Lowasa anafaa sana kuiambia dunia ukweli!!!!!. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lowasa anafaa sana kuiambia dunia ukweli!!!!!.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nyakarungu, Jun 24, 2011.

 1. N

  Nyakarungu JF-Expert Member

  #1
  Jun 24, 2011
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 449
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  Katika nyakati ninazozifurahia sana kuzitazama ua kuzisikiliza, ni wakati anapoongea mtu aliyesahaulika au mtu anayesubiriwa sana na wengi ili anukuliwe kauli zake, wengi hutegemea zitakuwa na mvuto mzuri kwa namna walivyo na hamu ya sauti yake au kama ni mtu wa kunukuu vipande vya wenzake na kama ni mtaalamu wa kuzichomeka nukuu hizo kwenye hotuba yake, basi lazima hotuba yake itawavutia wengi.
  Wakati mwenyekiti akiwataja watakaochangia leo asubuhi, mimi nilikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wanasubiri kwa hamu kubwa kusikia ATAKACHOONGEA.
  Kwa hili mimi sikuwa na mucho ya kusikia sauti yake tu,bali nilitaka kumsikia ataongea maneno ya aina gani hali akijua taifa zima watayasikia maneno yake,na wakiwa wanajua kila alilolisababisha kwa makusudi ya tamaa zake au kwa kuingizwa mkenge au hata kwa kudanganya na wenzake akiwa waziri mkuu na kuliingiza taifa kaitaka aibu kubwa.
  Nilifurahi sana aliposikika akicopy style ya Rev./Dr. Martin King luther ya utoji maneno yanayochochea hisia, ama za kuwafanya watu wavutiwe nae au wapatwe na hasira dhidi ya yule anayemuongelea.( nimesema alicopy style sio maneno)

  Namnukuu.....Watanzania wanajua...na Dunia inajua..(anataja mambo anayosema ni mazuri na ya kujivunia yaliyofanywa na yanayoendelea kufanywa na ccm)
  hili neno...Dunia inajua alilitaja zaidi ya mara nne, kama kitangulinzi (presufix) kabla ya kusia jambo alilolikusudia.
  Alihutubu kwa style hiyohiyo mpaka akamaliza na kuniacha mdomo wazi, kwani kuna kitu nilitegemea atakisema kama mwendelezo wa style yake ya kila watu wanachokiita hotuba, la! hasha ile haikuwa hotuba bali ni mchango wake kwa hoja iliyokuwa mezani.

  Lowasa kama kweli anadhajua anachokiongea, kwa nini asituambie kama dunia inajua kuhusu mauaji ya raia yanayofanywa na polisi/aseme kuwa dunia inajua maisha magumu ya watanzania waishio maeneo ya uwekezaji/aseme pia dunia inajua kuwa mfumo wa uchaguzi tanzania hauko sawa/aseme dunia inajua kuwa tozo la kodi si halali na wameamua kufanya alliance ya kiwizi/aseme pia dunia inajua watanzania wamechoshwa na mfumo mbovu wa utawala tz usiozingatia vipaumbele muhimu, na badala yake nchi inaongozwa kwa kuangalia upepo wa siasa...Lowasa anauwezo wa kusema mazuri tu yanajulikana na dunia..je maovu ya serikali dunia haiajui?
  Pia Lowasa alikosesha imani na uwezo wake wa kiutendaji wanaousifia na kumfanya atamaniwe na watu kuwa mgombea wa urais 2015,
  alisema kauli inayoashiria tanzania haina uwezo binafsi, badala yake lazima iige na kufuta taratibu za nchi za magharibi.
  ''kama marekani yenyewe imeongeza deni la taifa, iweje sisi tukatae'' akimaanisha tanzania lazima iwe nyuma kwa kila jambo akipinga hoja ya wapinzani kuitaka serikali ipunguze mikopo ya nje.
  Lowasa anasahau kuwa nchi yetu ina uwezo wa kujiendesha bila mikopo ya aibu kubwa kiasi hicho, tena anasahau yeye ndiye aalikuwa wa kwanza kuionyesha dunia kuwa nchi yetu ina raslimali zasizo na wasimamazi kwa aina ya wizi aliyoufanya na kutokuchukuliwa hatua.
  Mwisho nampongeza Lowasa kwa kutufungulia njia ya kuhoji, kama Dunia inajua mabaya yote tunayotendewa na watawala.
  kweli Lowasa ni kilongola, naomba mjue kuwa usifiapo jambo uwe makini sana kwani waweza kujikuta ukielezea ubaya wake bila wewe mwenyewe kujua.
  kilichowavutia watu kwa kwa lowasa ni kwa sababu walimkosa siku nyingi na wanamuonea huruma kwa kile kinachodaiwa anaonewa na utawala wa juu wa chama chake, lakini ukiingia ndani ya senteso zake hakuna chema alichosema zaidi ya kutufanya tuanze kutafakari maisha yetu yalivyo yumba kwa kukosa uadilifu kwake...na hapa ndipo ninahoji je, dunia inajua hata haya?


  niwaage kwa kuwapa tahadhali tu tusiishi kwa namna ifuatayao;-
  "politics without principle, dreaming wealth without work, pleasure without conscince, strugling to get knowledge without character".
   
 2. F

  Froida JF-Expert Member

  #2
  Jun 24, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,903
  Likes Received: 1,330
  Trophy Points: 280
  Hakua na la kusema ila alikuwa anapiga vijembe serikali yake kasema waazi bila kumung'unya maneno kasema lazima wawe na maamuzi magumu kwa maana ya kufanya mipango inayotekelezeka ,kaonyesha wazi uzaifi wa Jakaya na Pinda katika uendeshaji wa serikali,mengine yalikuwa ni ngonjera tuu za kuwasuta watu na hili linaonyesha ni kwa jinsi gani ambavyo hawezi kuvuliwa gamba si umeona wabunge wa CCM wamememgia makofi zaidi ya dakika mbili na yeye akiinama kwa heshima ha ha ha ha sinema ya lowassa na Jakaya imekolea kweli ngoja tungojee tuone reaction ya NNauye Juniour
   
 3. n

  never JF-Expert Member

  #3
  Jun 24, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 234
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Sijui ulikuwa wapi swahiba maana Lowassa leo kajadiliwa humu nikadhani umekuja na jipya kumbe yale yale. Then jana uliishambulia JF kule FB kwa watoto vinuka mikojo kwenye group ya JAMII FORUM swahiba wako au niseme mwanachama wa chama chako akakutaka ubadlishe kauli ya kuiponda JF ila hukufanya hivyo sasa leo unakushangaa umetufuata huku.. NANUKUU msiwe kama mashabili wa JF mwisho wa kunukuu sasa umefuata nini humu? MODS huu mtu hatufai humu aniponda hii forum na kudhalilisha member wote waliyopo humu na kuwafananisha na wale wauza sura wenzake kule plz MODS ondoeni hiki kiumbe humu kabla sijakasirika
   
 4. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #4
  Jun 24, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Havuliki gamba mtu mwaka huu!!
   
 5. M

  Marytina JF-Expert Member

  #5
  Jun 24, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,034
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  move on Lowassa!!!
  lowassa for ccm 2015
  waliobaki wote ccm wavivu wa bora wewe hata kama unakashfa
   
 6. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #6
  Jun 24, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  bora Mpemba agombee Urais 2015 kuliko huyu fisadi Lowasa. Lowasa, Kikwete, Rostam wote lao moja.
   
 7. e

  ebrah JF-Expert Member

  #7
  Jun 24, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 397
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  shame on him!
   
 8. N

  Nyakarungu JF-Expert Member

  #8
  Jun 24, 2011
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 449
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45

  watu wa aina yako, wenye ghiriba za majungu, wenye fitina za kinafki na wenye kushindwa kuandika kizatiti kama wao, wanaodandia na kutafuta upenyo wa kuongea umbea na mipasho kama wewe, ndio ninaowaita washabiki kilewo, tena hofu imekujaa na ndio maana unajificha kwa jina la kichina, naandika kile ninachokijua ninachoweza kukitetea na ninajiamini ninuwezo huo.
  wewe ni member kama mimi tena wewe ni member muoga mnafiki mweneza chuki, ndio maana unaniattach mimi na huwezi kujibu hoja, au kama wewe upo kwa kumlinda lowasa umtetee kwa hoja sio kwa fitina zako za kujuha, je, unahodhi nini ndani ya jf mpaka umwamuru mods aniondoe, chunga sana kilewo, take care.
   
Loading...