The magic ring
Mtunzi:tawfiq abdallah
Contacts:0712581515 & 0686565050
Email:tawfiqabdallah24@gmail.com
Sehemu ya kwanza
Upepo mkali ulioambatana na radi huku rangi ya mawingu ikizidi kuwa nyeusi . muwako na muungurumo mkali unasababisha maporomoko ya mawe yatokayo mlimani na kudondoka kwa kasi chini yalizidi kutetemesha mlima huo.
Juu ya mlima huo kulikua na viumbe wawili waliokua wakirumbana na kutoleana maneno kwa ukali. Ilisikika sauti ya kike na kiume huku kila mmoja wao akiwa hataki kuwa chini ya mwenzake. Marumbano hayo yaliishia baada ya msichana kutoa pete yake na kumrushia mwanaume ambaye hakuijali zaidi aliiacha tu hiyo pete ianze kubiringita kwa kasi kuelekea chini ya mlima.
Baada ya tukio hilo, Yule mvulana alibadilika na kua kama popo mkubwa na kupaa angani kwa kasi. Haikuchukua muda mrefu, na Yule msichana alibadilika na kuwa jamii hiyo hiyo ya popo mkubwa na kupaa angani kwa kuelekea upande wake.
Utengano huo wa majini waliokua wapenzi kwa muda mrefu na wakiwa katika hatua za mwisho kufunga ndoa,ulikua gumzo kwa jamii yote ya majini aina yao.
Hiyo ilikua na mara ya kwanza kutokea katika historia za majini ambao daima hua waaminifu na hua hawaachani mpaka kifo kinapo watenganisha.-Taarifa za ugomvi huo zilifika kwa mkuu wa majini na kuwaita kwa ajili ya usuluhishi, ila jini la kiume liligoma kuripoti hivyo zoezi hilo likafeli.
Uzito wa mahaba ya jini la kiume ulianza kuonekana baada ya kutengana kwa muda wa wiki moja tu. Jini la kike lilishindwa kula wala kupata usingizi mzuri. Alishindwa hata kuyafurahia maisha japokua alikua na uwezo wa kutembea ardhini na kupaa angani pasipo mipaka. Mateso ya moyo yaliyo muonyesha udhaifu wake juu ya mwanaume huyo aliyeziteka hisia zake, ndizo zilizomshawishi awe mpole na kukubali makosa yake.
***********************************
Baada ya jogoo la kwanza kuwika, niliamka huku nikifungua dirisha ili kuhakikisha kama kweli kulikua kumekucha. Niliindea ndoo yangu ya maji na kukuta imebaki nusu ndoo kutokana na kuoga nusu ya maji yaliyokua humo kwenye hiyo ndoo jana yake usiku nilipokua nimerudi kutoka kwenye mahangaiko yangu.
Muwako wa simu yangu ambayo mlio wake ulikua mdogo sana, ndio ulionifanya niichukue haraka na kuangalia kibox kilichoashiria kua message ilikua imeingia. Kabla sijaifungua hiyo sms, mtu aliyenitumia hiyo sms alinipigia simu.-Nilipokea haraka sana kwakua siku zote huyo mtu hua hanipigii simu kama hakuna dili ya maana ambayo tunaweza kufanya.
uko wapi we boya. Alinisalimia salamu ambayo haikuniumiza. Japokua kama mtu mwengine akiniita hivyo naweza kugombana nae kama si kushikana nae kutokana na kutolipenda jina hilo.
nipo geto joh niliitikia huku kidole changu nikikielekeza sehemu iliyoandikwa LOUD ili mradi niweze kumsikia kutokana na udogo wa sauti ya simu yangu.
njoo Tabata bima muda huu
kuna mzigo tunatakiwa tuupeleke Morogoro. Aliongea na kunifanya niitikie haraka bila kuuliza ni mzigo gani huo.
sawa mkuu. Niliitikia na kuchukua shati langu na kuanza kuvaa haraka huku simu nikiwa nimeishikilia mkononi.-chukua boda boda , hela yake nitampa huku huku. Aliniambia hivyo ili nijue ni jinsi gani alivyokua na haraka.
nimekuelewa mkuu. Nilijibu hayo maneno na simu yangu ikakatika.
Nilighairi kuoga, nilivaa suruali yangu haraka na kuufunga mlango wa chumba changu na haraka nikawahi kituoni ambapo nilichukua pikipiki fasta na kumuelekeza ni wapi ambapo tunatakiwa twende.
Baada ya kufika, hakukua na story zaidi ya kuingia kwenye gari kubwa lililokua na shehena ya mzigo ambao hata mimi sikua naujua wa nini na wala sikutamani kuhoji.
tutakunywa cha kibaha dogo.. naona mdmo umekukauka. Aliongea BOSCO na mimi sikujibu chochote. Aliwasha gari na safari ilianza hapo. Kwakua nilikua namuamini bosi wangu hyo,wala sikuulizia maswala ya mshiko, ila nilijua tu mshiko nitakaupiga siku hiyo, nitaweza kulipia hata chumba ninachodaiwa kwa mwezi mmoja sasa.
Gari ilipamba moto huku gesi ya gari hiyo ikiendelea kulalamika. Mafuta yaliendelea kuchomeka na kusababisha matokeo ya spidi ya gari kuwa kubwa huku muendeshaji akitikisa kichwa kutokana na mziki uliokua unalia humo ndani.-kama bado una usingizi, lala huko nyuma. Aliongea Bosco huku akitabasamu.
niko poa tu. nlijibu huku nikiwa na hofu kidogo ya usalama wangu kutokana na uendeshaji mbaya wa gari aliokua nao Bosco.
Tulifka kibaha na tukapaki gari na kuingia kwenye mgahawa mmoja mkubwa.
kula kama mwanaume ambaye anatarajia kushusha mzigo wa tani tatu peke yake. Sasa we agiza chapati mbili halafu uniambie eti huna spidi ya kazi. Alinitania na kumuita muhudumu ambaye alikuja kutusikiliza.
Kwakua aliniruhsu mwenyewe, wala sikufanya hiyana, niliagiza msosi wa nguvu bila kujali gharama yake na kumfanya Bosco atabasamu.
yeah
mi nataka majembe ya kula na kufanya kazi pia.. kama wewe Deo. Aliongea maneno hayo huku na yeye akikandamiza supu ya mguu wa mbuzi uliolala pale mbele huku seheni nyingine ikiwa imejaa chapati takribani tano.
Baada ya kupiga msosi huo, tuliingia kwenye gari na kuanza safari kwa mwendo kasi zaidi wa ule wa mwanzo kutokana na kutokua na foleni wala msongamano wa magari ya hapa na pale.-Sikua napajua ni maeneo gani, ila kulikua na milima mirefu na juu ya milima hiyo ilikua kama inafuka moshi kutokana na baridi na hali ya hewa iliyokua huko juu.
Sehemu hiyo ndipo gari yetu ilipopata hitilafu na kulazimika tupaki pembeni kwa ajili ya msaada kutoka kwa mafundi ambao tumeshawapigia simu.
ushenzi gani huu
mi nilitaka tufike leo leo na tugeuze leo hii hii ili tuje kula gambe dar usiku. Ila usijali mdogo wangu, lazima watulipe muda wote tutakao upoteza huko. Aliongea Bosco na kuonyesha ni jinsi gani alikua amekasirika.
Baada ya muda kama wa nusu saa hivi, kila mtu alichoka na kujikuta tunatamani kunyoosha nyoosha miguu. Mimi nilitembe kwa mwendo wa kama mita hamsini hivi, ndipo nilipoona kitu kinang`aa na baadae muwako wake ukazima. Nilishawishika kujua kilikua na kitu gani huko. Nikakisogelea na nilipoyatuliza macho yangu, niliiona pete nzuri iliyokua na chata ya sura ya kinyago Fulani hivi.
Kwenye macho yake kulikua na vitu kama vichupa ambavyo mimi nilihisi itakua ni almasi. Niliokota haraka na kuiingiza mfukoni kwangu.-Niliporudi, nilimkuta Bosco akijarbu kuwasha tena gari. Nilipofika tu, gari ikakubali kuwaka na tukaendelea na safari
..
ITAENDELEA
.................... Support yenu ndiyo itakayonifanya mimi nipate moyo zaid wa kuwadondoshea hadithi nyinginezo kama (all of me) na (the nightmare)
r