Lowassa alirudisha kadi ya CCM?



sawa mkuu
 
naomba kuuliza kama lowassa alirudisha kadi ya ccm?

Ni hayo tu waungwana
 
Kwani ni lazima kurudisha kadi??.kama nafsi yake na matendo yake kwa wakati ni UKAWA hata akiwa nazo 100 za vyama tofauti haina maana.
 
Kwanini arudishe wakati aliinunua kwa pesa yake.
 
Vyama vyote vina ibara katika katiba zao, zinazowaondolea uanachama wanachama wake Mara wajiungapo na chama kingine.

Kwa hiyo awe nayo asiwe nayo yeye si mwana CCM kwa mujibu wa katiba ya CCM.
 
Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya CHADEMA ni kwamba James Mbatia yuko ndani ya ukawa kwa ahadi ya kusaidiwa kushinda jimbo la Vunjo. Makubaliano yameanzia 2010 baada ya Mbatia kupinga matokeo yaliyompa ushindi Halima Mdee jimboni Kawe. Mbowe alijua kuwa Mdee alielekea kushindwa ile kesi ndipo akamwomba Mbatia aifute baada ya kuahidiwa msaada Wa kampeni.

Kwa upande Wa Lowassa na Mbowe, wameingia mkataba Wa muda utakaokoma baada ya matokeo ya urais kutangazwa. Ni kwamba Lowassa hana mpango Wa kuwa rais na anajua hatachaguliwa. Hivyo malipo ya bilioni 12 aliyoyafanya Lowassa kwa Mbowe ni sehemu ya masharti ya makubaliano hayo. Lengo la Lowassa ni kukiyumbisha CCM kwa kukiongezea chadema majimbo na wanachama. Mkitaka kuamini niyasemayo, subirini baada ya uchaguzi Dr Slaa atarejea Chadema kuendelea na kazi, Lowassa atajitoa chadema na kubaki mwanaccm asiyetambuliwa(kadi ya ccm anayo). Msioamnini subirini haka kamchezo kahovyo kabisa kuwahi kutokea.
 
Story tu ya kijiweni, haina ushahidi wala mashiko, ukawa watamsaidiaje mbatia kushinda vunjo wakati jimbo liko TLP
 
Yaani wewe kweli kabisa uko kwenye "heat" unahitaji msaada!

Mbatia asaidiwe nini pale Vunjo wakati tayari ana msaada wa UKAWA (NLD, CHADEMA na CUF)?

Kwa taarifa yako Lowassa ni Mandela wa Tanzania. Atakuwa Rais, atatawala kipindi kimoja tu (one term) na baada ya hapo anastaafu siasa!

Ukweli unaweza kuwa huu kwa ulichokisema: Kuwaonesha CCM kuwa kila kitu kinawezekana bila/nje ya CCM na kwamba CCM inaweza kufutwa kabisa ktk uso wa Tanzania hii!

Mwisho tuwakumbushe jambo moja nyie vibaraka wa CCM na watawala wenu wadhalimu, kwamba, hakuna propaganda itakayoleta disrtotion ya dhamira ya watanzania ktk kuleta mabadiliko wakati huu!!!
 
 
Na leo utasikia mamaia ya kadi yarudishwa ...ya EL iko wapi?
 

We vipi kuna mtu anarudisha kadi ya CCM siku hizi siumeona zinavyo chomwa wakizionea huruma wanazichanachana na kuzisugua kwa miguu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…