cosa nostra
JF-Expert Member
- Sep 17, 2010
- 1,773
- 1,809
Hii ni story ya throw backs!
Yaani matukio mbali mbali yaliowatokea waTanzania wanaoishi Tz, Canada, China na UK
Kulingana na maisha waliyoishi~wanavyoishi
Kwasababu ni ndefu sana na wabongo mnapenda kulia lia nikirusha waya mrefu, basi nafupisha!
Badala ya kuanza na mwaka 2008 naruka mpaka mwaka 2014 hadi 2017
Enjoy
Beige:
Baada ya kupigwa na maisha, mambo hayaendi, mambo machungu, mambo magumu, mambo yamesimama,nikikwambia ni sheeedah
Kwa malalamiko yake yeye mwenyewe anajiongelea rohoni
Nimemaliza chuo UK, nimerudi nimetafuta kazi weee lakini wapi! Utadhani nina gundu! Mzee wangu anajiandaa kustaafu, tangu mwaka 2010 mpaka 2014 sijaitwa hata sehemu 1 kwa interview
Nikaamua kwenda kujisomea masters, nikamaliza nikarudi tena Tz, pamenunaa, kweli bongo sio pamchezo mchezo.
Nikajua mzee wangu kuajiriwa kwake kwa miaka mingi nitapata connection hata kwa marafiki zake lakini waaapi! Kila mtu amenuna! Hakuna cha msaada kwa mjomba wala shangazi wala best friends
Basi najikaliaga tu ndani naangalia tv nikaamua kufanya angalau vibiashara, weee! Kama nimetikisa kuzimu! Biashara haiendi
nimeuza nyanya, nimesambaza dagaa maofisin kwenye mabenki na majumbani na nyumba za ibada, nguo za kike na kiume za mitumba nimeuza, mtoto wa UK nimechooookaaa yani nikaona Mungu kaenda likizo kulala! Maana sio kwa kupauka huku! Utadhani nimeshushwa Mbinguni kuja duniani kuhubiri injili! Jesoooooos Christ Mungu jaman nihurumie Abeg.
Nilikuwa na ki bwana changu ki boyfriend nilikipata UK, yeye akawa ameshapata kazi, akawa ananipetipeti elfu 20, elfu10, laki 2 inategemea na mwezi ulivyowaka kwake. Lkn me sikuridhika na ile hali, japo naishi na wazazi lakini bado asee, wazazi hawawezi kuku- support hela kiila siku, Hakuna kitu kinasumbua kama kukaa nyumbani miaka 4 hauna kazi, hauingizi pesa, hauingizi shilingi, me mtoto wa kike, ninamahitaji yangu,nikijiangalia ni mtu wa maendeleo, napeeeenda maendeleo, nina akili ya maisha, nimefanya biashara zote zimekataaa, sasa nimebakia nawaza sijui nimelogwaaa au?!
Kwakweli kama kuombewa nimeombewa sana tu, hakuna mtu anaetoa sadaka kama mimi, sijui 1st fruit (malimbuko), sijui zaka (thithe) hata siibi, sadaka za kila j2 nipo, michango ya kanisani na ahidi ikifika siku ya tukio kulipa sina hata sumni, basi Mungu ananiona ananisamehe, nikaacha mchezo wa kuahidi kanisani. Maana sina chanzo cha kuniingizia pesa mjini!
Yani ukiniangalia mimi.Beige wa UK sio Beige wa Dar
Kukawa na reunion ya watoto tuliosoma UK, tunajijua sie, tulivyo na swaga za kufa mtu!
Nikashindwa kwenda ila natamani
Wakarusha whatsapp sherehe ilivyobamba, wakaandika tumekumiss Beige, bila wewe shughuli haikunoga kiviiile, uuuwi nikamshukuru Mungu maana ningeenda na tenge langu pale ingekuwa noumer! Niliuzaga nguo zangu zooote za UK wakati nauza nguo za mitumba, nikabakiwa na nguo za kibongo, sikuweza hata ku attend reunion.
Mzee akastaafu bwana hapo ndo niliijua kuzimu inafananaje. Maisha ya shida, hapa nilipo nina CV 10 za aina tofauti tofauti, nimesha apply kazi elfu 8 lakini sijaitwa interview hata 1, dah Mungu jaman Mbona unanionea?!
Maisha yangu ni kuchat whatsapp na kuforwad sms za kuchekesha
Biashara zote ziligoma, nimeuza mpaka vitenge wapi, kwanza watu wanakopaaaa, jamani wabongo wanakooopaaa! Kulipa sasa ni sheedah! nimeanzisha blog wapi, yani utadhani kuna shetani ametumwa akae tu na mimi benet aniharibie
To make a long story short, rlshp yangu na yule boyfriend ikawa a-mess, tulianza from scratch! Lakini alipokaa juu kwenye high horse, akaniona me kama mavi, nikamfumania fumu, kiruuu, na mdada m1, ambae nilikuwa na suspect, yeleuuuwi nilichanganyikiwa, rlshp ya miaka 8, mwanaume anakutupa nje kisa hauna kazi, hela, nililala home kama kichaa, naliaaaa.
Sio kama sikuwa na wanaume waliokuwa wananipenda, wanataka kunioa lkn nilikuwa zuzu enuf kuwakataa, nilikuwa very faithfull na rlshp yangu, nikaliaaaaaaa, liaaaaaa, jamaani nililiaaaaa, mamangu mzazi halali alijua ntajiuaaaaaa, nikawa kama nimechanganyikiwaaaa, asee Mungu tu na Mama yangu ndio wanajua, kupotezewa miaka 8 ya mahusiano ni mbayaaaaa, nikakaa mwaka mzima nalia, natukana, nimechanganyikiwaaa, naliaaaaa, dada zangu wanapiga simu wako UK, CANADA wamesikia nimetendwaaa, wananiambia we told u soooo, fanya mpango ukuje ukae hukuuu, mama anawaambia hapaanaaa, huyu ndo namtegemeeaaaa, ndo kila kitu hapa ndani, mwacheni akae na mimi
ITAENDELEA SAA 10 JIONI
This story must be true Ic,Imenikumbusha story ya Dem Wangu
Nilikua na dem katoka UK kamaliza degree yake ya kwanza alikua ana swag sana yani nilikua nikitaka kumtoa out ananiambia sasa hapa mbona ovyo , wakati ndio kamaliza chuo tu hana hata pesa,ndio kwasababu nilimpenda nikawa na go with it
akawa ananiambia mimi sitaki kazi ya mshahara less than 1M enzi hizo 2011,Aka apply kazi akawa akiitwa kwenye interview anataja mshahara kubwa ikawa wanampiga chini coz ilikua nje ya Budget
Akasema ngoja kwanza apige ACCA yani CPA ya UK ili akiunganisha na degree yake ya UK aajiliwe kama Chief Accountant mshahara uwe mrefu zaidi nikawa nawaza vipi awe chief accountant bila uzoefu nikamshauri aanzie msharara mdogo ndio uzoefu utampa mshahara mkubwa hakunisikia,Alipo jaribu kuappy VISA ili arudi UK aka chukue hiyo ACCA ubalozi wa UK kipindi hicho uko Kenya sijui kama wamesha rudi dar kwa sasa, wakampiga chini so VISA akakosa na kazi akawa hana
Kipindi hicho mimi ni kawa nishaanza kumpotezea taratibu coz nilimuona sio wife material hakuwa na mawazo ya uhalisia wa maisha ya Tanzania.
Nikapata kazi mkoa,Tukawa tuna wasiliana kama marafiki tu, akanipigia simu siku hiyo analia maisha ni magumu sana anatafuta kazi yoyote coz home kwao kushakua kwa moto anazinguliwa na kaka zake kisa anaonekana haoneshi juhudi za kusaka kazi
Saizi kazi EXIM Bank analipwa Mshahara Sh 270,000 baada ya makato amechoka mbaya ,Nilipo onana nae akaniambia saizi amenyooka alikua anajidanganya sana sana alipo fika from UK kwani alikataa mshahara wa laki 8 na mpaka saizi ungekua umesha ongezeka.
Umri wake umekwenda ana 30 yrs ananiambia anataka mchumba wa kumuoa ila hajapata anahisi hata olewa kabisa
In my heart nikawaza angekua mke wangu ila ndio tayari nishaoa na nina watoto sasa.
She is so lonely
Nilicho jifunza kutoka kwa huyu dem wangu wakitambo ni kwamba wasichana wengi wanaotoka kusoma nchi za nje huwa wana expections kubwa sana
Nawaomba wabadilike
