Lowassa anasafishwa!

Ni nini kilimfanya JK kumpa Lowasa Uwaziri Mkuu pamoja na kufahamiana vizuri tangu miaka ya '70?
 
Mlalahoi, kumbuka Mbeki hakuondolewa na Bunge lake; ameondolewa na Chama chake. Hili linawezekana Tanzania.

I doubt kama hili linawezekana given mazingira ya CCM. Kwanza, sasa hivi ni vigumu kutenganisha CCM na JK. Gia yake ya kuingilia madarakani ilijumuisha na kukiteka chama chake.
Pili, ni vigumu kuamini kuwa EL na JK wamekosana kiasi cha uhasama wao kufikia hatua ya kusalitiana kiasi hicho. Waangalieni vizuri hawa, mtabaini kuwa pamoja na yote yanayosemwa, lao moja, ingawa kuna element za mambo machache ambayo hawakubaliani, lakini kimsingi, siamini kama wamefarakana kiasi hicho
 
Ana sifa kama za Zuma? Zuma alikuwa shushu tena akitoa amri unauawa sio kumwagiwa acid tu!
Kisha Zuma hajipendi kabisa uliona alivyocheza rafu na kimwana mwenye ukimwi. Mwenzetu anajipenda kama nini! Familia yake na wanae ndio Tanzania. sasa sijui kama Watananzania na vijana waliouziwa jengo lao wamo ndani kama hili watalifagilia ndugu yangu. Kazi!
 
Kwa kuwa uzuri ni kipimo cha ubaya na pepo hazina sifa ila pawapo Jehanamu.. ni naamini ukiachilia mbali masuala ya kutaka kujilundikia mali Lowasa bado namuona ni Kiongozi shupavu mwenye sifa nyingi kama sio thabiti za kuweza kuja kuwa kiongozi mzuri..

Ubaya wake waweza kuwa umepimwa kupitia uzuri wake (pengine)
 

Well, tulianzia hapa kujenga hoja hii!
 
Jamani msimkweze sana huyu Lowassa....
Hana chake tena...ndio ameshajimaliza mwenyewe.
Isitoshe ametupotezea nafasi ya uwaziri mkuu kwa watu wa kaskazini.
Kiongozi gani shupavu na hodari anayewaibia watu wake. Give me a break!
 
Jamani msimkweze sana huyu Lowassa....
Hana chake tena...ndio ameshajimaliza mwenyewe.
Isitoshe ametupotezea nafasi ya uwaziri mkuu kwa watu wa kaskazini.
Kiongozi gani shupavu na hodari anayewaibia watu wake. Give me a break!

Yaani licha kuwadhurumu watu wa Morogoro kwa kuzalisha mawaziri kwa mgongo wa viti maalumu na kuwapata Shamsa na Nkya bado mlitaka na uwaziri mkuu uwe hukohuko tena! Ninyi watu si wema kumbe, na huu tuuite nini kama si ufisadi.

Usijali Edward atarudi tena kwa nafasi hiyohiyo 2010, ila haka kamchezo ka Northern kanaiumiza nchi.
 
Tuombe Mungu. Lakini ukweli unabaki kuwa CCm lazima umalize miaka yako 10.

Lowassa hana ubavu huo na yeye anajua!
 

Japo kuwa waafrika tunafanana fanana Zuma ni Zuma na EL ni EL tu na siasa za S.A au unaweza kuita ZA ni tofauti na za Bongo mjomba! nchi zenyewe ni tofauti ikiwa wao wenzetu watahost world cup sisi hata kuhost Africa cup hatufikirii. Mkuu nakuheshimu sana na ninakufeel sana lakini kabla ya kupost jaribu sana kuangalia kitu kinaitwa ufanano wa kile unachotaka kukifananisha then ukiona ni sawa na mbingu na ardhi usipost!

Haitakuwa na wala haitawezekana Lowasa kuwa kama Zuma kwani Zuma amesafishwa na Mahakama. Swali kwako Mwanakijiji Lowasa yupo tayari kusafishwa na Mahakama?

Nangoja jibu.
 


Mramba na Yona tayari wako Lupango, kosa lao kama lile la Lowassa la MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA. Lakini mwenzao bado anadunda Monduli. Wajinga ndio waliwao!

Miaka hiyo hiyo ya misamaha hiyo ya makodi ndio kipindi ambacho Makampuni ya Madini kama Barrick yalisamehewa makodi yao kinyemela fedha tukamwagiwa kwenye uchaguzi. Hapa napo hapaguswi.

Halafu wakati huo huo ndio maEPA ya Kagoda yakachota mihela nayo ikamwagwa kwenye uchaguzi kupitia kwa Rostam.

Tukashinda kwa kishindo, na zigo lote sasa analo mzee wa NYASI

........ndiyohiyo
 
Hivi unaweza kusafisha kitu kilichooza? Bado naona kuna double-standards because of who knows who? ....and who gave who before what? Anayeshika au kukaa karibu na kitu kilichooza lazima achukue harufu mbaya kiasi chake!!!
 
Kuna uchafu mwingine unasafishika na mwingine ukiingia hata utumie chemicals za namna gani hautoki; uchafu huo usiotoka ndio aliokuwa nao Lowassa. Sasa hao wanaotaka kumkosha wanataka kumchuna ngozi? uchafu wake kama ni mwilini maana yake umeingia ndani ya damu hatima yake ni mauti tu kwa hiyo analogy yake kisiasa ni kuwa AMEKUFA na ukisha kufa huwezi kufufuka. Adios LOWASSA.
 
Last edited:
Ni kweli kwamba huyu bwana na swahiba wake Rostam hawajakata tamaa lakini historia na Mungu kwa bahati yetu nzuli haviko upande wao. Fedha walizotuibia ni nyingi na watazitumia kuwahonga wanaccm wenzao lakini umma wa watanzania umezinduka na unafahamu njama zao; kama Lowassa haamini aangalie yaliyompata fisadi mwenzie role model wake waziri mkuu wa Thailand ameishia wapi na fedha za wizi.Tafadhalini don't underestimate watanzania ukitaka kujua ishara juu ya hasira walionayo wananchi juu ya ufisadi angalia jinsi walivyowazomea Yona na Mramba pale Kisutu.
 
Najiuliza sana how come lowassa isn't being charged yet? Kuna nini?
 
Good question. Labda Takukuru haijaona kosa alilofanya. Nasikia hata faili la Karamagi lilirudishwa wakati akina Yona na Mramba wanapelekwa kisutu.
 
That is why is time to vote for opposition the only problem is hawajui kujipanga upinzani umejaa ubinafsi ubinafsi,udini na ukabila.

Bibi umekwenda mbali sana kwa Lowassa hufiki kwa Lowasa kama hujaanza na Rostam na namna Kikwete anavyooperate labda anasubiri karibu na uchaguzi who knows.
 

Tatizo sio opposition bali wapiga kura NDIVYO TULIVYO tukipewa fulana moja tu tunawapa ulaji wa miaka mitano mizima wakati fulana ukiifua mara mbili tu ndani ya mwezi inaruka hadi juu ya kitovu hapo unampa mwanao kwenda kuchungia ng'ombe huku tukiimba nambari wani ehhhhhhh!
 
Ni utaratibu tu wa kisheria huwezi ukakurupuka kumshitaki mtu bila ya kuwa na ushahidi wa kutosha
 
Wapiga kura ? fulana unachukua na kura huwapi hapo ndio wapinzani wanaposhindwa kuwaconvince wapiga kura.Tatizo viongozi wa upinzani wanaposimamisha wagombea sita kugombea Urais kama si kuwachanganya wapiga kura ni nini ?matokeo yake wanaona bora hao mafisadi wa Ccm.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…