Lowasa: Serikali iwawezeshe wanawake kiuchumi

ANC-KWA ZULU NATAL

JF-Expert Member
Jun 5, 2013
325
37
Mbunge wa Monduli (CCM), Edward Lowassa, amesema kuna haja kwa taifa kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa kuzingatia mchango wao mkubwa katika maendeleo na ustawi wa familia.

Lowassa aliyasema hayo juzi alipokuwa akizindua Jumuiya ya Akiba, Mikopo na Maendeleo ya Dodoma (Jamimado) katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere, mjini Dodoma.

Jamimado ni Muungano wa Vikundi vya Wanawake Wajasiriamali mkoani Dodoma, wakiwamo wafanyakazi wa ngazi za chini katika sekta za umma na wafanyabiashara wadogo.

Alisema ni lazima Serikali ithamini jitihada za wanawake hasa walioko katika vikundi vya Kuweka Akiba na Kukopa kwa kuwa wanawake wakipata nguvu za kiuchumi wanazielekeza nguvu hizo katika familia na kusababisha jamii ipige hatua za kimaendeleo.

"Nathamini sana Saccos za kinamama, maana ukimwezesha mama umemwezesha baba na watoto, yaani familia nzima, ukiwekeza kwa kinamama umewekeza mahali sahihi," alisema.

Lowassa alitoa mchango wa Sh10 milioni kama sehemu ya hamasa kwa jumuiya hiyo na kuwataka kuandaa harambee kwa lengo la kukusanya sh500 milioni.

Lowasa alisema ingawa amekuwa akihudhuria harambee, lakini hana fedha kama inavyoaminiwa na baadhi ya watu na kwamba alichonazo ni nguvu ya kushawishi watu.

"Mimi sina pesa ila nina ushawishi mkubwa kwa watu…. mkiandaa harambee, mkaniletea watu wa kutosha, mtaona nguvu na ushawishi wangu…ninawahakikishia mtazipata hizo shilingi milioni 500," alisema

 
Back
Top Bottom