Ni ukweli usiopingika kwamba raia wanampenda Lowassa kwa dhati ya mioyo yao. Kila kona unakopita lazima mjadala unakuwa juu ya Lowassa, ana nini huyu mzee? Ukitaka kuthibitisha hilo angalia mijadala hapa jamvini inavyopamba moto pale jina la Lowassa linavyojitokeza. Hata mana-ccm yenyewe mpaka yanasahau kumnadi mgombea wa yenyewe yanabaki kujambajamba tu humu ndani!!
Ukiangalia posts zinazowahusu watu hawa wawili (Lowassa na Magufuli) unakuta kwamba kwa Lowassa kunakuwa na watu wengi sana wanaotembelea post hiyo tofauti na ya Magufuli ambayo inakuwa na watu wachache sana. Hebu angalia posts za leo, ya Magufuli akiwa Shinyanga (uwanja wa Kambarage) na ya Lowassa akiwa Hai utaona wazi kabisa mpaka ma-ccm yamehama kwenye uzi wa yenyewe yanabaki kuchungulia kwenye post ya Lowassa. Hii inatoa picha kwamba Lowassa ndo baba lao watake wasitake, ije mvua-lije jua ukweli ndo huo!!
Nawaomba wana-UKAWA mlioko Kilimanjaro mtupie picha za kutosha mpaka haya magamba yapukutike!!!
Tukutane 25 Oktoba.