Love story: Utamu mpaka basi

brightmind

Member
Dec 24, 2018
70
102
Shebby si mwanangu kiviile sema anahusika sana kunipa mapande mbalimbali. Mchizi wangu kibonge Suddy ndo zinapanda sana japokokuwa hana mchongo wa maana hapa town. Huwezi amini majuzi kati nmechill zangu gheto mara mwamba Shebby huyu hapa, halafu yuko na pisi mbili kali kishenzi.

“Oya kamanda vipi?”
“Kama dawa mzee” Nilimjibu huku nikiwacheki wale maduu.
“Kaka mambooo!” wale dadaz walinisalimia na visauti vya kuibia waume za watu.

“Ni fresh, karibuni” nilitia tabasamu ya kimwamba. Si unajua maisha yetu ni kukaza kila kitu.
“Kwani una maniaje unafanya sasaivi?” Shebby aliniuliza, nikajua mwamba tayari anataka nipa connection la nguvu.
“Hapana dingi, nilikuwa nina mishe fulani nataka kuifanya sema ntaipiga mida, vipi kwani?”

“Jiongeze basi fundi, twenzetu DADAZ PUB kama upo free”
“Poa bingwa dakika sifuri”. Nilizama chumbani nkawaacha Shebby na wale warembo wamekaa kwenye sofa sebuleni. Maana nilikuwa nimeweka zangu kigongo kimoja kikali sana cha kituruki kinaitwa war of sex. Huwa kama sina mishe ya kufanya napoteza muda kwa namna hiyo.

Natupia jacket langu maana jioni hapa Moshi ni baridi kinyama, nakula buti la mgambo, kepu na kadeti fulani nzito. Ofcoz nishajua Shebby anahitaji kampani maana pisi zilikuwa mbili na sikujua Shebby anasimamia ipi. Nikajipanga fresh kivita, sikuwaza gharama za Pub maana Shebby mfukoni huwa mambo safi.

“Mali safi sana hizi, hasa hii yenye kibebifesi” akili ilikuwa inazungumza yenyewe.

Chapu natoka zangu, tunaingia kwenye Vanguard ya mzee baba Shebby, hatuhesabu hata dakika tunaingia DADAZ. Ni mapema sana, mida ya saa moja na kitu hivi. Tumeshuka zetu tukaingia kona moja hivi mafichoni, kulikuwa na meza na viti vitano. Basi tukala pozi pale wakati naendelea kuusoma mchezo.

“Yupi atakuwa wa kwangu hapa?” bado maswali hayakukauka.
Anakuja mhudumu pale, naye mali poa si mchezo.
“Karibuni, niwahudumie nini”
“Tupe kitimoto kilo moja na nusu na ndizi. Halafu leta bapa mbili kubwa. Oyaa! Mwambieni mnatumia vinywaji gani”. Basi mhudumu akachukua oda na kusepa.

“Kelly, hebu njoo mara moja. Warembo tunakuja” Basi Shebby akanichomoa pale na tukaenda pembeni, bila shaka ilikuwa nipate ABC.

“Sa skia, yule demu mwenye alovaa kimini cha pinki na lips nene ndo atakuwa chakula changu. We pambana na huyo kibebifesi, anajua kaja kufanyaje maana niliongoea na huyu bi malips akanambia atakuja na rafiki yake hivyo nikamwambia pia ntakuwa na mshikaji wangu sio mbaya.
“Anaitwa nani?

“Aah acha kunifelisha, hayo maswali si utamwuliza” Basi, mimi na Shebby tukarudi zetu kukaa. Tayari maji yalikuwa yashawekwa mezani pale tukiwa tunasubiri nyama.

Shebby akaendelea kubonga na bibie wake huku wakishikana hapa na kule. Na mimi nikaona nisicheze faulo.
“Mambo vipi mrembo”
“Safi tu, vipi wewe”
“Ni poa sana” Basi tukaendelea kupiga stori, kupiga maji na tukala. Pub ilikuwa imechangamka sana kwa sababu ni wikendi. Kucheki taimu ngoma inasoma saa saba. Mademu wamelewa, wanafanya mambo ya ajabu tu. Mara wacheze, mara waongee utumbo fulani hivi. Nikamtonya Shebby inatosha. Nilikuwa nishampanga kibebifesi hivyo ratiba nzima ilikuwa inaeleweka. Ninachompendea Shebby michongo yake ni uhakika.

“Nafikiri kila mtu kainjoy, twenzetuni. Kelly ntakudondosha pale kwako na bibie. Nitakuja saa tatu kumchukua”.
“Fresh mwamba”.
Ujue mi si mchizi yule ana good life ila kuna tuvitu fulani muhimu kigetogeto tumetulia. Shwaa! Tunachomoka Pub baada ya Shebby kulipa bills na ananiacha kwangu na mrembo. Kwani ana nguvu hata za kutembea? Kalegea kama kuku wa kideli.

“Asubuhi tuwasiliane” Shebby aliniaga.
“Poa bingwa”. Basi nikamsaidia kuingia ndani Kibebifesi nikiwa nimemshika kiuno naye mkono wa kushoto kaupitisha begani mwangu.

Niliona nikimkalisha kwenye sofa atasinzia hapo, ikabidi nimbebe mpaka chumbani, nikamvulisha viatu na kumlaza kwenye sita kwa sita au paite machinjioni.

ITAENDELEA...
 

Igombe fisherman

JF-Expert Member
Apr 28, 2017
1,682
2,850
Hebu tulianze picha letu huku tukiandama na ma introduction. Sheby ndo stering kwenye hili sinema

Alaah
Tutampata kibonge ndani ya hili simulizi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Top Bottom