YEHODAYA
JF-Expert Member
- Aug 9, 2015
- 36,902
- 51,995
Akihutubia wakati wa kampeni Lowasa alikuwa akionyesha kuwa ana uchungu na maisha yaliyochoka ya watanzania na kuwa ana mikakati kabambe ya kuitoa nchi ilipo kuipeleka kwenye neema kubwa.
Kama ule uchungu bado anao na ni mzalendo wa kweli anayetaka watanzania watoke kimaisha basi tunaomba mikakati yote aliyokuwa nayo amkabidhi Magufuli tena ikiwezekana mbele ya vyombo vya habari ikiwa katika maandishi.
Ni imani yangu kuwa ule uzalendo na uchungu aliokuwa nao haukuwa tu wa majukwaani.Kwa sasa atoe msaada kwa Magufuli kwa kumpa hiyo mikakati ili aifanyie kazi.