Lowassa amchangia Mufti Simba 13mil

Mbunge huyo amemkabidhi Mufti fedha hizo leo akisema amezipata kutoka kwenye michango mbalimbali ya marafiki zake
 
Mwenyezi mungu amzidishie amuondolee jicho la husda na amlindde na maadui zake.
Ah fedha Bwana, wee acha tu, tutasikia dua za namna hii nyingi sana. Kumbe penye udhia penyeza rupia. Yaleyale ya fisadi mmoja wa kihindi baada ya kuona kabanwa na kashfa kibao akakimbilia "Kufadhili klabu mojawapo kubwa ili apate sympathizers ili endapo mambo yangebumburuka apate wa kumpigia debe eti anaonewa.... ni njama za klabu pinzani... Sasa tusubiri misaada ya namna hii kwa asasi za kikristo tuone kama wote hamkulainika.
 
Duh, Siasa is the game of chance, hivi hivi jamaa akipata watu wa kumsapoti kama 6 wenye utashi kwa wananchi - anapewa nchi. tutabakia midogo wazi.
 
 
Hongera Lowasa! Wewe uchagui pakutoa ata Kanisani huwa unatoa sana tu, moyo huo unao
 
Shule hiyo ilianza kujengwa mwaka 2006 na ilipewa jina hilo akiwa waziri mkuu. Tangu wakati huo wameshindwa kuimalizia na Mufti anasema walikuwa wanahijati sh 13mil tu kumalizia. Baada ya msaada huo, wataweza kuikamilisha na wanatarijia kuanza kazi mwakani!
 
Tulisemwa pamoja, tulihuzunika pamoja, tukalia pamoja na tutashinda pamoja...............
 
Mimi binafsi sina tatizo na msaada uliotolewa na Mhe. EL, hofu yangu ni jinsi fedha hizo zilivyopatikana.
Hata mimi sina tatizo na msaada wa EL wala sina hofu na jinsi zilivyopatikana ila, hofu yangu ni lengo la mtoa msaada.
 
Ni heri mwenye shibe anayemkumbuka mwenye njaa.
 
Kupokea pesa ambazo zimepatikana katika njia ambayo ni ya wizi na kila mtu anajua hilo siyo kitu cha kushangilia.Watanzania tuliowengi ili suala la kusema tunapewa misaada hata kama mtu kakuibia milioni kumi akikupa laki basi unashangilia ni baya sana na nisababu moja wapo iliyotufikisha hapa kwa kupewa t shirt na kofia sie tuna mpa kura alafu miaka mitano tuko hoi na tunalalamika.Ndio maana Pinda kasema hivi viposho ni vyakugawia watu tu.Mtu kuwa tajiri siyo dhambi ila dhambi ni pale inapojulikana kuwa utajiri wake ni dhuruma
 
Mmh Mmh ok, Fedha zote zimeandikwa '' Fedha halali kwa malipo ya shiling xx''.

Anazitakasa fedha za EPA.

hahahaha! hii nimeipenda, alishawahi kufika kijweni manzese akamuita muuza kahawa tukapiga gahawa.
 
<BR><BR>

Mh Lowasa ni mbunge - na ukwasi wa wabunge wetu tunafahamu kwamba si mdogo. Hizo pesa hata kama kazitoa peke yake hakuna la ajabu.
 
du! jamaa ndo ashaanza kugawa takrima nini kwa ajili urais 20..................................................................15
 
Waislam tuendelee hivyo hivyo wala tusilalamike siku moja na wala mtu hasije hakanyanyuwa mdomo wake kusema neno kafiki hata siku moja; na hata michango ya wauza nguruwe sasa tukusanye kupate shule za watoto wetu.
 
Kweli pesa sio mchezo, fikiria unakutana na...Rostam Aziz Catholic High School au Bin Laden Anglican Teachers College

Nafikiri hii inawezekana kwa Tanzania tu

Mkuu shida haina adabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…