Lowassa anastahili kuheshimiwa na kuenziwa!

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,991
Maamuzi ya Edward Lowassa katika uwanja wa siasa nchini yamelitendea haki taifa letu!

Kama asingekuwa Lowassa, kuna uwezekano mkubwa tusingempata Rais Magufuli!

Kama asingekuwa Lowassa na wanamtandao ndani ya CCM, kuna uwezekano mkubwa hata upinzani usingeshamili kwa kiwango cha sasa.

Kama asingekuwa Lowassa, tusingefahamu kwenye kambi ya upinzani kuna wanasiasa ambao wanachokisema hawakimaanishi!

Kama asingekuwa Lowassa, tusingefahamu kama vyama vyote vya siasa nchini ni maigizo mengi!

Kama asingekuwa Lowassa, tusingefahamu kwenye kambi ya upinzani kuna wapiga dili wa kisiasa (political entrepreneur) ambao wako tayari kumtumia hata fisadi kuingia Ikulu!

Kama asingekuwa Lowassa, tusingefahamu kama kuna baadhi ya wapinzani ni wanafiki na walaghai!

Lowassa ametoa fundisho ambalo vizazi vijavyo vitatumia kama benchmark katika mbio za kisiasa. Fundisho alilotoa lowassa linasema, unaweza kujiandaa kwa muda mrefu katika maisha yako kifedha na kisiasa kuwa Rais wa Tanzania na usiweze kuwa Rais wa Tanzania!

Lowassa ametueleza kivitendo kuwa, mpe mchawi mwanao akulelee! Hii ina maana kuwa, mtu ambaye anaweza kukuchafua sana kisiasa, huyo huyo anaweza pia kukusafisha sana kisiasa!

Maamuzi haya ya Lowassa lazima taifa liyaenzi kwa kizazi cha baadaye!
 
Ila kweli...
Wakati wa campaign nilikuwa nabishana na wana CDM nikiwabana wenyewe wana confess kuwa kwenye siasa kusema uongo ni normal...since then sina imani na chama chochote cha siasa...nachagua mtu ninaye muamini maana vyama havina tofauti
 
Vyama vya siasa nchini ni majanga tu.

Wanachokisema sio wanachomaanisha kivitendo.
 
Jina la Lowassa linatakiwa kuwa makumbusho ya wezi sahizi. Nani anamtajataja hii mizi sana.
Napenda pia likiwa huko makumbusho, wananchi wamuheshimu na kumuenzi kwa yale aliyoyafanya ambayo yamesababisha kuwachambua vizuri kifikra na kimatendo wanasiasa wetu na vyama vyao.
 
Maamuzi ya Edward Lowassa katika uwanja wa siasa nchini yamelitendea haki taifa letu!

Kama asingekuwa Lowassa, tusingefahamu kuwa hata kwenye kambi ya upinzani kuna wanasiasa ambao wanachokisema hawakimaanishi.

Kama asingekuwa Lowassa, tusingefahamu kama vyama vyote vya siasa nchini ni upuuzi mtupu.

Kama asingekuwa Lowassa, tusingefahamu kama hata kwenye kambi ya upinzani kuna wapiga dili wa kisiasa (political entrepreneur) ambao wako tayari kumtumia hata fisadi kuingia Ikulu.

Kama asingekuwa Lowassa, tusingefahamu kama kuna baadhi ya wapinzani ni wanafiki na walaghai.

Lowassa ametoa fundisho ambalo vizazi vijavyo vitatumia kama benchmark katika mbio za kisiasa. Fundisho alilotoa lowassa linasema, unaweza kujiandaa kwa muda mrefu katika maisha yako kifedha na kisiasa kuwa Rais wa Tanzania na usiweze kuwa Rais wa Tanzania.

Lowassa ametueleza kivitendo kuwa, mpe mchawi mwanao akulelee! Hii ina maana kuwa, mtu ambaye anaweza kukuchafua kisiasa, huyo huyo anaweza kukusafisha kisiasa.

Maamuzi haya ya Lowassa lazima taifa liyaenzi kwa kizazi cha baadaye!
Huyo mwizi ni miongozni wa vibaka walioifikisha nchi yetu mahali pabaya. Ataenziwa na kukumbukwa na wezi na mafisadi km yeye. sisi watanzania sisi tuna Rais wetu mpendwa Dr John Pombe Magufuli. full stop..!!!!!
 
MsemajiUkweli

You are the one to get a life
Kama unataka watu waachane na hoja zako ambazo hata si hoja JF unazileta as nini....?
Get a life and leave Lowassa alone.
 
Maamuzi ya Edward Lowassa katika uwanja wa siasa nchini yamelitendea haki taifa letu!

Kama asingekuwa Lowassa, tusingefahamu kuwa hata kwenye kambi ya upinzani kuna wanasiasa ambao wanachokisema hawakimaanishi.

Kama asingekuwa Lowassa, tusingefahamu kama vyama vyote vya siasa nchini ni upuuzi mtupu.

Kama asingekuwa Lowassa, tusingefahamu kama hata kwenye kambi ya upinzani kuna wapiga dili wa kisiasa (political entrepreneur) ambao wako tayari kumtumia hata fisadi kuingia Ikulu.

Kama asingekuwa Lowassa, tusingefahamu kama kuna baadhi ya wapinzani ni wanafiki na walaghai.

Lowassa ametoa fundisho ambalo vizazi vijavyo vitatumia kama benchmark katika mbio za kisiasa. Fundisho alilotoa lowassa linasema, unaweza kujiandaa kwa muda mrefu katika maisha yako kifedha na kisiasa kuwa Rais wa Tanzania na usiweze kuwa Rais wa Tanzania.

Lowassa ametueleza kivitendo kuwa, mpe mchawi mwanao akulelee! Hii ina maana kuwa, mtu ambaye anaweza kukuchafua kisiasa, huyo huyo anaweza kukusafisha kisiasa.

Maamuzi haya ya Lowassa lazima taifa liyaenzi kwa kizazi cha baadaye!
Dogo unalipwa na nani kuandika haya mashairi? Uchaguzi ulishapita bado unajitekenya na kucheka mwenyewe?
 
Bila lowassa tusingejua kuwa familia ya raisi wa awamu ya nne wauza unga,bila lowassa tusingejua state man hajui kiingerza na maswala ya kidiplomasia(gadafi raisi qa kuwait),bila lowassa tusingejua kuwa waccm wameg a wana mabilioni ya walipa kodi,kinana kalamba billion,diomond dangote bilioni,wema sepetu milioni 900 wakati huo shule hazina madawati,waalim hawajalipqa stahokizao,hospital hakuna Huduma hata ya panadol
 
Safari hii umesema ukweli uliotukuka, ni kweli bila Lowassa hata mie nisingejua Mbowe ni mnafiki na mpuuzi kiasi alichonacho.

Na bila Lowassa tungeliingiza ikulu lichama lisilofaa kushika dola.
Ndiyo maana nimesema Lowassa anastahili heshima na kuenziwa.

Maamuzi yake yametufundisha mambo mengi muhimu ya kisiasa!
 
Lowass sifa zake kwa watu ni za wizi na ufedhuli, si mambo mazuri. sasa ukianza kulazimisha watu wamkubali kwa sababu tu kanunua tena CHADEMA kwa fedha yake ya wizi, huu ni upotofu. Lowassa atakumbukwa kwa wizi tu na kuipeleka nchi yetu hapa tulipofika kwa kushirikiana na swahiba wake JK na L. Aziz.

Huwa watu wanaoelewa nani aliuza taifa letu na kusababisha JK kuyumba hatutaki kusikia kitu Lowassa. Mipango yao 2005 ndo imefikisha taifa hapa. Na aliendelea kukumbatia dhana yake ya kutumia matajiri kuendesha taifa. Sasa nashindwa kujua utetezi wako na wengine wenye maono kama yako. Lowassa atakumbukwa na wezi tu na pengine maeneo mengine kama China tusingemuona katika jamii.
Ndiyo maana nimesema Lowassa anastahili heshima na kuenziwa.

Maamuzi yake yametufundisha mambo mengi muhimu ya kisiasa!
 
Back
Top Bottom