Lowassa aliwapa CUF wabunge 9 bara. Je, Prof. Lipumba wangapi?

GALLABA

Member
Dec 19, 2016
63
119
Nimeshangazwa na msomi mahiri wa uchumi, prof.Lipumba kunena kwamba 'ilikuwa mzigo kumnadi Lowassa kwenye uchaguzi 2015' na vile vile ''aliitwa na wanachama kuja kuikomboa CUF'' naomba niweke mafanikio ya CUF chini Lipumba kama mgombea uraisi na mafanikio ya Lowassa kama mgombea uraisi

Lowassa ameweka historia kubwa ndani ya CUF, ambayo legacy ya Lipumba haifikii hata hata robo, Prof.Lipumba amekuwa mwenyekiti wa CUF kwa miaka karibia 20 tangia 1995 na amekuwa mgombea uraisi kwenye changuzi zote lakini hajawahi kuifikia rekodi ya Lowassa, CUF iliambulia wabunge wawili tu bara Wilfred Lwakatare 2000 na Frank Magoba 2000, kutokana na uongozi wake mbovu wakapoteza majimbo 2005, 2010 wakapata majimbo mawili tu, kwa kifupi chini ya uongozi wa Prof.Lipumba chama hakijawaki kupata zaidi ya wabunge wawili bara na hata kuongoza halmashauri, kimekuwa ni chama cha kupoteza majimbo

Lakini chini ya "Mzigo" Lowassa anavyosema huyu profesa Lipumba , CUF kimepata wabunge tisa na kutoa manaibu meya wawili, hivi nikisema prof.Lipumba anachanganyikiwa nitakua nakosea, hivi nikisema Prof.Lipumba amefilisika kisiasa na nitakua nakosea, huu ndo ubaya wa kutumika CCM kuvuruga upinzani

USHAURI: PROF.LIPUMBA TAFUTA CHUO CHA KUFUNDISHA ILI UENDELEE KUFANYA TAFITI ZAKO NA KULINDA HESHIMA YAKO, HOJA ZAKO DHIDI YA MAALIM SEIF NI ZA KITOTO, WANAOKUAMINI WANATAFUTA HELA YA KULA WAKINA ABDUL KAMBAYA NA GENGE LAKE
 
CCM kufikia 2015 ilikuwa imechokwa sana, hao akina Bobali, Nachuma na wegine wa CUF walianza kujiimarisha majimboni mwao kabla ya uchaguzi wakiwa na Lipumba na kazi kubwa UKAWA waliifanya bila ya Lowassa na kuna majimbo mengine CCM wamehusika moja kwa moja kupitisha watu UKAWA kwa sababu aliyepitishwa na CCM alikuwa hakubaliki na wengi.
Yaan wewe ni kijana na unaamini kuwa Lowassa ameongeza udadi ya wabunge bila kuangalia factors zingine ambazo ni main mfano kuchokwa kwa CCM basi utakuwa na tatizo sehemu.
 
Mawazo mengine ni ya kijinga sana,lowasa hajawapa Cuf hata mbunge mmoja acheni kulipa sifa zisizostahili hilo fisadi lenu,kama yeye ni bingwa wa kuwapa ubunge wagombea wa vyama vingine mbona Nccr wameambualia mbunge mmoja na NLD hawajapata hata mmoja?

Sio mawazo ya kijinga ni masuala ya facts, shida CCM mnapenda number lakini hamjui kuzisoma
 
Kwa kweli Lipumba ni muongo.
Hata Nape na Kikwete alikiri kuwa Lowasa alikua ni habari nyingine.

Lowasa hakuwa mtu wa kunadiwa bali wa kunadi.
Hata Zanzibar ambapo CCM walishindwa kuiba kura kutokana na aina ya tume iliyokuwepo kule kabla ya Jecha kufuta matokeo Lowasa alimzidi mgombea wa CCM.
Baadhi ya Watanzania mwaka 2015 hawakuwa wanataka kusikia habari yoyote ya kumhusu Lowasa zaidi ya kusubiri siku ya kura wamchague. Sasa mtu anaposema kuwa palikua na wakati mgumu wa kumnadi Lowasa anakosea.
Lowasa ni habari nyingine kabisa kisiasa kwenye siasa za Tanzania.
Uzuri wa CCM waliliona hilo wakaamua kuja na mtu wa kuweza kuleta mbinu mpya ya kampeni yaani mh. Magufuli ambaye kiukweli alitumia sayansi ya hali ya juu kujinadi na hatimaye kushinda uchaguzi.
Sasa Lipumba anataka kuwalaghai watanzania kwa siasa uchwara.
Ni bora hata CCM ivutane na CUF kuliko vurugu za vijana watiifu kwa Lipumba. Hawa wapambe wa Lipumba wakiweza kumiliki Silaha wanaweza kuwa watu hatari sana kwa amani ya Taifa letu.

Hata Mh. Rais mwenyewe anakaa kwa busara bila kutoa maneno ya kashfa kwa Lowasa kama hawa wanasiasa wa vurugu vurugu wanavyomkashfu Lowasa.
 
CCM kufikia 2015 ilikuwa imechokwa sana, hao akina Bobali, Nachuma na wegine wa CUF walianza kujiimarisha majimboni mwao kabla ya uchaguzi wakiwa na Lipumba na kazi kubwa UKAWA waliifanya bila ya Lowassa na kuna majimbo mengine CCM wamehusika moja kwa moja kupitisha watu UKAWA kwa sababu aliyepitishwa na CCM alikuwa hakubaliki na wengi.
Yaan wewe ni kijana na unaamini kuwa Lowassa ameongeza udadi ya wabunge bila kuangalia factors zingine ambazo ni main mfano kuchokwa kwa CCM basi utakuwa na tatizo sehemu.
Haahhhahhh 2010 CCM ilikuwa haijachoshwa na kauli mbiu ya maisha bora kwa kila mtanzania??? Je ilikuwaje basi CUF hawakutimia hiyo fursa zaidi wakaporomoka huku bara???
 
Kwa style hii ipo siku mtamuuliza dr slaa aliipa cdm wabunge wangapi!
Hapana mkuu huwezi linganisha uwezo wa slaa na huyo lipumba..... slaa was an asset ila lipumba alikuwa mzigo tu miaka yote chama bara hakipati wabunge haya kaondoka ndio kimefanikiwa leo hii ndio wakusema lowassa mzigo??? Tukiwa realistic cuf ingemsimamisha lipumba na chadema ingestick na lowassa nani angevuna aibu???
 
Si walibebwa na wabunge wa visiwani ila kwa takwimu za sasa CUF haijwahi fikisha wabunge 42 kma ilivyofanya sasa
Kwa hiyo wabunge wa visiwani kwa sasa wametokea chadema?

Kwa hiyo lowassa kaleta neema au balaa CUF??
 
Haahhhahhh 2010 CCM ilikuwa haijachoshwa na kauli mbiu ya maisha bora kwa kila mtanzania??? Je ilikuwaje basi CUF hawakutimia hiyo fursa zaidi wakaporomoka huku bara???
vipi kama lipumba angekuwa mgombea wa UKAWA unadhani idadi ya wabunge wa CUF ingekuwaje?
 
Vipi Nccr,lowassa kawapa wabunge wangapi? Chuki kwa lipumba isiwe chanzo cha kusingizia wabunge wameletwa na lowassa,ina maana ukawa yote ilikua ni jeshi la mtu mmoja?wengine wooteee (viongozi wa ukawa ni useless eeh!!
Hapana mkuu huwezi linganisha uwezo wa slaa na huyo lipumba..... slaa was an asset ila lipumba alikuwa mzigo tu miaka yote chama bara hakipati wabunge haya kaondoka ndio kimefanikiwa leo hii ndio wakusema lowassa mzigo??? Tukiwa realistic cuf ingemsimamisha lipumba na chadema ingestick na lowassa nani angevuna aibu???
 
Nimeshangazwa na msomi mahiri wa uchumi, prof.Lipumba kunena kwamba 'ilikuwa mzigo kumnadi Lowassa kwenye uchaguzi 2015' na vile vile ''aliitwa na wanachama kuja kuikomboa CUF'' naomba niweke mafanikio ya CUF chini Lipumba kama mgombea uraisi na mafanikio ya Lowassa kama mgombea uraisi

Lowassa ameweka historia kubwa ndani ya CUF, ambayo legacy ya Lipumba haifikii hata hata robo, Prof.Lipumba amekuwa mwenyekiti wa CUF kwa miaka karibia 20 tangia 1995 na amekuwa mgombea uraisi kwenye changuzi zote lakini hajawahi kuifikia rekodi ya Lowassa, CUF iliambulia wabunge wawili tu bara Wilfred Lwakatare 2000 na Frank Magoba 2000, kutokana na uongozi wake mbovu wakapoteza majimbo 2005, 2010 wakapata majimbo mawili tu, kwa kifupi chini ya uongozi wa Prof.Lipumba chama hakijawaki kupata zaidi ya wabunge wawili bara na hata kuongoza halmashauri, kimekuwa ni chama cha kupoteza majimbo

Lakini chini ya "Mzigo" Lowassa anavyosema huyu profesa Lipumba , CUF kimepata wabunge tisa na kutoa manaibu meya wawili, hivi nikisema prof.Lipumba anachanganyikiwa nitakua nakosea, hivi nikisema Prof.Lipumba amefilisika kisiasa na nitakua nakosea, huu ndo ubaya wa kutumika CCM kuvuruga upinzani

USHAURI: PROF.LIPUMBA TAFUTA CHUO CHA KUFUNDISHA ILI UENDELEE KUFANYA TAFITI ZAKO NA KULINDA HESHIMA YAKO, HOJA ZAKO DHIDI YA MAALIM SEIF NI ZA KITOTO, WANAOKUAMINI WANATAFUTA HELA YA KULA WAKINA ABDUL KAMBAYA NA GENGE LAKE
Akili yako mbofu sana. kura moja ya lowasa ndio ilichagua hao wabunge 9?? nonsense
 
Back
Top Bottom