Lowassa amgaragaza Magufuli kwenye "media coverage"

Lowassa amgaragaza Magufuli kwenye "media coverage"

Malisa Godlisten

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2010
Posts
202
Reaction score
1,588
Zaidi ya wiki mbili sasa vyombo vyote vya habari vinaripoti kuhusu Lowassa. Radio, TV, Magazeti yote ni Lowassa. Either Magufuli kaachwa mpweke au media zinampuuza.

Magazeti hayaandiki kabisa kuhusu Magufuli. Na yakiandika yanampa nafasi hafifu sana kwenye habari za kawaida. Kwa wiki mbili sasa Magufuli hatokei kwenye ukurasa wa mbele wa gazeti, Na akitokea anawekwa kwenye "strap story" or "anchor story". Magufuli sio story ya kuuza gazeti tena.

Lakini Lowassa ambaye CCM wanadai ni "makapi" anaongoza vichwa vya habari kwa wiki mbili sasa. Magazeti yote ya Kiswahili na Kiingereza yanampa nafasi Lowassa kwny "Lead story". Yani Lowassa ni habari ya kuuzia gazeti. Leo magazeti 17 ya Kiswahili, magazeti 16 yameandika kuhusu Lowassa, gazeti la UHURU na HaBARI LEO tu yamempa Lead Story Magufuli.

Itz amazing kwamba Lowassa hata akikohoa tu NI HABARI, lakini Magufuli hata akisindikizwa na Rais kuchukua fomu SI HABARI. This is amazing fact ambayo mtaalamu yeyote wa media ameiona.

Siku Magufuli anachukua Fomu ya Urais pale NEC, siku hiyohiyo CHADEMA walifanya Mkutano mkuu na kumpitisha Lowassa kuwa mgombea Urais. Vyombo vyote vya habari vili-cocentrate kwenye mkutano mkuu wa CHADEMA. TV zikarusha Live, Radio zikatangaza siku nzima, magezeti yote kesho yake yakaandika kuhusu Mkutano mkuu wa CHADEMA.

Hakuna aliyejua kama Magufuli amechukua fomu hadi watu walipoona clip kwenye "whatsapp". Yani chombo cha habari kilichompa promo kidogo Magufuli ni TBC na "whstsapp". Hii ni aibu kwa Mgombea Urais kutegemea "whatsapp" kama media strategy yake. Ni wazi timu yake ya mikakati imeprove failure.

Baada ya Magufuli kuchukua fomu ya Urais Magazeti yaliyoandika kesho yake yote yalimpa Lowassa nafasi muhimu zaidi ktk gazeti "Lead Story" na habari ya Magufuli ikawekwa kama "Strap story".

Maana yake ni nini? Maana yake ni kuwa story za Magufuli hauziki? Hazina mvuto, haziandikiki. Gazeti lolote likiandika "Lead Story" ya Magufuli ni wazi siku hiyo mauzo yatashuka sana. Hakuna mtu ana muda wa kusoma habari za Magufuli labda JK na familia yake.

Lakini ukitaka gazeti lako liuze nakala nyingi sana weka habari za Lowassa. Ndio maana hata magazeti yanayomilikiwa na makada wa CCM kama MTANZANIA, MAJIRA, JAMBO LEO na JAMHURI yamempa coverage kubwa Lowassa kuliko Magufuli.

Hii ni dalili ya wazi kuwa Lowassa anauzika na kukubalika zaidi kuliko Magufuli. Pia ni wazi kuwa Timu ya Mikakati ya UKAWA ipo vizuri mara 100 zaidi kuliko timu ya Mikakati ya CCM.

Baadhi ya rafiki zangu ambao ni viongozi wa CCM wanakiri wazi kuwa tumewazidi mikakati. Nikiwa napiga nao story "off the record" wanakiri wazi kuwa "Tumewashika pabaya".

Huwezi kumwambia mgombea Urais akachukue fomu siku CHADEMA inafanya mkutano mkuu. Ni sawa na kutoa matangazo ya "dawa ya panya" siku ya ujio wa Obama. Unadhani kipi kitapewa coverage kubwa?
#TUTAHESHIMIANA_OCTOBER_25

Malisa GJ,
 
Magufuli kwisha habari yake mwaka huu lengo ni kutoa madarakani ccm ya ccm tutafanikiwa kwa kiasi kikubwa waliojiandaa kwa mabadiliko ni wengi sana ccm ndo kwishney mwaka huu mkienda huko msalimie Komba
 
Gazeti la Uhuru na TBC wanampa makufuli covarage yakutosha sana tu
 
Malisa, nakubaliana kabisa na your observation and media analysis kwenye suala la Lowassa vs Magufuli.

Hata itakapolazimu kufanyika kisayansi zaidi, kwa kutazama Advertising Vue Equivalence ya coverage za wote wawili for the past three months, thamani ya stories za Lowassa ni over triple the value za zile za Magufuli.

Possibly media strategy ya CCM haiko logical na realistic to suit contemporary local politics. Yawezekana waliadopt one from another country yenye mazingura tofauti kabisa na ya sasa
 
vyombo vyote isipokuwa tbcccccm,uhuruccccccm,habari leocccccccm ,cloudsccccccm,na startvccccccccm
 
nyi jidanganyeni tu na hizo promo, tar 25 october mtaanza kulialia humu ooh wametuibia kura, Magufuli hajashinda kihalali....
 
Magazet hayapigi kura!!!!" Tehtehteh

Hayapigi kura kweli but stories repeatedly issued in newspapers has a significant influence to readers choice on who to vote and who not to vote. Majority wanawajua wagombea wa vyama vyote thru media, hawajawahi kutana a nao msikitini wala kanisani, msibani ama harusini, shambani wala sokoni.

Pata picha chama kingekuja na mgombea anaitwa bazobonankira bafakulelawamba, kila mtu angejiuliza, who the hell is the dude?
 
Acha wanahabari nao wavune pesa zao Lowasa na media magufuri na watanzania hasa wapenda maendeleo bahati nzuri magazeti hayapigi kura.

kumbe na wewe una MB 125? Hujui kuwa magazeti yanatoa taarfa na habari kwa watu? Na taarfa hizo ndo znaimpact maamuzi ya wasomaji?
 
Ni ukweli jamaa anasapoti ya vijana, bila kuwa na coordination ya kutosha " Wamiliki wa TV na magazeti, pamoja na wamiliki wa makampuni ya simu" ywatafaidika na mafuriko ya Lowasa kwa kuuza kopy nyingi za magazeti na vifurushi vya Internet. Si kila mtu anaweza kuzichanga karata zake vizuri kama tunavyoona na kusikia.
 
Umiliki wa Magazeti Tanzania.

1. Nipashe, Gurdian- R Mengi ; Team Lowassa
2.Mtanzania Rai - Rostam Aziz & Lowassa
3. Tanzania Daima- Mbowe
4. The Citizen & Mwananchi - Rostam Aziz - Minority Shareholders
5. Majira - Mbuguni Close family Friends of Lowassa
6. Channel 10 - Rostam Aziz -Mmiliki wa Dowans
7. ITV-Mengi

Sioni cha kushangaa kwanini Lowassa anakuwa Front Pages kwenye vyombo vinanvyomilikiwa na yeye mwenyewe na associates wake. Hata mbio za CCM alikuwa yeye ndio Front Cover boy.

Bado ni asubuhi mno, subiri machweo. Hatutafuti mtu Maarufu tunanatafuta Rais wa Tanzania.

 
Umiliki wa Magazeti Tanzania.

1. Nipashe, Gurdian- R Mengi ; Team Lowassa
2.Mtanzania Rai - Rostam Aziz & Lowassa
3. Tanzania Daima- Mbowe
4. The Citizen & Mwananchi - Rostam Aziz - Minority Shareholders
5. Majira - Mbuguni Close family Friends of Lowassa
6. Channel 10 - Rostam Aziz -Mmiliki wa Dowans
7. ITV-Mengi

Sioni cha kushangaa kwanini Lowassa anakuwa Front Pages kwenye vyombo vinanvyomilikiwa na yeye mwenyewe na associates wake. Hata mbio za CCM alikuwa yeye ndio Front Cover boy.

Bado ni asubuhi mno, subiri machweo. Hatutafuti mtu Maarufu tunanatafuta Rais wa Tanzania.


Hiyo si sababu ya msingi kwakuwa hata ww kama ungekuwa ni mfanya biashara lazima ungeandika habari za Lowasa ili upate kuingiza mapato zaidi kwaiyo hapo ulichoandika naona hamna point ya maana
 
Back
Top Bottom