Lowassa amezushiwa Buzwagi 31.10.07

mkama

Member
Oct 19, 2007
67
9
Je huu uchukuliwe kama msimamo rasmi wa mheshimiwa.

Mwaandishi wa makala hii ni mwandishi wake

Tanzania Daima

Saidi Nguba

KWA mara nyingine tena, gazeti la MwanaHalisi, limechapisha habari na makala kuhusu Waziri Mkuu Edward Lowassa.

Safari hii ni katika toleo Na. O68 la Jumatano Oktoba 24-30, 2007, habari ya ukurasa wa kwanza yenye kichwa: "Buzwagi: Waziri Lowassa yumo. Alikuwa London siku ya mkataba. Alilala hoteli moja na Karamagi (Waziri wa Nishati na Madini)" na makala ya Uk. 3, ingawa mwandishi aliita habari, inayosema: "Lowassa: Kioo kilichovunjika".

Habari na makala hiyo, zote hazina ushahidi wa hayo ambayo waandishi wake wanajaribu kumsingizia Waziri Mkuu Lowassa. Ni mkusanyiko tu wa tetesi na hisia zenye lengo la kutaka kumvunjia mtu heshima, kumkashifu na kumpaka matope.

Kwanza, Waziri Mkuu Lowassa hakulala hoteli moja na Waziri Karamagi. Lowassa alifika London Februari 16, 2007 akitokea Ufaransa, ambako alihudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na serikali wa Ufaransa na nchi za Afrika, ambako alitumwa na Rais Jakaya Kikwete kumwakilisha. Alipitia hapo akiwa njiani kurudi nyumbani na alilala katika Hoteli ya Four Seasons na si Churchill ambako, kama gazeti linavyosema, ndiko alikofikia Karamagi. Haikuwa siri na yeyote aliyetaka kujua taarifa sahihi za jambo hilo, angezipata tu. Habari za kudodosadodosa ambazo ni dhahiri hazikufanyiwa utafiti wa kina, ndizo zilizolifanya gazeti la MwanaHalisi kuandika kuwa Waziri Mkuu Lowassa alilala Hoteli ya Churchill.

Kwamba Waziri Mkuu Lowassa alikuwa London, basi ndiyo alishiriki katika kuukamilisha mkataba wa Buzwagi? Mkataba wa Buzwagi hauna saini ya Lowassa.

Lakini isitoshe, serikali imekwishatoa tamko ndani ya Bunge na nje, kuwa mkataba wa kuchimba madini wa Buzwagi, hauna matatizo yoyote ya msingi. Waziri Mkuu Lowassa alirudia tamko hilo katika ziara yake ya Mbeya hivi karibuni.

Badala ya kulalamika na kusingizia kuwa "Waziri Mkuu Lowassa yumo", kwanza utolewe ushahidi wa kweli basi kama "yumo", na si tu kuwa alikuwepo London.

Pili, utolewe ushahidi basi juu ya ubaya wa mkataba wa Buzwagi. Ukweli ni kwamba mkataba wa Buzwagi, kwa kulinganisha na mingine ya madini, ndiyo unaowabana zaidi wawekezaji kulipa kodi ya mapato sasa na si kusubiri kwanza kupata faida au baada ya miaka kadhaa.

Lakini vile vile kuna suala la taaluma ya uandishi. Si sahihi kumtuhumu mtu kuwa "yumo" na kuchapisha tuhuma hizo bila ya yeye mwenyewe kuulizwa ili majibu yake yachapishwe pamoja na tuhuma hizo.

Hii ni moja ya kanuni za msingi zilizomo katika maadili ya uandishi wa habari, kama yalivyotolewa na Baraza la Habari Tanzania, lililoundwa na waandishi wenyewe, na si serikali, na wenyewe kuahidi kuyatekeleza.

Katika kijitabu cha Kanuni za Maadili ya Waandishi wa Habari, kiichochapishwa na kutolewa na Baraza la Habari, mwaka 2001, sehemu 2.5 inasema: "(Mhariri) atahakikisha kwamba katika habari, maoni yanatofautishwa na matukio au ukweli halisi; kwamba ni habari za kweli tu ndizo zinachapishwa au kutangazwa na kwamba uchapishaji/utangazaji wa tetesi na hisia unapigwa vita."

Sehemu 2.8 inasema: "(Mhariri) atahakikisha pande zote za wahusika muhimu katika taarifa zinafuatwa. Pale ambapo mhusika anakataa kuongea, basi chombo kionyeshe hivyo."

Na sehemu 2.19 nayo inasema: "(Mhariri) anahakikisha kuwa umma unapatiwa habari zisizoegemea upande mmoja, zilizio sahihi na zilizokamilika."

Vilevile, sehemu 2.25 inasema: "(Mhariri) atasahihisha makosa haraka na kwa umuhimu ule ule kama wa kosa na atatoa fursa ya kuijibu."

Katika habari na makala za MwanaHalisi, zilizomtaja Waziri Mkuu Lowassa kwenye toleo Na. 068, ni dhahiri kanuni hizi zilizotungwa na wanahabari wenyewe hazikufuatwa. Kilichoelezwa kuwa habari ni tetesi na hisia, mtajwa muhimu katika habari na makala hiyo (Waziri Mkuu Lowassa) hakufuatwa kuulizwa chochote.

Habari na makala hiyo zimeegemea upande mmoja wa kutuhumu tu, bila ya kutuonyesha na kututhibitishia ukweli wenyewe!

Kwamba eti Waziri Mkuu Lowassa alifikia hoteli moja na Karamagi, ni uongo wa wazi na kwamba Waziri Mkuu Lowassa "yumo" kwenye mkataba wa Buzwagi, pia ni uongo wa wazi na hakuna ushahidi wowote kuhusu hilo.

Kama hivyo ndivyo, nini tena ilikuwa shabaha ya habari na makala hiyo katika MwanaHalisi, kama si hila za kuvunjiana heshima, kukashifiana na kupakana matope?

Uadilifu, kama ulivyoelezwa na Baraza la Habari, uhahitaji MwanaHalisi kusahihisha taarifa hizo potofu, tena kwa umuhimu ule ule kama wa kosa.

Saidi Nguba ni mwandishi wa habari wa Waziri Mkuu. Aliwahi kuwa Mhariri Mtendaji wa magazeti ya UHURU na Mzalendo na ya MWANANCHI.
 
Thank you mzee Nguba. Chapa kazi yako kwa umakini,makosa ya Tesha yalimgharimu sana Mh.Tluway
 
Ewe ndugu Nguba,

Baada ya yaliyotokea bungeni, unaweza kumtetea bado huyu jamaa yako EL?

Nina kila sababu ya kuamini alikuwepo Buzwagi......

Nashangaa wabunge wanajipendekza kwa kumpa pongezi bosi wako, ajue kwa sasa akiongea mbele ya watanzania anawakumbusha machungu mengi sana. Mizengo Pinda hawezi kulinganishwa nae.
 
Lowasa alizushiwa mambo mengi sana. Sijui kwa nini aliandamwa hivi, yaani kama Lyatonga alivyoandamwa kipindi kile.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom