Freddie Matuja
JF-Expert Member
- Jul 21, 2018
- 1,467
- 2,861
Ndugu zangu,
Tanzania inapita kwenye kipindi cha mpito cha mageuzi ya kiuchumi. Na wakati wa kipindi hiki kuna nyimbo nyingi sana zinaimbwa kama namna ya kutatua tatizo la ajira. Edward Lowasa aliona tatizo la ajira kama bomu linalosubiri kulipuka, Jumanne Kishimba nae hana majibu ya nini kifanyike kwa vijana wake 6 waliomaliza chuo kikuu wakati huo aki-challenge thamani ya cheti cha mhitimu wa chuo kikuu maana kama anakosa ajira, kijana hana tools za kumsaidia kuyakabili mazingira yake.
Vyuo vikuu kwa sasa vinakomaa kuja na matangazo mengi kuwa aina ya kozi mpya wanazofundisha zitawafanya vijana wapete kazi, bila ya kuwa na majibu kazi watapata wapi.
Vijana wengi wawe wa vyuo vikuu au vyuo vya kati au walio maliza la 7, form 4 au VETA wote wana something to offer kwa ajili ya kukuza uchumi wa nchi hii. Tatizo lilianza baada ya kuua viwanda na kutegemea imports ya hata toothpick, tollet paper; leo hii baadhi wanaona bodaboda kama mkombozi wakati kiafya inafahamika huwezi kuendesha boda kwa zaidi ya miaka 15 na ukawa mzima kifuani kwa aina ya mavazi wanayovaa vijana wetu.
Kishimba akauliza bungeni, kati ya vijana elfu 40 waliohudhuria usaili wa nafasi 50-70 TRA; kama wangegoma kutoka uwanjani na kukomaa na maafisa waliopo wakilazimisha kuajiriwa, kuna udhibiti gani ungetumika kutuliza hali; wengi pengine hatujui.
Katika historia ya Misri baada ya Yusuf myahudi aliewahi kuwa mkuu wa nchi kufa, akaja Farao (mtawala) ambae hakutaka kuendeleza privilege walizopewa wahayudi na ndugu yao aliekuwa sehemu ya utawala wa Misri. Utawala wa Misri kuogopa wingi wa Wayahudi waliozidi kuzaliana, wakapitisha azimio la kuwafanya watumwa. Lengo lilikuwa kuwa-keep busy na wazalisha kwa maslahi ya uchumi wa Misri. Idadi ilipozidi kuongezeka wakaja na mkakati wa kuwaua watoto wa kiume wa kiyahudi.
Leo idadi ya vijana wenye elimu ya kidato cha nne mpaka shahada ya chuo kikuu ni wengi kuliko walio kazini. Je, kama nchi kuna mkakati wa nini kifanyike walau wawe "enslaved" kama ilivyokuwa Misri ili wazalishe?
Kwa mtazamo wangu, jinsi hawa freshers wanavyozidi kuwa wengi kitaa na kuishia kwenye betting centres na kuwa busy na smartphones, sioni kama ni afya kwa usalama wa uchumi wetu na usalama wa kizazi kinachofatia baada ya hiki cha sasa, kisiasa na kijamii.
Makazini watu wanakuwa organized namna ya kufanya kazi, kuna watu kuwajibishana, kuna watu kutoka katika clerical level mpaka kufikia seniority fulani na kuongeza thamani kwenye jamii kwa mfumo wa kulea jamii ya kazini na kutoa mchango kwenye familia. Hivi kwa trend ilivyo, kama nchi, je tunawafikiria hawa vijana au tunachukulia poa tu? Natamani kitu kifanyike ile tuwe na organized system ya kuwafanya vijana wazalishe na kuwa na pattern ya kuwakuza kiakili na kimalezi.
Naomba kukiri wazi kuwa mfumo wa vikundi vya vijana kuchukua fedha za halmshauri 5% kama mikopo isiyo na riba ni mfumo wenye model mbaya na ndiyo maana hatuoni mfumo wa biashara na shughuli zao za kiuchumi wanazofanya ukitoa matunda. Mfumo kama huo huo wa vikundi, sijui nani aliuanzisha Tanzania unatumiwa na baadhi ya mabenki kama Posta, baadhi ya micro-finance na hata Benki ya kilimo nao wame-adopt model hiyo; suala la kujiuliza tumezalisha waajiri wangapi ambao kupitia vikundi hivi ambao wana staff ya walau wafanyakazi 5-15 ambao wako kwenye mifumo rasmi ya mishahara, pesheni na bima ya afya?
Naomba nikiri kumuunga mkoni JPM kwa asilimia 100. Ila ninashauri in the course of building macro-projects, pia tujenga small and medium projects ambazo ziko kwenye organized system kwa kuanzia na mahitaji ya bidhaa ambazo tuna-import ambazo raw materials zake ziko ndani na kama tuta-agiza basi finished products zifanyikie hapa ili mzunguko wa fedha ubaki ndani.
Kuna siku nilitoa mfano hapa, kuwa Bakhresa ana-import maziwa ya unga na ku-reconstitute ili apate lita laki moja kwa maziwa anayopack. Ukichanganya na maziwa anayongenezea ice cream huenda akiwa anatumia kila siku zaidi ya lita laki 1.5.
Ili kupata lita laki 1.5 tunahitaji walau ng'ombe 6,000 ambapo kila ng'ombe anatoa wastani lita 25 kwa siku; kwa kufanya hivi kama kila farm itakuwa na ng'ombe 600 maana yake ni farm 10; tutoa ajira ngapi za vijana, tutatoa huduma ya madaktari wa mifugo wangapi; tutatoa huduma ya viwanda vya kuuza madawa ya wanyama wangapi; tutatoa vyanzo vingapi vya agro-dealers?
Samaki, kila mwaka huwa tuna-import tani laki 4; walaji wapo. Mpaka zitoke China na Vietnam kweli na forex hizoo zaenda kununua samaki.
Sasa wazee wetu wa uchumi pale BOT, hazina hivi hatuwezi kufikiria namna gani ya kufanya ili tu-cut down imports. Au nyie kazi yenu ni ku-analyse na kutoa reports basi?
Ushauri wangu, it always begins with leadership. Wazungu sio wakweli kwa kutuambia wajengeeni wananchi miundombinu halafu wao watajiletea maendeleo wao weyewe. Sio wakweli hata kidogo.
Wazungu kwa kujua umuhimu wa kilimo na ufugaji kama chanzo cha raw materials za viwanda vyao wanatoa ruzuku kwa wakulima na wafugaji ili viwanda viendelee kuwa operational na ajira za viwandani ziendelee at expense ya kuwa na uhakika wa soko la ndani na kuuza excess nje ya nchi zao. Fikiria nchi kama Netherlands ni ndogo kwa size ya mkoa mmoja Tanzania. Leo hii wanauza milk products mpaka kwetu.
It begins with leadership to organize its subjects to make things happen.
Ilimhitaji Yesu kutoka mbinguni kuja kuwaokoa wanadamu kutoka dhambini. Kwanini wanadamu hawakujiokoa? It begins with leadership
Ilimhitaji Musa akomae na Farao ili kuwatoa Israel Misri, kwanini Waisrael hawakuamua kutoka Misri mmoja mmoja? It begins with leadership
Ilimhitaji Julius Nyerere kuwaondoa wakoloni Tanzania na baaada kuongoza mampambano Kusini wa Afrika; kwanini hakuacha wakomae wao wenyewe... it begins with leadership
JPM anakuwa kama mlaumiwa kwa msingi ambayo ilikiukwa tokea awamu ya pili kuanza. Hata hivyo, JKN nae alihujumiwa sana kwenye model yake ya ujamaa.
Ujamaa (Usoshalist) uliopo Israel, Slovenia, Sweden mbona kule haujafeli? Mwl alikosa watu wenye akili ya kuelewa namna bora ya kukuza ujamaa ambao ungezaa ubepari baadae bila kuua ujamaa pia.
Honestly, tunahitaji organized pattern ya ku-harness nguvu za vijana wetu na akili zao at our advantage. Otherwise wakiwa kwenye nafasi ya they have nothing to loose, 20 years later kundi hili likiwa kubwa sana, yasije yakatokea ya Tunisia, Aljeria, Sudan na Misri.
Kuna Watanzania wenye kuwa sehemu ya suluhisho tupo. Vitu vingine vinahitaji kufikiri kwa pamoja na kuamua kwa pamoja ili kutengeneza mkondo wa maji ili mafuriko ya vijana wanaokuja wa-fall in kwenye huo mkodo wa kuwa kwenye organized economic pattern ya kukuza uchumi wao ambao eventually watachangia uchumi mkubwa wa Tanzania.
Marshall Plan ilikuwa inclusive kwenye sector zote za uchumi wa Ulaya magharibi kwa kuogopa threat ya ulaya kuchukuliwa na Ukomunist wa USSR. Kuchelewa kufanya maamuzi ya haraka yalipelekea Czechoslovakia kuotwaliwa na mabeberu.
Njaa huwa sio rafiki na migomo ya njaa hata kwa wanafunzi ilikuwaga anasababisha uharibifu mkubwa sana. Tusifikie kuwa na wananchi wenye njaa wengi wakajaribiwa kuuza haki ya uzaliwa wa kwanza kama Esau. Esau angekuwa kashiba it could a different story.
Hata Yesu mjaribu alimfuata akiwa na njaa. Ukiona vijana wa Nyerere ambao aliwaamini na kuwasomesha huku na kule na wakafanyiwa vetting wakajaribiwa kwa vipande vya fedha, hali sio njema mjaribu akiwafikia vijana ambao Nyerere wakati tunamzika '99 wao walikuwa wananyonya na baadhi yao walikuwa hawajaanza kuvuta pumzi ya dunia hii.
Shalom.
Wishing you a happy furahiday