Lowasa ashindwa kuzisoma alama za wakati......... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lowasa ashindwa kuzisoma alama za wakati.........

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Oct 30, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,964
  Likes Received: 420,622
  Trophy Points: 280
  Gazeti la Mtanzania likidhani ndiyo linamjenga JK kumbe la hasha limemnukuu Bw. Lowasa akimnadi mgombea wa CCM wa Uraisi JK kwenye kichwa cha khabari kisemacho.........."JK hana mpinzani na zamu hii atashinda kwa kishindo kikubwa zaidi....."

  Tatizo hapa ni kuwa kama mwaka 2005 JK alipata asilimia 80 inamaanisha ya kuwa Lowasa anatarajia JK kuvuka hicho kiwango jambo ambalo haliwezekani hata kidogo......

  Hivyo Lowasa amenithibitishia ya kuwa ameshindwa kuzisoma alama za wakati hata chembe na ni vyema akajikita kutetea kiti chake cha ubunge ambacho kipo kwenye hati hati ya kuporwa na mgombea ubunge wa Chadema ambaye yaelekea ndiyo chaguo la wengi hapo Monduli hata kumlazimu Bw. Lowasa kuigiza kampeni za JK za kuitumia familia yake kwa minajili ya kulinda ulaji wake hapo bungeni............
   
 2. mnyikungu

  mnyikungu JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2010
  Joined: Jul 26, 2009
  Messages: 1,447
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280
  wqataweweseka sana mwaka huu
   
 3. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,382
  Likes Received: 3,141
  Trophy Points: 280
  Lowasa yuleyule aliyetengeneza richmond (richard monduli)? Au
   
 4. K

  KunjyGroup JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2010
  Joined: Dec 7, 2009
  Messages: 352
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  I normally doubt the sanity ya Lowassa. Kweli kwa record yako Lowassa, kweli unasimama na kuomba kura? Kwa lipi umelifanya?
   
 5. MWANA WA UFALME

  MWANA WA UFALME JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2010
  Joined: Sep 10, 2010
  Messages: 578
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawa watu hawana hata aibu, wajisitiri kama mwenzao msabaha alivyokuwa kimya, nani anamzungumzia sasa?
   
 6. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #6
  Oct 30, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Nimesikiliza moja ya hotuba ya kampeni za Lowasa, nilichochukia katiba ile hotuba ni pale aliposema Kikwete ndiye pekee mwenye uwezo wa kuongea na wazungu ili tusaidiwe. Hii tabia ya kutegemea misaada hata baada ya nusu karne tangu tupate uhuru inaleta mashaka kwani rasilimali tulizo nazo ni nyingi sana. Hotuba ilinikumbusha jamaa yangu mmoja (sasa marehemu) alidiriki kumweleza mke wake wa ndoa kuwa hawara yake ndiye anawawezesha kuendelea kufurahia maisha hapa duniani, yaani mke wake wa ndoa aridhie mume wake aendelee na nyumba hiyo ndogo ili kufaidi uwezo wa kifedha wa yule mwanamke. Kama Israel sehemu kubwa ya ardhi yake in kavu lakini wanauza matunda nje ya nchi yao, kwanini viongozi wetu wanadiriki kutuambia bila misaada ya wazungu maisha yatakuwa magumu sana? Kwanini tusiumize vichwa namna ya kutumia rasilimali tulizonazo kwa maendeleo yetu sisi wenyewe?
   
 7. W

  We can JF-Expert Member

  #7
  Oct 30, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 681
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kama una hasira ni kesho. Tena LALA SASA HIVI ILI USIKU UZUIE WATU WASIRUBUNIWE. Wachakachuaji wanachakachua hata pale kwenye msatri wa kupiga kura, TAKE YOUR recording materials with you. Ukilala, utaamka mwana si wako.
   
Loading...