Love story-3

Manun'guniko

Senior Member
Jul 23, 2014
155
59
LOVE STORY-3

Baada ya miriamu kusikia vile kutoka kwa mama wa Brayan alikimbia na kutoka nje ya nyumba Brayan alimkimbilia na alipotoka nje alimkuta analia alijaribu kumbembeleza lkn miriamu alilia sana huku akiongea kuwa mimi maskin ndo natengwa hivyo?

Mimi mwenyewe sikupenda nilitamani niwe na elimu nzur na maisha mazur pia lkn nitafanyeje wazaz wangu ni masikin lazima nikubaliane na hilo Brayan alijikuta machozi yanamtoka kwa jinsi mpenzi wake alivyokuwa analia kwa masikitiko makubwa alijaribu kubembeleza lkn miriamu alimwambia naomba unipeleke nyumbani sijisikii vizur furaha yangu imeyeyuka kama barafu.

Brayan alimpeleka nyumbani alipomfikisha akamwambia kwa vyovyote vile mpenzi wangu naomba tupiganie penzi letu najua unanipenda na mimi pia nakupenda tusiache nafas ya mtu yoyote kulivunja penzi hili nakupenda akambusu busu la shavuni alafu akaondoka miriamu akabaki analia kwa muda kisha akaingia ndani akakutana na nyuso za furaha za wazaz ambao walikuwa na shauku la kujua nini kimetokea.

Lakini furaha yao ilikatishwa baada ya kumuona miriamu akiwa mwenye uchungu na uso uliojaa machozi walimkalibia na wakamuuliza kwa upole nini kilichotokea mwanetu miriamu alizidisha kulia badala ya kuwasimulia aliwakumbatia kwa huzuni.

Baada ya Brayan kufika nyumbani alikuwa na hasira na alifika moja kwa moja bustanini ambako wazazi wake walikuwa wamekaa akaanza kuongea huku akilia mama kwa nini umemfanyia vile mpenzi wangu ni msichana ambae nimemchagua mwenyewe na ninampenda she is poor but she deserves happiness.

Baba yake akamkatisha na kumwambia mama yako alichokifanya ni kitu kizur msichana gani unatuletea wasichana wote wasomi ina maana ujakutana na hata mmoja mpaka ukamchague msichana ambae hana mbele wala nyuma umetuangusha sana mwanangu sitokubaliana na hilo labda nitoweke duniani.

....brayan alichanganyikiwa ashindwe afanye nini ukizingatia anampenda sana miriamu lakin pia wazaz wameleta shida pia....baada ya moyo kutulia miriamu aliweza kuwaeleza wazazi wake yale yote mama yake alimshauri akamwambia jambo la muhimu mnapendana usitake kuachana na brayan kisa wazazi naamin ipo siku wataelewa na watawakubalieni

maneno ya mama yake yalimpa moyo miriamu na pale brayan alipokuja kumtembelea alimwambia nipo tayari kupigania penzi letu hadi nione mwisho wake.....baada ya wazaz wa brayan kumshawishi aachane na miriamu kugonga mwamba waamua kumpigia simu Patricia aje nchini

msichana ambae anampenda brayan kwa siku nyingi makazi yake ni nchini Canada ambako ndiko brayan na wazaz wake walikuwa wanaishi na ndio kisa cha brayan kuama canada nakuja nchini kwa lengo la kumuacha patricia kwa sababu hakuwa anampenda,

simu ile inafufua tumaini jipya kwa patricia na kumfanya awe na furaha kwamba anakuja nchin kwake na pia anakuwa karibu na mwanaume ampendae anawahaidi wazazi wa brayan kwamba siku yoyote anaweza kuwa nchini kufanya mapinduzi,

wazazi wa brayan wanaamin hiyo ndio njia kuu inayoweza kusambaratisha penz la brayan na miriamu kwa sababu walijua ni kiasi gani patricia anampenda brayan, na kipindi brayan anakuja nchini patricia alitamani kumfuata lkn masomo yalimbana sasa furaha yake amemaliza chuo na anarudi nchini kwake na pia anakuja kulipigania penzi la mwanaume ampendae...."usikose next episode bye"
 
Imetokea wapi hii, tunaomba sehemu ya I na ya II kwanza, ili twende vizuri
 
Back
Top Bottom