Lowasa:Kihukumuni ccm kwa kutekeleza sera zake

Dr wa ukweli

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
900
264
Katika newz za chanel ten saa 1 usiku namsikia lowasa anasema wananch wakihukumu chama chao kwa kutekeleza ahadi zao vizuri na siyo siasa za chuki.
 
naye asituchanganye...juzi kasema serikali iunde tume kwa ajili ya kushughulikia suala la kupanda kwa hali ya maisha na maslahi ya wafanyakazi....leo tunaye mtu huyo huyo akisema tukihukumu chama kwa kutekeleza ahadi zake na si siasa za chuki...kazi kweli kweli!!!!
 
Hatuchanganyi anajichanganya mwenyewe. Sisi wembe ni ule ule mpaka kieleweke.Hadithi hizi za kufikirika akawasimulie wajukuu sio sisi.
 
Kuna agenda ya siri katika hili la Lowasa. Alianza na mishahara TUCTA wakamtoa nduki, mara saizi CCM ihukumiwe na kutekeleza sera zake. Ama kweli shetani akizeeka anakuwa malaika.
 
"2015" Lowasa nitoke vipi? ...... kwa wanayoikumbuka ile Bongo Flavour (Misosi).
 
duuuuu huu mshuwa kweli anataka kuchukua form ya kugombea ya urais 2015 mbona ankuja kwa kasi sanaaaaa mazeeeeeee>>>>>>>>>>>>>.
 
duuuuu huu mshuwa kweli anataka kuchukua form ya kugombea ya urais 2015 mbona ankuja kwa kasi sanaaaaa mazeeeeeee>>>>>>>>>>>>>.

Baba, hiyo ndiyo sloughing (kujivua gamba) iliyoelezwa kwenye Raia Mwema. Lakini tatizo ni kwamba hata akijivua gamba anabaki kuwa nyoka yule yule kwa tabia na vitendo vyake. Watanzania wameandika vizuri sana mateso wanayoyapata kutokana na ukatili wake yeye na washirika wake. Wanamsubiri kumlipizia kisasi 2015.
 
''Lowasa anasema wananch wakihukumu chama chao kwa kutekeleza ahadi zao vizuri''

Kwa hiyo mishahara imeshaboreshwa sio? Ugumu wa maisha umepungua?
 
Mbona low ass amekuwa vocal sana siku hizi wakati jkoiktwt amekuwa kimya kabisa?
 
CCM yenyewe ndio hii eti inatuambia mfumuko wa bei ukitokea China na Tanzania unatokea, sasa mimi nashindwa kuelewa mfumuko wa bei wa China una uhusiano gani na bei za sukari, mchele, chumvi, unga na bei za vyakula kwa ujumla? kwa maana hivi vyote tunalima hapa hapa vina uhusiano upi na mfumuko wa bei wa China?
 
Katika newz za chanel ten saa 1 usiku namsikia lowasa anasema wananch wakihukumu chama chao kwa kutekeleza ahadi zao vizuri na siyo siasa za chuki.

Lowasa umelonga, chukua form 2015 maana kiti mpaka sasa kipo wazi hao wanaokupinga ni kikundi kidogo cha watu waliojaa wivu juu yako maana wanajua ukisimama hakuna wa kukupinga.
 
Hukumu ya wananchi kwa CCM bado haijasomwa,sasa namshangaa Low ass analalamika wakati hukumu haijasomwa na wananchi wa Tanzania.
 
Sisi hatuangalii utekelezaji wa sera chafu, sera za kifisadi bali tunaangalia kwanza kama sera ni safi na zinalenga kuboresha maisha ya kila mtanzania sio kikundi cha watu wachache kama za Richmond na Dowans ambazo alizihasisi yeye na kupelekea kujiuzulu kwake, halafu ndio tunaangalia utekelezaji wake ndani ya muda uliopangwa.

Hata afanyeje, Eddo Lowasa ni fisadi tu. Atuelezee kwanza la sakata la mwanae kule London kama si la kifisadi?
 
Lowassa ukimsema,kumjadili kuwa ni mtu mwema then ukafa ghafla ndugu yangu hutoiona pepo kamwe
 
Nakihukumu hivi!!
1. Kimefanya uchumi ushuke sana na hali ya maisha ya mtanzania kuwa duni.
2. Kimepandisha sukari kutoka tsh. 750 mwaka 2005 hadi 2000 mwaka 2010
3. Kimeleta matatizo ya umeme na kuishababishia serekali hasara ya 1 trilioni kwa mwezi.
3. Ni moja ya serikali duniani ambayo haina msemaji kila mtu ni msemaji wa serikali.
4. Nauli zinapanda bila mpangilio.
5. Kashfa kubwa ya rushwa sana duniani au africa ya mabilioni ya shilingi.
6. Ni moja ya serikali ya kipekee kabisa ambayo imemficha gavana wa benki kuu kusudi asifichue maovu yao.
 
Back
Top Bottom