Lowassa ampa Apson kiasi kikubwa cha fedha Kutekeleza maazimio ya kikao cha akina Mbatia

Chabruma

JF-Expert Member
Sep 19, 2013
5,660
1,777
Wadau, amani iwe kwenu.

Jana Jumatatu Agosti 18, niliweka mada yenye kichwa cha habari mbio-za-urais-2015-mbatia-aungana-na-team-lowassa-chini-ya-uratibu-wa-apson-mwangonda. Katika taarifa hiyo, nilieleza kuwa JAMES MBATIA, BEATRICE SHELUKINDO na MOHAMED ABDULAZIZ walikutana nyumbani kwa APSON MWANG'ONDA Mbezi Beach, Dar es Salaam Jumamosi Agosti 16, 2014. Nilieleza kwamba lengo la kikao hicho lilikuwa kuendeleza kupanga mikakati ya namna ya kumwezesha EDWARD LOWASA kuwa Rais ajaye baada ya uchaguzi wa 2015.

Nilieleza kuwa walikutana nyumbani kwa APSON kwa vile yeye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya kupanga mikakati hiyo na kwamba nyumba hiyo ipo salama zaidi hasa ikizingatiwa kuwa APSON MWANG'ONDA ni Mkurugenzi Mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa na hivyo tahadhali zote za kiusalama zimezingatiwa kwenye nyumba hiyo. Aidha, nilidokeza kuwa katika kikao hicho, JAMES MBATIA amepewa jukumu la kushawishi viongozi wa vyama vikuu vya upinzani ili wawe sehemu ya mkakati huo.

Pia nilieleza kuwa JAMES MBATIA aliomba kuwezeshwa kifedha ili 'kuwapoza' wabunge wake kutokana na kukosa posho za vikao vya bunge la katiba.

Kwa hali hiyo, siku ya Jumapili Agosti 17, 2014, EDWARD LOWASA alienda nyumbani kwa APSON MWANG'ONDA na walifanya mazungumzo yaliyoanza saa 6:05 na kumalizika saa 8:10 mchana. Katika kikao hicho, APSON MWANG'ONDA alimpa mrejesho wa yale yaliyozungumzwa jana yake (siku ya Jumamosi Agosti 16). Kubwa zaidi likiwa maombi ya fedha yaliyowasilishwa na akina SHELUKINDO na MBATIA kwa lengo la kutekeleza mkakati huo.

APSON alimhakikishia EDWARD LOWASA kuwa mpango huo utatekelezeka na kwamba kuingia kwa JAMES MBATIA kwenye Kamati hiyo akiwakilisha kambi ya upinzani kutazaa matokeo chanya hasa kwa vile MBATIA ana uwezo mkubwa wa kushawishi viongozi wenzake. Pia APSON alimshauri LOWASA kutumia mvutano baina ya UKAWA na CCM kujipenyeza ndani ya UKAWA hasa ikiwa atakuwa tayari kutoa kiasi cha fedha ambacho hata hivyo hakikuweza kubainishwa.

Kuonesha kuwa EDWARD LOWASA ameridhika na taarifa aliyoipata kutoka kwa APSON, siku hiyo hiyo ya Jumapili Agosti 17, 2014, vigogo hao wawili walikutana Golden Tulip Hotel iliyopo Masaki,Dar es Salaam majira ya usiku. Baada ya kukutana ambapo walikaa moja ya vyumba mahsusi kwa wageni maalum, LOWASA alimpa APSON Kiasi Kikubwa cha fedha ambacho hata hivyo hakikubainika ni kiasi gani lakini inakadiriwa kuwa ni zaidi ya milioni 200.

Aidha, LOWASA alimhakikishia APSON kuwa yupo serious na mpango huo na alimtaka kuusimamia kwa umakini mkubwa bila ya kuumbuka.

Wadau, kwa leo naishia hapo ila nitaendelea kuwadokeza kadri itakavyokuwa inajitokeza. Pia niwaweke sawa kuwa taarifa hii si uzushi wenye lengo la kumchafua mtu fulani. Huu ni mkakati halisi unaotekelezwa kwa umakini na watu waliobobea katika kupanga na kutekeleza mikakati mikubwa yenye kugharimu kiasi kikubwa cha fedha. Aidha, taarifa hii inanisikitisha sana hasa baada ya kuona mtu mmoja anamiliki kiasi kikubwa cha fedha ambazo bila shaka zimepatikana kwa njia ya ufisadi na anazitumia kwa kutafuta madaraka huku wananchi wengi wakiteseka kutokana na kukosa huduma muhimu za kibinadamu ikiwemo matibabu.

Inauma sana tena sana. Huwa najiuliza, kwa nini madaraka yatafutwe kwa kiasi kikubwa cha fedha? Pia najiuliza, ni nani atalipa gharama hizi pindi Lowasa atakapofanikiwa kuwa Mkuu wa Nchi?

Nawasilisha
===========================

Mapesa ya Lowassa yamuibua Apson

- Ni Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa Usalama wa Taifa

- Adaiwa kupewa mamilioni kusaka urais wa Lowassa

- Avunja ukimya, asema yuko huru; kwani tatizo nini?


WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa anayetajwa kuusaka urais kwa udi na uvumba, anadaiwa kumkabidhi fungu kubwa la fedha Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Apson Mwang'onda ili kuratibu vema mikakati ya kuhakikisha anakuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyanzo kadhaa vya habari, inadaiwa kwamba Lowassa na Apson walikutana Jumapili iliyopita katika moja ya hoteli zilizoko Masaki, jijini Dar es Salaam, ambapo Apson alikabidhiwa fedha hizo.

Tukio hilo la Lowassa kukutana na Apson linatanguliwa na tukio la Jumamosi, Agosti 16 mwaka huu, siku ambayo Apson anadaiwa kufanya kikao na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, Mbunge wa Kilindi, Beatrice Shelukindo na Mohamed Abdulaziz.

Kikao hicho kinatajwa kufanyika nyumbani kwa Apson, Mbezi Beach, Dar es Salaam na walijikita zaidi kujadili namna ya kuendeleza mikakati ya kumwezesha Lowassa kuwa Rais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015.

Kwa mujibu wa habari hizo ambazo zilisambazwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii, Apson ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Mikakati ya Ushindi wa Lowassa na ili kufanikisha mipango, Mbatia anadaiwa kupewa jukumu la kushawishi viongozi wa vyama vikuu vya upinzani, vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wawe sehemu ya mkakati huo.

Madai mengine yaliyojitokeza yanamhusu Mbatia kuomba fungu la fedha kwa ajili ya kuwafidia posho wabunge wa chama chake ambao hawahudhurii Bunge Maalumu la Katiba (BMK) na kwa hiyo kukosa posho za Bunge hilo. Hata hivyo, madai haya yalikwishakanushwa na Mbatia kupitia gazeti dada na hili la Raia Mwema, linalochapishwa siku ya Jumatano, kila wiki.

Ikiwa ni mwendelezo wa kikao hicho cha awali cha Jumamosi, siku ya Jumapili (Agosti 17 mwaka huu), inadaiwa kwamba Lowassa alikwenda nyumbani kwa Apson ambako walifanya mazungumzo kuanzia saa sita mchana hadi saa nane mchana.

Katika kikao hicho cha Agosti 17, Apson alitoa muhtasari kwa Lowassa kuhusu kikao alichokiendesha Agosti 16 kilichomhusisha Mbatia, Abdulaziz (aliyepata kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga) na Beatrice Shelukindo. Ndipo kwenye muhtasari huo, aliwasilisha maombi ya kupatiwa fedha kwa ajili ya Shelukindo na Mbatia.

Inadaiwa kwamba Apson alimshauri Lowassa kutumia mvutano uliopo kati ya kundi la Ukawa na CCM ili ajipenyeze ndani ya Ukawa na namna ya kujipenyeza ni pamoja na kutoa fedha za kutosha kwa Ukawa.

Katika hali inayotafsiriwa kwamba ni kuridhika kwa Lowassa na muhtasari huo, alikutana tena na Apson siku hiyo ya Jumapili Agosti 17, 2014, katika Hoteli ya Golden Tulip kuanzia saa 12 jioni.

"Baada ya kukutana Golden Tulip walikaa moja ya vyumba mahsusi kwa wageni maalumu, Lowassa alimpatia Apson kiasi kikubwa cha fedha ambacho hakikubainika ni shilingi ngapi, japo naweza kukadiria kuwa ni zaidi ya Sh milioni 200.

"Lowassa alimhakikishia Apson kuwa yupo ‘serious' na mpango huo na alimtaka kuusimamia kwa umakini mkubwa bila ya kuumbuka," kinaeleza chanzo chetu cha habari.

Apson avunja ukimya

Alipoulizwa na Raia Tanzania, Apson Mwang'onda alijibu; "Huo ni upuuzi mtupu, wanasema Lowassa anipe pesa ili nifanye kazi yake (mkakati wa kumwingiza Ikulu), kwa lugha nyingine wanasema eti mimi nina bei... hivi mimi nanunulika... nina bei? Hizi ni siasa za kipumbavu zinazolenga tu kuchafuana.

"Na hili suala limeanzia kwenye mitandao, wameandika upuuzi huu huko kwenye mitandao, wanasema nimekutaka na Edward (Lowassa), Abdulaziz pamoja na Mbatia. Ni kweli wote hao nawafahamu lakini hapakuwa na mkutano wowote nyumbani kwangu siku hiyo (Jumamosi iliyopita).

"Yote hii ni kujaribu kumchafua Edward (Lowassa). Huu ni uongo wa kupindukia, wanasema mimi ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mikakati ni uongo, mimi sio mwenyekiti. Sitaki malumbano, kwanza hata nikiwa Mwenyekiti tatizo ni nini? Kwani hata hao wengine wanaotaka kugombea hawana wenyeviti wa kamati? Hivi (anawataja majina) hawana wenyekiti? Hivi Edward akiwa na mwenyekiti kuna tatizo gani... kuna tatizo gani kuwa na mwenyekiti? Kwa nini akifanya Edward inakuwa dhambi, wakifanya wengine inakuwa sawa?

"Nasema hata kama ningekuwa mwenyekiti wa hiyo kamati kuna tatizo gani? Namjua Edward kama ninavyowajua hao wengine wanaotaka urais," alisema.

Alipoulizwa kuhusu ukweli kwamba amekutana na Lowassa katika Hoteli ya Golden Tulip Jumapili iliyopita, Apson alisema; "Ni upuuzi mtupu. Kwa nini nikutane naye Golden Tulip? Hivi wanadhani watamzuia Edward kwa upuuzi kama huu wa kunihusisha mimi. Halafu wanamhusisha Mbatia ili tu agombane na wenzake katika Ukawa ionekane anatumika. Lengo ni kuchafua watu.

Kuhusu madai kwamba anamsaidia Lowassa kuingia Ikulu ili baadaye amteue tena kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Apson aliyestaafu wadhifa huo mapema baada ya Rais Jakaya Kikwete kuingia madarakani, alijibu; "Suala la mimi kutaka kuwa Mkurugenzi Mkuu tena ni upumbavu. Mimi nimestaafu halafu eti Rais aniteua tena! Hapo wanataka tu ionekane Lowassa kama akipita basi atafanya uteuzi kwa kuzingatia vigezo vya urafiki. Nasema ‘my time is out, I don't' kurudi. Nina heshima yangu ya kuitunza. Mimi ni mtu huru, naweza kujiunga na yeyote, huu mkakati hautawasaidia. Ni upuuzi."
attachment.php
 

Attachments

  • lowassa.jpg
    lowassa.jpg
    96.9 KB · Views: 1,771
Kuelekea 2015 tutasikia mengi ya Lowasa! Siku akimpa bintiye keki ya birthday uje umtangaze tena!
 
Mkuu Chabruma unataka kuhama CCM? Hujui hayo ni mambo ya kawaida chamani mwako? Heri ujitoe kama huwezi kuchangamana na mambo hayo

Mkuu Petro Mselewa, sidhani kama vitendo hivi vya ufisadi ni vya chama fulani. Kama James Mbatia amekuwa sehemu ya mpango huo na walengwa wakubwa ni viongozi wa vyama vikuu vya upinzani, kuna chama kitapona? Hakika Lowasa ni zaidi ya tumjuavyo
 
Chabruma naamini wewe ni reliable source kwa hiyo naamini habari hizi ni kweli endelea kuwaumbua tuone mpinzani wa kweli ni nani
 
Stress and fatigue often accompany each other. Not only does stress cause emotional exhaustion but can cause physical exhaustion as well.
 
Leo umegudua Abson Ni Mkurugenzi mstafuu, jana ulisema anaandaliwa kupewa madaraka.....
 
go go go Lowassa!!! bora lowassa Jk alipewa mahela na wauza unga ndio maana ata alivyo ingia marakana wauza madawa wamezidi kupeta na hata wanao kamatwa awa wajibishwi..


Mwanae.....
 
Unajua watu wanastahafu kwa mujibu wa sheria lakini si kwa kupenda. Bado anatamani kuwa Mkurugenzi wa Idara hiyo na anaamini Lowasa akishinda malengo yake yatatimia

Mkuu, kuna uzi uliwahi kuwekwa humu jf kuhusu APSON ukimwelezea anavyomiliki mali kama majumba ya kifahari, mashamba makubwa ya kahawa na viwanda, huo ukubwa anaoutafuta wa nini tena?
 
Chabruma asante sana kwa taarifa hii.

Hakika inaonekana ni nyeti na yenye habari zinasadikiwa kuaminika. Swali langu la msingi ni kuwa, wewe binafsi yako ulipataje hizi habari na hata kujua kiasi kabisa cha fedha alizopewa bwana Apson?

Je wewe ulikuwa mmojawapo wa wajumbe kwenye kikao hiki au mmoja wa wajumbe alikupa muhtasari wa kikao hiki?

Na kama ni kweli habari hii nini matarajio yako kwa wanaosoma?

Naperuzi tu mkuu, ntadadisi baadae ukisha paste majibu yako yatokanayo na maswali yangu.

Asante bulaza
 
go go go Lowassa!!! bora lowassa Jk alipewa mahela na wauza unga ndio maana ata alivyo ingia marakana wauza madawa wamezidi kupeta na hata wanao kamatwa awa wajibishwi..


Mwanae.....
Binafsi sikubaliani na mtu anayetafuta madaraka kwa kutoa fedha.
 
Chabruma asante sana kwa taarifa hii.
Hakika inaonekana ni nyeti na yenye habari zinasadikiwa kuaminika. Swali langu la msingi ni kuwa, wewe binafsi yako ulipataje hizi habari na hata kujua kiasi kabisa cha fedha alizopewa bwana Apson?
Je wewe ulikuwa mmojawapo wa wajumbe kwenye kikao hiki au mmoja wa wajumbe alikupa muhtasari wa kikao hiki?
Na kama ni kweli habari hii nini matarajio yako kwa wanaosoma?
Naperuzi tu mkuu, ntadadisi baadae ukisha paste majibu yako yatokanayo na maswali yangu.
Asante bulaza

Mkuu, maswali yako hayana faida. Muhimu ni hizi taarifa nilizokupa
 
Chabruma wewe uko kambi ipi? Nadhani haya ni mambo yenu ya CCM sie akina CHADEMA hayatuhusu katu, hebu MSALANI na Simiyu Yetu pamoja na Juliana Shonza njooni nataka nijue comment zenu kwenye hili maana halitoki CHADEMA HILI LATOKA KWENYE KINYWA CHA KADA NA gAMBA MWENZENU!

Hivi inawezekanaje ujue waliyoyaongea bila kujua kiasi cha fedha kilichotolewa? Maana ulisema alimhkakikishia kuwa mpango huo ni serious wakiwa chumba maalum, ulishindwaje kujua kiasi hicho cha pesa? Apson nae alikua mjinga kiasi gani au Lowasa alikua mzee kiasi gani asitamke amount hiyo? kwahio walipeana tu kama vile wanapeana bangi?

Aagghh mie mlevi tu najipitia ngoja wenye nyumba yao akina CHAMVIGA na lusungo wafike hapa tuwasikilize, Ya Ngosweeeeeeeeeeee
 
Last edited by a moderator:
Chabruma ,
whether you like it or not, by hook or by crook, edward lowasa is your next president.hutaki unaacha.ukizingatia hilo siku nyingine hutojisumbua kuandika lisred lirefu likiwa limejaa pumba tupu.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu, kuna uzi uliwahi kuwekwa humu jf kuhusu APSON ukimwelezea anavyomiliki mali kama majumba ya kifahari, mashamba makubwa ya kahawa na viwanda, huo ukubwa anaoutafuta wa nini tena?

Hakika binadamu hatosheki
 
nimeshaona comments za Hot Lady na za thatha kwa kweli nimefurahi sana maana nimeona mnavyoparurana! safi sana hongera Chabruma
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom