Lowassa ana bahati sana, sababu Magufuli hafai

Lowassa ana bahati sana, sababu Magufuli hafai

Lastname

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2012
Posts
921
Reaction score
297
Hata kama angegombea Lipumba angepata urais maana wananchi wameamua kubadilisha chama na sio mtu. Mgombea wa CCM kwanza hata watoto wanamuogopa kwa maamuzi yake ya kukurupuka. Kujenga barabara amejitahidi lakini huku ndiko kumemfanya asipendwe na victim wa kubomolewa nyumba, maeneo yote ya mjini mjini kuna barabara na victim wa Magufuli.

Wenye kujielewa wanasema yeye sio kiongozi kwa maamuzi yake yasiyokuwa na subira, bila JK an Pinda Jengo la tanesco na ofisi ya mkuu wa mkoa dar es salaam yasingekuwepo.

Magufuli ni miongoni mwa mawaziri wanaopenda kusifiwa katika utendaji wao Wa Kazi.


Bwana huyo amekuwa Na maamuzi ya peke yake na anachotaka yeye ndicho hicho.kwa mfano suala la kukamata meli ya Samaki , baadhi ya watendaji walimshauri lakini kama kawaida yake alikataa Na matokeo yake serikali inadaiwa fidia Na wahusika.

Kuna suala la kubomoa petrol station Mwanza, kuna suala la ugawanaji Na uuzaji Wa Nyumba za serikali hakika huu in ufisadi mkuu.

Mambo yote hayo ni kero kubwa kwa wanachi.Kama haitoshi kuna suala la ununuzi Wa boti kuukuu kwa kiasi kikubwa cha fedha za umma kiasi cha bilioni 8 boti ambayo haifanyi safari .Zote hizo in kodi za watanzania lakini zinateketea kirahisi.
 
kila mtumia bara bara mwenye gari na asiyekuwa na gari akipita barabani lazima atukane aliye simamia ujenzi wa barabara hizo inasikitisha sana ukimchukuwa mama mjamzito lazima ajifunguliye barabarani ndani ya jiji la dar es salaam mashomo kama mapango bara bara hazina mwaka au miaka 2
 
Lastname

Magufuli ni nyapara sio meneja; katu hafai kiuwa Rais na hilo ndio somo tutakaloliimba na kulirudia rudia kwenye campaign trail mpaka kielweke. Dossier yake imeshakamilika!
 
Last edited by a moderator:
Tatizo la marekebisho halitakwisha kwa sababu ccm imekuwa ikiendesha nchi bila mipango. Watu wanajenga barabarani, sehemu za wazi, mabondeni, nk huku serikali ikijisifia kuwa na mipango mji safi. Linapofika suala la miundo mbinu, usalama na maendeleo, panakuwa hakuna jinsi zaidi ya kubomoa na kuudhi watu walioachwa kujenga maisha kiholela. Sasa ukitaka uwe rafiki wa hao waliojenga kiholela, usiwa bomolee ama kuwafukuza lakini uwe adui wa public yote kwa kushindwa kuwajengea miundo mbinu sahihi ya maendeleo ambayo hitaji lake linaongezeka kulingana na ongezeko la watu, maendeleo ya technolojia na mabadiliko ya hali ya hewa na mazingira.

Kwa hili ni tatizo la Magufuli na serikali yote ya ccm ambayo haitumii wataalamu na haijali thamani ya elimu kiasi cha kuendesha nchi kwa zimamoto na kubahatisha.

Ccm yote tunaitakataa kwa kuwa hakuna aliyebora wala anayeweza kutenda jema katika mfumo wa ccm.
 
Mkuu kelele pembeni Lowassa mwenyewe afanye Kazi ya ziada kumshinda Magufuli. Mimi tangu mwanzo niliutaka sana huu mpambano.
 
Ukiangalia kwenye kura za maoni kati ya Dr. Slaa na Lowassa. Dr. Slaa alimshinda Lowasa mbali sana ila nilichojifunza ni kwamba wananchi wamechoshwa na kitu CCM tu. Wanataka mabadiriko angalau wapumzike kwa miaka kumi au mitano.
 
Hatuwataki mabepari sisi a.k.a wachumia tumbo.Magufuli ndiye raisi .
 
Pambano ni kali sana, hakuna takwimu wala mchambuzi wa kutabiri matokeo kabla. Mwisho tunaweza kumpongeza Magufuli kwa kutangazwa mshindi na Lowassa kwa kupata kura Nyingi.
 
Lastname

unataka kiongozi mpaka rangi ww? una nia ya dhat na tz au kkrpuka? all we need is a real & trustworth prsd. magufuli dd & gav all he had to tzns & tht's work hueez kuwapendeza wote. all the best jembe magufuli & all the bst fsd el. Mungu ni mwema atatujib sawsaw na htaji la watz zingine mbwbwe tu
 
Last edited by a moderator:
Hivi ni Pesa kiasi gani zinatumika kwa mwaka kulipia mahoteli kwa viongozi kwa ukosefu wa nyumba baada ya zile zilizokuwepo kugawiwa "nyumba ndogo' za wakubwa akiwepo wa waziri muhusika?
 
Lowasa vs magufuli???? Mpambano mkali km mayweather vs pacman
 
Ukipenda bwana tabu,fisadi Leo mmemgeuza shujaa.nchi hii mazuzu wengi sana.

Mageuzi ya kweli lazima yatoke CCM, kwa mtu anayeifahamu CCM, ufisadi ndani ya ccm ni wa kimfumo hauwezi kukomeshwa hata angechaguliwa kiongozi msafi kama Augustin Mrema bado angepata ugumu kuisafisha CCM.
 
Sidhani kama unajua maana ya mfumo na mmetiwa ujinga na viongozi wenu na mmeingia king.kama tatizo ni mfumo,Chadema kupata hati chafu ya cag nao ni mfumo?kama ni mfumo mnajitenga vipi na mfumo wa Chadema?pili,mbowe aliwahi kukataa gari LA serikali na badae akalichukua kimya kimya,huo ni mfumo au ni mambo binafsi?mbowe huyu aliwahi kuchukua fedha za umma na badala yake anaenda kutumbua na demu wake uarabunj.huu ni mfumo au ni mambo binafsi?Dk slaa aliwashinikiza ili agimbee urais mmhakikishie kipato chake cha ubunge,huu ni mfumo au mambo binafsi?nani anaweza kubadili mfumo wakati mfumo anaouishi na kuuamini hatimizi masharti yake?mfumo gani unaohalalisha tuhuma za lowasa na kugeuka lulu kwenu?hivi mfumo unaongozwa na mungu au binadamu?kama mfumo unajengwa na binadamu lowasa anajitenga vipi na mfumo huo alioujenga kwa miaka yote hiyo?angeshinda ndani ya chama angebadili mfumo uliomkuza na kusadiki kwa miaka yote hiyo?pelekeni upumbavu wa kufanya watu mazuzu.semeni kwamba mnataka kubinafsisha nchi na kufanya Mali ya matajiri wanaokodolea macho gesi na mafuta.wapuuzi nyie.
 
Back
Top Bottom