TataMadiba
JF-Expert Member
- Feb 7, 2014
- 9,868
- 5,753
Zikiwa zimebaki siku 30 kabla ya uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na Madiwni unaotarajiwa kufanyika oktoba 25 mwaka huu, Mgombea anayegombea kupitia umoja wa Katiba ya Wananchi, Edward Lowassa anadaiwa kuanza kutoa vitisho kwa baadhi ya wafanyabiashara ambao wamekuwa wakigoma kushiriki kuchangia fedha kwa ajili ya kuwezesha kampeni zake kwa kuwambia kuwa akichaguliwa kuwa rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania atawashugulikia.
Aidha amekuwa akiwaahidi wafanyabishara wanaomchangia ili kuweza kufanikisha kmpeni zake kuwapa rasilimali ya nchi ikiwamo vitalu vya gesi na Bandari.
Madai ya Lowassa kuwatisha wafanyabiashara wanaogoma kuchangia kampeni z UKAWA yanathibitishwa na Kauli ya Mwenyekiti wa CHADEMA wakati wa harambee iliyofanyika juzi katika Ukumbi wa Mlimani city kuwa kuna wafanyabiashara wanagoma kuchangia kwa kuhofia kushughuliwa na vyombo vya dola. Hata hivyo taarifa za ndani zinadai, sababu aliyoitoa Mbowe siyo ya kweli ila ukweli ni kwamba wafanyabiashara hao wamejiridhisha kuwa LOWASSA hawezi kushinda na kuchangia kampeni hizo ni sawa na kuchezea bahati nasibu.
chanzo: SAUTI HURU.