Lowassa aandaa waraka kumchanachana Kikwete kesho (Julai 20, 2015), kutimkia ng'ambo...

Status
Not open for further replies.
Hatimaye mbunge wa Monduli Edward Lowassa kesho atatoa waraka mzito utakaoelezea namna ambavyo alifanyiwa kile alichokiita 'hila' na rais Kikwete.

Waraka huo unatarajiwa kulitikisa taifa na huenda ukaigawa vibaya CCM.

Baada ya waraka huo pia Edward Lowassa anatarajiwa kutoa rasmi hatima yake kisiasa huku kila dalili ikionyesha kuwa ataisambaratisha vibaya CCM kutokana na maamuzi atakayochukua.
Porojo!!!!!!!!
 
Tatizo kubwa la hii Kambi ni maneno Mengi sana, wenzao wapo kimya kimkakati wanajipanga kwa kadiri mtavoamua. Punguzeni maneno i;i tuone matendo. Mlitupigisha Stori nyingi mwishowe Kitengo cha Jakaya na wenzake wakapiga Hatrick. Kosa kubwa mlofanya ni kupiga kura ya kumpitisha Magufuli. Kambi yenu ilikuwa na 70% ya wajumbe kama sio uroho wa Posho si mngeondoka zenu then hiyo Halmshauri kuu au Mkutano Mkuu akidi YA KUPIGA KURA isingetimia na Kikao kisingefanyika KISHERIA!

Upo sahihi mno, ktk hizi siasa, naona strategist wa CCM always huwa hawana pupa, wakisoma mchezo unavyoenda, mwisho wa siku wakifanya counter attack, wanamaliza mchezo kabisa. Hili vuguvugu la kuhamwa na waraka unaotegemewa vitapata counter response ambayo itatushangaza neutrals na wapinzani wao. Na hapo tutajua kuwa 'He who laughs last laughs longest'
 
Anamchana kikwete wakati amesha maliza muda wake? Akiulizwa alikua wapi miaka yote hii kusema atajibu nini? Mi naona kama watu ndio wanamzushia lowasa, hawezi kuwa mpumbavu kiaai hiki. Unless ametamani maisha ya kifukara.
 
Nayasuburia mafuriko kwa hamu, hakika hakuna mwanaccm hata mmoja atakayesalimika.
 
Hatimaye mbunge wa Monduli Edward Lowassa kesho atatoa waraka mzito utakaoelezea namna ambavyo alifanyiwa kile alichokiita 'hila' na rais Kikwete.

Waraka huo unatarajiwa kulitikisa taifa na huenda ukaigawa vibaya CCM.

Baada ya waraka huo pia Edward Lowassa anatarajiwa kutoa rasmi hatima yake kisiasa huku kila dalili ikionyesha kuwa ataisambaratisha vibaya CCM kutokana na maamuzi atakayochukua.

Kipindi cha "katiba" ulikuwa unatoa habari nyingi zenye kuelekea kwenye ukweli.. lakini siku hizi habari zako nyingi zina walakini.. Jaribu kubaki katika viwango ulivyoanza navyo zaidi ya hayo tutakuchukulia kama akina Laki si pesa..
 
Nafikiri huyu mzee EL anashauriwa vibaya na watu wasiomtakia mema. Ni busara kwake kuachana na siasa na Regina aendelee kumuuguza kwa amani vinginevyo atajikuta ICU na hatimaye mautini. Siasa ni mchezo hatari sana na yeye ameshapoteza uwezo wa kupambana; yeye anapaswa kulifahamu hilo!
Habari za mauti hata wewe zinakuhusu si EL peke
 
Hatimaye mbunge wa Monduli Edward Lowassa kesho atatoa waraka mzito utakaoelezea namna ambavyo alifanyiwa kile alichokiita 'hila' na rais Kikwete.

Waraka huo unatarajiwa kulitikisa taifa na huenda ukaigawa vibaya CCM.

Baada ya waraka huo pia Edward Lowassa anatarajiwa kutoa rasmi hatima yake kisiasa huku kila dalili ikionyesha kuwa ataisambaratisha vibaya CCM kutokana na maamuzi atakayochukua.

hilo litakuwa sawa na dua ya kuku halimpati mwewe
 
Lowasa hasafishiki! Sikiliza hotuba za chadema za Slaa na Lema uone je, kwa kauli zile watamuunga mkono? Kama ndivyo basi fedha fedheha!
Hata Sauli katika Biblia aliokoka na kuwa mtume Paulo sembuse Lowasa? Kama anaweka hadharani uozo wa chama chake kwa faida ya Watanzania basi atakuwa Paulo wa kizazi hiki
 
Hatimaye mbunge wa Monduli Edward Lowassa kesho atatoa waraka mzito utakaoelezea namna ambavyo alifanyiwa kile alichokiita 'hila' na rais Kikwete.

Waraka huo unatarajiwa kulitikisa taifa na huenda ukaigawa vibaya CCM.

Baada ya waraka huo pia Edward Lowassa anatarajiwa kutoa rasmi hatima yake kisiasa huku kila dalili ikionyesha kuwa ataisambaratisha vibaya CCM kutokana na maamuzi atakayochukua.
Kama yeye ni mwanaume kweli aitishe vyombo vya habari aongee live kama mwenzie Kingunge aache unafiki na uoga! Uzee una msumbua..Kama kukatwa ameshakatwa anacho fanya ni sawa na mgonjwa aliye katika hali mbaya na kapelekwa I.C.U na amekaribia kukata roho sasa ana rusha viungo vyote!
Na mshauri ajipambanue kama yeye ni baridi au moto!
 
Nafikiri huyu mzee EL anashauriwa vibaya na watu wasiomtakia mema. Ni busara kwake kuachana na siasa na Regina aendelee kumuuguza kwa amani vinginevyo atajikuta ICU na hatimaye mautini. Siasa ni mchezo hatari sana na yeye ameshapoteza uwezo wa kupambana; yeye anapaswa kulifahamu hilo!

Alishalifahamu hilo kabla hata yako na ndio maana anaendelea na mchakato wa kuwamaliza.
 
Sioni mantiki ya Lowassa kuwa furious baada ya kuukosa urais.
Je anajihisi amesalitiwa ndo maana hadi leo anataka kufanya revenge?
 
Mkuu kwa hii taarifa yako unampa Kikwete muda wa kujiandaa kujibu Waraka wa Lowassa, huwa hakawii kuzungumza na wazee wa Dar es salaam
 
ENL siku zote na falsafa yake ya maamuzi magumu ni wakati wake sasa kuutekeleza Lowasa njoo wagaragaze ccm tumechafukwa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom