha hizo na alitoa taarifa akidai kuwa fedha hizo zilikuwa miradi hewa na kasma kivuli.

Zitto alisema kuwa Dk Magufuli na Katibu Mkuu wake walipohojiwa walidai kutumia fedha hizo kulipa madeni.

“Kwa nini mlidanganya Bunge? Mliomba fedha za kuanza miradi maalumu. Hamkuomba fedha za madeni. Kwa nini mliunda kasma kivuli na kuifuta baada ya pesa kulipwa?” Zitto alimhoji Balozi Mrango.

Katika majibu yake, Balozi Mrango alisema kwa nia njema, fedha hizo zilitumika kuwalipa makandarasi waliokuwa wamechachamaa, huku baadhi yao wakisisitiza kusitisha kuendelea na miradi. Hivyo wakalazimika kuomba fedha kwa njia hiyo ili miradi kuendelea katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Zitto hakuridhishwa na majibu hayo akisema hapakuwa na haja ya kutumia fedha hizo kuwalipa makandarasi wakati kulikuwa na kasma yao ya awali. Alisema kama kulikuwa na haja hiyo, wizara isingeita mradi rasmi.

“Jambo hili siyo sahihi hata kidogo kulidanganya Bunge na hadi sasa wewe na waziri wako hamuonyeshi kukubali kosa hili, hata Waziri Lukuvi naye alisisitiza bungeni kwamba fedha hizo zinaombwa ili kutekeleza mradi maalumu lakini sasa imebainika sivyo, kwa mujibu wa Kanuni za Bunge tutawafikisha kwenye Kamati ya Maadili ili wahojiwe nao wajieleze kwa kulidanganya,” alisema Zitto.

Pia kamati hiyo imeitaka wizara hiyo kutoa ufafanuzi wa kina kuhusu matumizi ya Sh100 bilioni zilizotumika kinyume na maombi yaliyowasilishwa kwenye Bajeti ya mwaka huo wa fedha.

CAG ameshauri madeni yote ambayo Wizara ya Ujenzi inadaiwa yaorodheshwe ili yawe wazi kuepuka migongano katika matumizi ya fedha.

Alipoulizwa kuhusu madai hayo, Lukuvi alisema haelewi chochote na kusisitiza kuwa akipata taarifa rasmi za Kamati ya PAC, atatoa ufafanuzi.


Halmashauri zinavyotafuna mabilioni

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAACc), imeeleza namna mamilioni ya fedha za Serikali zinavyoibwa kutoka Hazina kupitia halmashauri za wilaya huku Ilala ikitajwa kuongoza kwa ufisadi huo.

Mwenyekiti wa LAAC, Rajab Mbarouk Mohammed aliwaambia waandishi wa habari jana kwamba Hazina imekuwa ikipeleka fedha kwenye halmashauri zikiwa zimezidi na kwamba kiasi kinachozidi hakirudishwi badala yake huliwa.

Alisema kamati hiyo imefanya uchunguzi kwenye halmashauri 43 na kubaini kwamba mtindo huo ndiyo unaotumika kuiba fedha za Serikali.

“Mwaka 2011/12 kiasi cha Sh1.5 bilioni zilipelekwa zikiwa zimezidi kwenye halmashauri hizo lakini hazikurudishwa Hazina kama inavyoonyesha kwenye ripoti ya CAG.

Alisema kati ya kiasi hicho, Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ilipewa ziada ya Sh213 milioni ikifuatiwa na Geita iliyopewa Sh129 milioni.

“Fedha hizo za mishahara zilipelekwa kwenye halmashauri hizo na Hazina kimakosa zikiwa zimezidi lakini watendaji wa hawakuzirudisha kama wanavyotakiwa kisheria badala yake zikayeyuka,” alisema.

Mwenyekiti huyo alisema kuwa uchunguzi huo pia ulibaini kwamba katika halmashauri hizo 43 kiasi cha Sh693 milioni hulipwa mishahara hewa ambayo wafanyakazi wake walishakufa na wengine kustaafu.

Alisema Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema ililipa mishahara hewa yenye thamani ya Sh79.4 milioni ikifuatiwa na Ukerewe iliyolipa Sh57.5 milioni.

Kwa upande wa fedha za miradi ya maendeleo, mwaka 2011/12, Hazina ilipeleka katika Halmashauri ya Mbarali, Mbeya Sh724 milioni kwa ajili ya Mradi wa Maendeleo ya Elimu Sekondari wakati mradi huo ulikuwa ukihitaji Sh70 milioni tu.

“Kiasi cha Sh654 milioni zilipelekwa kimakosa na Hazina lakini badala ya kurudishwa zilitumiwa katika mazingira ya kutatanisha,” alisema.

Alisema Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe ilipelekewa ziada ya Sh500 milioni na Mvomero ilipewa Sh85 milioni. “Kuna mtandao mkubwa wa Hazina na halmashauri ambao ukiachwa utaendelea kupoteza fedha nyingi za walipakodi,” alisema.
 
Hoja imepelekwa kwenye kamati ya mashirika ya umma baada ya Magufuli kushindwa kujibu ufisadi huu, japo naona hapa JF hoja imefungwa bila kufikia mwisho , moods why
 
Kaka usisumbuke. Ndungai ana Kadi ya CCM na Magufuli pia anayo ya CCM. Ukilijua hilo amini kuwa sasa hauna bunge bali jukwaa la kampeni.
 
KIKO WAPI,MAGUFURI HAJAJIBU CHOCHOTE.
ANAAMBIWA BILIONI 252. hakuna mahali amelijibu.
KABWABWAJABWABWAJA TU.
eti TANROAD inajulikana kimataifa(hela mzee iko wapi?Tunataka majibu)
Mara ooh: chombo hiki tusiki disturb kinafanya kazi nzuri.
MZEE SAWA KINAFANYA KAZI NZURI,KWELI KINAJULIKANA.
je hela iliyo potea bila maelezo iko wapi??????
 
Magufuli kashikwa pabaya -kashindwa kabisa kujibu kabaki kubwabwaja tu! Mara hawezi kuongelea shati bila vest.Zitto jembe
 
Zitto amemlipua Magufuli na ccm wamekwapua billion 252 kwa kujenga barabara hewa kwa mujibu wa report ya CAG na Magufuli ameshindwa kujibu.

huyu magufuli kazi yake kutaja kilometer kumbe anachakachua na kukwiba fedha za watanzania.
CCM n chama cha wezi.
 
Last edited by a moderator:
wamezidisha kutuibia hawa watu. Laana ipo juu yenu na itawatafuna hapa hapa ulimwenguni
 
Usije kushangaa hiyo bilioni 252,ikawa EPA nyingine,kwa maana ya kuwa CCM,inajiandalia pesa kwa ajili ya kuwanunulia waTZ,khanga,vitenge,fulana na kofia kwa ajili ya kuwahonga waTZ,kwenye uchaguzi wa mwaka 2015!!

Kama hilo wanaCCM,watalikanusha watueleze ni kwa nini suala hilo ia upotevu wa hizo bilioni 252,ambalo siyo habari za udaku wa wapinzani,bali ni ripoti ambayo imetolewa na CAG,wa serikali ya CCM,sasa ni kwa nini wabunge wa CCM,haewakutaka kabisa kuunga mkono hoja hiyo ya Zitto,ambapo ushahidi upo wazi kabisa kuwa hizo bilioni 252,zimechotwa na watendaji wa serikali ya CCM?!
 
Kwa kuwa hilo bunge limekuwa linatumiwa na wabunge wa CCM,kuwalinda watendaji wa serikali,wanaofisadi pesa za walipa kodi wa nchi hii,kwa hiyo vyombo bus habari vinapaswa walivalie njuga suala hilo la upotevu wa hizo bilioni 252,hadi Magufuli aeleze hizo pesa wamezipeleka wspi.

Hivi hawa viongozi wa CCM,wanajisikiaje wakati magereza yetu yamejaza wafungwa,ambao wengi wao wamefungwa kwa kesi za kubambikiwa,au kwa wizi mdogo mdogo wa kuku na visimu vya mchina,wakati hao majambazi wakubwa,waliokwapua bilioni 252,wakikingiwa kifua na Dr Magufuli?!
 
Huu upepo utapita tu...Watanzania ni mabingwa wa kusahau...I wish ningekuwa CDM, Hii ni bonge la point ya kuing'ang'ania mpaka mwisho...
 
KIKO WAPI,MAGUFURI HAJAJIBU CHOCHOTE.
ANAAMBIWA BILIONI 252. hakuna mahali amelijibu.
KABWABWAJABWABWAJA TU.
eti TANROAD inajulikana kimataifa(hela mzee iko wapi?Tunataka majibu)
Mara ooh: chombo hiki tusiki disturb kinafanya kazi nzuri.
MZEE SAWA KINAFANYA KAZI NZURI,KWELI KINAJULIKANA.
je hela iliyo potea bila maelezo iko wapi??????

nimeipenda sana....jamaa kakomaa kukariri alakini Zito nae kakomaa...!
ziko wapi,??!!
 
Kwa staili hii ilioonyeshwa leo na wabunge wa CCM,kuwakingia kifua waliokwapua,hizo bilioni 252,za wizara ya ujenzi,sasa ndiyo tunatarajia wsbunge hao ndiyo waishinikize serikali hii ya CCM,warejeshe zile dola za kimarekani milioni 197,ambazo zilitangazwa na benki kuu ya uswisi,kuwa vigogo 6 wa serikali ya CCM, wameficha mabilioni hayo ya mapesa huko nje ya nchi, sasa ndiyo kweli tuwatarajie wabunge hao wa CCM,wawe na ubavu wa kushinikiza hayo mabilioni yarejeshwe nchini??!!
 
Mwaka 2011 tulipohoji kifungu chenye Fedha tshs 252bn kwenye Wizara ya Ujenzi, Naibu Waziri
Harrison Mwakyembe alijibu "hizi Ni Fedha za miradi maalumu ya barabara ambapo tukipata misaada ya wafadhili hizi ndio michango yetu Kwa miradi". Bunge likapitisha. Hazina ikatoa pesa zote kwenda Wizara ya Ujenzi. Mwaka huu tumehoji, hizi Fedha zilitumika namna gani? Waziri John Magufuli akasema "tulilipa Madeni". Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali anasema kwenye taarifa yake "ilitengenezwa miradi hewa ya barabara yenye namba ya mradi hewa. Pia hakuna uthibitisho kuwa Madeni yalilipwa kwani hakuna nyaraka za kuonyesha malipo". Tumehoji kutaka majibu, tumepigwa chenga. Kweli? Tshs 252 bilioni hazina maelezo? Tutahakikisha Uwajibikaji katika hili.


COPIED.
 
Back
Top Bottom