Kaazi kwelikweli!Waandishi wa habari ni miongoni mwa watu waliotengewa fedha nyingi kwa kazi hiyo. Miongoni mwa mikakati ya awali ni kugeuza mwelekeo wa kumtengeneza Lowassa rais wa mwaka 2015 na kumsafisha kwanza kwa kutumia magazeti ya Mtanzania, Rai, The African, Tazama na huenda fedha hizo zikapenyezwa kwenye vyombo vingene.
Haya kazi kwenu wana JF- huenda tukampata Rais Lowassa, rais Rostam au Rais Msabaha miaka michache ijayo.
Tuinusuru Tanzania yetu kwa nguvu zote.
Nakubaliana na mawazo yako.Unajua wana JF tunaangalia upande mmoja wa shilingi,huyu Bw anatuhumia kwa mambo mengi sana ndani ya nchi hii,je mnajua aliyeko juu anatuhumiwa kwa mambo gani? au kwa kuwa yupo juu ndio watu wanaongopa kuongelea mazambi yake.Lowassa kama ananiya ya kugombea uraisi mwakani ni jambo zuri sana, kwa ni aliyeko juu atapata changamoto kubwa,jamani hii nchi kila mtu ni fisadi maana kizazi chote kimesha ambukiwa gonjwa hili.
Hata mimi nimesoma mwanahalisi na kuunganisha na ile thread iliyozungumzia kununuliwa hisa za channel 10.
Nimeangalia jana taarifa ya michezo ya channel 10, nimeona Mh. Lowassa akifunga mashindano ya Lowassa cup kule monduli na kupewa coverage ya dakika zisizopungua 4 hivi.
Kumbukumbu zangu zikanirudisha kwenye thread ya Mwanakijiji nikajua kweli harakati za jamaa kurudi kwenye siasa za kitaifa zimeishaanza!
Lowassa mjanja sana, naona kajiandaa chini kwa chini tu, kajiweka sawa kwenye media na sasa tarajia lolote kuanzia nyakati hizi!JK kUWA KAMA PUTIN??
Ya, ni haki yake kikatiba na nikweli pia kuwa JK ameonyesha kuwa mtawala dhaifu kabisa na mnafiki , angalia asivyotaka kuonyesha yuko wapi katika vita dhidi ya mafisadi! anataka kina Rostam waendelee kumpenda kama shoga yao wa siku nyingi huku pia kina Anne kilango waendelee kumpenda na wananchi wawe wanaendelee kudhani eti anawatuma kina Mwakyembe, Kilango, Mengi n.k
Asiwe Lowassa tu hata wengine wanaojiona wanafaa kuuondoa ubovu huu uliopo wajitokeze waziwazi .
Mimi nadhani kama kweli atagombea itakuwa habari nzuri. Maana kama atahukumiwa kwa kigezo cha ufisadi hata JK mwenyewe anatuhumiwa kuingia ikulu kwa pesa za ufisadi. Kwangu naona itakuwa habari nzuri maana yake sasa tutaanza kuona upinzani mkubwa kwa rais aliyeko madarakani na hilo litakuwa zuri kwa ukuaji wa demokrasia. Na itakuwa somo kwa CCM kuwa mtu akichaguliwa kuwa rais siyo lazima aende vipindi viwili.
Kwangu mimi natoa shime kwa Lowassa kuchukua fomu na kupiga kampeni. Kama wananchi wanakutaka watakuchagua. Lakini ukichukua fomu katika nchi utakuwa umefanya kitendo cha kijasiri cha kuthubutu kumchallenge rais aliyeko madarakani ambaye mnatoka chama kimoja.
Naanza kutafuta uraia wa nje jamani! Sidhani kama nawezavumilia kushuhudia akiapishwa!!
Too late, kishawashika pabaya! Uliza ni vyombo vingapi vya habari kishaweka mkono ndipo ujue kazi ipo, si ndogo...Ashindwe mtu huyu kwa jina la YESU aliye hai
Nakubaliana na mawazo yako.Unajua wana JF tunaangalia upande mmoja wa shilingi,huyu Bw anatuhumia kwa mambo mengi sana ndani ya nchi hii,je mnajua aliyeko juu anatuhumiwa kwa mambo gani? au kwa kuwa yupo juu ndio watu wanaongopa kuongelea mazambi yake.Lowassa kama ananiya ya kugombea uraisi mwakani ni jambo zuri sana, kwa ni aliyeko juu atapata changamoto kubwa,jamani hii nchi kila mtu ni fisadi maana kizazi chote kimesha ambukiwa gonjwa hili.
Mimi nadhani kama kweli atagombea itakuwa habari nzuri. Maana kama atahukumiwa kwa kigezo cha ufisadi hata JK mwenyewe anatuhumiwa kuingia ikulu kwa pesa za ufisadi. Kwangu naona itakuwa habari nzuri maana yake sasa tutaanza kuona upinzani mkubwa kwa rais aliyeko madarakani na hilo litakuwa zuri kwa ukuaji wa demokrasia. Na itakuwa somo kwa CCM kuwa mtu akichaguliwa kuwa rais siyo lazima aende vipindi viwili.
Kwangu mimi natoa shime kwa Lowassa kuchukua fomu na kupiga kampeni. Kama wananchi wanakutaka watakuchagua. Lakini ukichukua fomu katika nchi utakuwa umefanya kitendo cha kijasiri cha kuthubutu kumchallenge rais aliyeko madarakani ambaye mnatoka chama kimoja.
Hapana,
Mimi si fisadi na sitakuwa fisadi maishani mwangu. BWANA YESU amefanya makao moyoni mwangu.