Lowassa Amgaragaza Magufuli kura ya maoni

client

JF-Expert Member
Dec 13, 2015
661
846
Waziri Mkuu wa zamani Mhe.Edward Lowassa amemgaragaza Rais John Pombe Magufuli kwenye kura ya maoni (opinion poll) iliyoendeshwa na gazeti la Raia Mwema kupitia ukurasa wake wa Tweeter. Katika kura hiyo RaiaMwema waliuliza ni mwanasiasa gani aliyekua na mvuto zaidi kwa mwaka 2016, ambapo 39% ya wapiga kura wamemtaja Lowassa, 36% wamemtaja Rais Magufuli, huku Tundu Lissu akishika nafasi ya 3 kwa 17% na January Makamba akiburuza mkia kwenye orodha hiyo kwa 08%.
 
Wametoa wapi ruhusa ya kupiga kura ya maoni na Raia Mwema nani kawapa ruhusa ya kufanya hivyo..? Huu ni uchochezi..!! Na mnaanza kumjaribu Mh. Rais.. tutaligodbless Gazeti sasa hv..
 
Waziri Mkuu wa zamani Mhe.Edward Lowassa amemgaragaza Rais John Pombe Magufuli kwenye kura ya maoni (opinion poll) iliyoendeshwa na gazeti la Raia Mwema kupitia ukurasa wake wa Tweeter. Katika kura hiyo RaiaMwema waliuliza ni mwanasiasa gani aliyekua na mvuto zaidi kwa mwaka 2016, ambapo 39% ya wapiga kura wamemtaja Lowassa, 36% wamemtaja Rais Magufuli, huku Tundu Lissu akishika nafasi ya 3 kwa 17% na January Makamba akiburuza mkia kwenye orodha hiyo kwa 08%.
uchaguzi lini mkuu?
 
Mnashindanisha kijiko na sinia Lowassa ni rais wa mioyo ya watu hata waitishe uchaguzi kesho hakuna wakushindana naye
 
Kwanza hilo gazeti ni wachochezi tu, yaani Makamba naye wanamuweka kwenye list ya wanasiasa wenye mvuto? Dah! Nahisi gazeti hili utafiti wao wameshirikiana na TWAWEZA kupendekeza majina ya hao wapigiwa kura
 
Ningepata taarifa za kura kabla ya kupigwa hakika pasenti ingeongezeka.
 
Back
Top Bottom