client
JF-Expert Member
- Dec 13, 2015
- 664
- 861
Waziri Mkuu wa zamani Mhe.Edward Lowassa amemgaragaza Rais John Pombe Magufuli kwenye kura ya maoni (opinion poll) iliyoendeshwa na gazeti la Raia Mwema kupitia ukurasa wake wa Tweeter. Katika kura hiyo RaiaMwema waliuliza ni mwanasiasa gani aliyekua na mvuto zaidi kwa mwaka 2016, ambapo 39% ya wapiga kura wamemtaja Lowassa, 36% wamemtaja Rais Magufuli, huku Tundu Lissu akishika nafasi ya 3 kwa 17% na January Makamba akiburuza mkia kwenye orodha hiyo kwa 08%.