Ili uongoze lazima uogopwe kwa maamuzi thabiti yasiyoyumba bila kumuonea wala kumuonea haya mtu, namkubali Lowasa kwa hilo na nitamkumbuka daima, masiasa saisa yenu mi sipo. Hebu tujiulize au kama hujui uliza watendaji serikalini waliokutana na EL kipindi akiwa PM, uliza makatibu wakuu na wakurugenzi wa halmashauri walikuwa katika hali gani mara waliposikia Lowasa anatia timu, kama umesahau hebu vuta picha halafu pima jinsi jamaa alivyokuwa anasafiri mikoani kama popo na si kwa ajili ya kuzindua mbio za mwenge bali kwenda kujenga shule. Shule zimeshajengwa sasa tunalia zinafelisha, ni kweli na ndo kipibdi cha kutafuta walimu na vifaa, lakini la shule tayari zipo na ni za bwana EL na kimsingi mpaka kesho zitabaki kuwa kamtaji kaCCM.Ametoka sawa then kipi kinachofanyika? Naona mikoa mipya ya katavi yenye wilaya mbili itakayohitaji RC, RAS, REO, etc maDC wawili, maDAS wawili,nk, na maofisa kadhaa. Baada ya kujenga barabara safi kutoka sumbawanga kwenda mpanda unahitaji mkoa mpya wa nini? boresha teknohama shida ndogondogo mnamalizana na technologia. Wakati wenzutu wanaishi marekani wanafanya kazi china, sisi tunaishi mpanda na tunafanya kazi mkoa wa katavi. Dah mbona nchoka kabsa.