Lowassa aliwapa CUF wabunge 9 bara. Je, Prof. Lipumba wangapi?

Lowassa aliwapa CUF wabunge 9 bara. Je, Prof. Lipumba wangapi?

Kura alizopata Lipumba mara zote alizo gombea urais hazifiki nusu ya alizopata Lowassa mara moja aliyogombea.
Lipumba ataishia kutumiwa na CCM kujarabu kuangamiza CUF na UKAWA hana mbele wala nyuma
Lipumba bado ana uwezo wa kutembea na kukemea ufisadi na watu tukamuelewa. Ebu piga picha dj anakemea ufisadi, sipati picha!
 
Hakuna ushindi wowote wa vyama vya upinzani uliopatikana katika chaguzi zilizopita kwa kusimama vyenyewe wala sio lowassa wala chama chochote isipokuwa ACP ambacho kinaweza kujidai kimepeta ushindi kwa kutumia nguvu zake.
 
CCM kufikia 2015 ilikuwa imechokwa sana, hao akina Bobali, Nachuma na wegine wa CUF walianza kujiimarisha majimboni mwao kabla ya uchaguzi wakiwa na Lipumba na kazi kubwa UKAWA waliifanya bila ya Lowassa na kuna majimbo mengine CCM wamehusika moja kwa moja kupitisha watu UKAWA kwa sababu aliyepitishwa na CCM alikuwa hakubaliki na wengi.
Yaan wewe ni kijana na unaamini kuwa Lowassa ameongeza udadi ya wabunge bila kuangalia factors zingine ambazo ni main mfano kuchokwa kwa CCM basi utakuwa na tatizo sehemu.
Upuuzi huo
 
KATIKA SIKU AMBAZO NIMEMDHARAU LIPUMBA, NI LEO. KATUMWA HUYU SI BURE, KIUHALISIA, UKISHINDA KAZINI MIEZI 10, WEWE UMEJIFUKUZISHA KAZI, HAKUNA MJADALA. LIPUMBA LEO ALIPOONA MASWALI YANAMBANA, AKAWA ANAKAZANA KUNYWA MAJI ILI KUPUNGUZA JOTO!
 
kwa huuu mwavuli wa kampeni manager .............
MGOMBEA URAISI DR SLAAA

Bila LOWASA waliweza zuia Bunge la KATIBA YA WANANCHI
MI HUWA NAJIULIZA, Huu mziki wa ukawa CCM wangetokea wapi 2015
KANDA YA ZIWA ...............SLAA NA JOSEFINE
KATI NA MAGHARIBI..........ZITTO NA LISU
PWANI .............................LIPUMBA
NYANDA ZA JUU..............SUGU NA MSIGWA
KASIKAZINI.....................MBOWE NA LEMA

aksante lowasa CCM watakukumbuka sana kuepusha UKAWA . Ntakuheshimu milele wewe ni bigwa na JK
 
KATIKA SIKU AMBAZO NIMEMDHARAU LIPUMBA, NI LEO. KATUMWA HUYU SI BURE, KIUHALISIA, UKISHINDA KAZINI MIEZI 10, WEWE UMEJIFUKUZISHA KAZI, HAKUNA MJADALA. LIPUMBA LEO ALIPOONA MASWALI YANAMBANA, AKAWA ANAKAZANA KUNYWA MAJI ILI KUPUNGUZA JOTO!
SHERIA YA SERIKALI AU VYAMA VYA SIASA;

WATU WANGU WANAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA
 
Kura alizopata Lipumba mara zote alizo gombea urais hazifiki nusu ya alizopata Lowassa mara moja aliyogombea.
Lipumba ataishia kutumiwa na CCM kujarabu kuangamiza CUF na UKAWA hana mbele wala nyuma
Pesa alizotumia Lipumba kwa kampeni akigombea urais haijawahi kufika hata asilimia tano yaani moja ya ishirini ya ile pesa aliyotumia Lowasa
 
CCM kufikia 2015 ilikuwa imechokwa sana, hao akina Bobali, Nachuma na wegine wa CUF walianza kujiimarisha majimboni mwao kabla ya uchaguzi wakiwa na Lipumba na kazi kubwa UKAWA waliifanya bila ya Lowassa na kuna majimbo mengine CCM wamehusika moja kwa moja kupitisha watu UKAWA kwa sababu aliyepitishwa na CCM alikuwa hakubaliki na wengi.
Yaan wewe ni kijana na unaamini kuwa Lowassa ameongeza udadi ya wabunge bila kuangalia factors zingine ambazo ni main mfano kuchokwa kwa CCM basi utakuwa na tatizo sehemu.

Ni kweli CCM ilikua imechokwa sana ;
Lakini jiulize nini maana ya Lipumba kukimbia wakati ambapo Chama chake Kingekua na uwezo wa kupata wabunge wengi na UKAWA kwa ujumla?
Juliulize Kwa nini 2010 alipoona Dr. Slaa anataka kuiangusha CCM aliamua kuzunguka misikitini na kumpigia Kikwete Kampeni?

Kwa nini tena 2015 akaamua kufanya yale yale ya kuinusuru CCM kwa kukimbia kampeni amabapo kwa pamoja wangeshirikiana Lipumba ,Lowasa ,Mbowe ,Zito Kabwe na DR. Slaa huenda nusu ya wabunge na madiwani wangekua ni wa vyama vya upinzani jambo ambalo lingekua na tija kwa nchi yetu kuliko kukimbilia urais tu wakati kwa sasa ameonekana wazi kuwa hana uweze hekma ya kuwa Rais wa nchi ya amani kama Tanzania.
Labda aende Burundi au Kongo.
Badala yake Lipumba akaamua kujiuzulu na kukimbia nchi wakati wote wa uchaguzi bila hata kuwapigia hao wabunge na madiwani wake wanaosababisha leo chama chake kiendelee kuwa chama na kupata Ruzuku.

Hebu kwa akili ndogo kabisa kabisa aliyojaliwa binadam hebu tuwaze tu kama viongozi wote kabisa wa CUF wangejiuzulu wakati wa uchaguzi kwa kumuunga mkono Lipumba ambaye alikua mwenyekiti wao leo CUF ingekuaje?
Yani kuanzia wale waliokua wanagombea ubunge na udiwani wote wangeamua kusema kuwa tunajiuzulu wote kama ishara ya kuunga mkono maamuzi ya mwenyekiti wetu, bila shaka CUF ingebaki kama CCK.
 
Lipumba hata akigombea ubunge jimbo lolote lile, hawezi kupata. Nenda kaongee na maprofesa wa pale UDSM ili ujue utendaji wa Lipumba hata alipokuwa chuoni.

Kwanza inashangaza inakuwaje mtu kama Lipumba kuwa hata Dr achilia mbali kuwa profesa. Pili Lipumba ni mwongo. Hata alipopata kazi za muda mfupi nje ya Tanzania, alikuwa akidanganya kuwa ameombwa na serikali za nchi hizo.

Pale idara ya Economics, kila mwanataaluma alifurahi kusikia Lipumba anaondoka na kwenda kushughulika na siasa. To the department and the University it was a great blessing without Lipumba.
 
Simkubali sana Lowassa lakini ni UJINGA kutumia nguvu sana kujaribu kushawishi watu kwamba lowassa alikuwa "mzigo" kwa ukawa uchaguzi uliopita, lakini ni ujinga zaidi kukataa impact ya Lowassa kwenye ongezeko la idadi ya wabunge wa Ukawa, ukweli ni kwamba Lowassa alisaidia sana kutengeneza mmeguko mkubwa Ccm ambao umeusaidia upinzani kwa kiasi kikubwa sana, hata kama kungekuwa na ukawa

Kitendo cha ccm kumuweka magufuli ambaye hakuwa na maskendo mengi automatically kulilifisha nguvu ya ukawa juu ya issue za ufisadi, sio lipumba sio Dr slaa walikuwa na nguvu na kupambana nae, Lowassa ndo ilikuwa kete pekee ya nguvu kwa ukawa, na ilikuwa kama bahati kuwepo kwake make kama angeamua kubaki ccm akaungana na akina magufuli hali ingekuwa mbaya sana uchaguzi ule kwa upande wa ukawa
 
Kitendo cha CDM kutosimamisha mgombea na badala yake kumnadi wa CUF ndiyo kimeipa CUF idadi hiyo ya wabunge.

CUF ina wafuasi kibao tu ambao ni matokeo ya juhudi za Lipumba&Co kilichokuwa kinatokea ni CDM kugawa kura za CUF Pwani na mikoa yaKusini na CCM inashinda.

Kama Mamvi Ana huo uwezo mbona haanzishi chama chake tuone matokeo?
 
Back
Top Bottom