1st CLASS BEYAAACH:
Kwakweli poleni Beige na Fu~Mi. Poleni sana,
Am no angel either ( me sio malaika pia) lakini maisha yangu sio ya kudanganya!
Me nimezaliwa na kijiko cha silver mdomoni, mama yangu alikuwa balozi nchini Canada, Baba alikuwa Mfanya biashara mzuri tu, kwetu tumezaliwa 3, me ndo msichana pekee wengine wote wanaume. Kwetu me wa mwisho kaka zangu wamenitangulia so nilikuwa protected always na kaka zangu, nilipeeeendwa yani me na baba yangu tumeivaaa. Kuanzia Nursery mpaka Chuo nimesoma Canada, nilizaliwa Bongo nilipofika mwaka Mama akahamishiwa Canada, life yangu ni kama ya akina Prince William, Charles, sijui shida, what is shida?! Eh?! Me sijisifii
Ninekuja kusoma Nursery expensive schools, nakaa expensive streets, houses, hotels, 1st class flights, 1st class saloons, parties, music, books yani harry potter haijatoka mtaani me nasoma manual script! Nyie mnakuja kucheki harry potter me naongelea movie zingine!
Nikamaliza shule nikaingia chuo,nikapiga business nikamaliza BBA, nika fall inlove na fashion, nikaomba nipelekwe kwenye fashion industry, nakutana na akina Naomi campbell, Tyra Banks, eh! Nyie mpaka mje kuwaskia me nime~hang nao sanaaa tuu! Nikaanzisha clothing line yangu nikiwa canada, mzee aka weka pesa yake pale, nikafaulu nguo zikatemaaa, nikapata karibia dola laki 5, kaka zangu wakaniona me wa ukweli,
Kakangu wa kwanza daktai Canada, ni Neuro~surgeon, ana mke na watoto 3, kakangu wa pili ni Financial Analyst, alianza kufanya kazi HSBC BANK baadae akapata IMF baadae akahamia World Bank. Ameoa ana watoto mapacha 2 wote wakike na kiume mmoja
Yani kwetu shida hamnaga! Au niseme kulikuwa hamnagaaa, mzee wangu na ma connection yake ya business yupo mbaaalii, tunaonana jioni kwa dinner table tuu, me sikubahatika kuolewa nilijiona mdogo sanaa, nikawa natafuta hela nanunua ma hisa Canada na Marekani na UK, kiukweli me ni raia wa Tz lakini nimekulia Canada tz siijui saaaana maana nimeondoka na mwaka
Nikaamua kwenda kusoma Master ya MBA, univeristy of Toronto, nikamaliza nikaendeleza bness yangu ya fashion lakini nikawiwa sana kuja Africa kujifunza fashion hizi za vitengee sijui nini, mwaka wa 2013 mwishoni kwenda 2014.
Nikateremka kwa mrembo wa France, bibie Nanawax, tukaongea biashara ya kutengeneza vitenge, nikamwuzia idea akaikubali, akawa model mwenyewe me nika pinch in some money (invinsible investor) akafanya vizuri sana, nikawa nawatuma wazungu wanakuja ku cut design and stuff! Mpaka sasa NANAWAX sidhani kama ana mpinzani, kwakweli namshukuru Mungu me maisha ya shida shida hata siyajui nawasikia nyie na inanifanya nizidi kumshukuru sana Mungu kwa jinsi alivyonipendelea
Wenzake wakaangaliana tu kweli Mungu aache kututania!
Akaendelea na ubuyu, maisha yakaja kunipiga au sijui nilikosea wapi, me sikuwahi kuwa na boyfriend wala nini, buzy na maisha tuu so mpaka umri wa miaka 26 nikawa bado bikra
Wenzake wakasema tobaaa! Enhe!?
Sasa siku moja nipo zangubkwenye ndege (1st class) naja zangu na maza Tz, aliitwa huku bwana, tukaingia Tz tukafikia hotelini The Kilimanjaro Hotel, tumekaa mpaka alipopata nyumba Oysterbay! Tukahamia Oysterbay, tukakaa me na biashata zangu kwenye ipad! Siku moja maza yupo ofsini nikasema niende kutembea Mbudya! Kama nilikosea sijui nilipatia, nikalipanda boti pale sea cliff, kufika mbudya watoto wa kibongo kibao na much know zao ushuzi mtupu me nawaangalia nawadharaaaau nimejikalia na kichupi na sidiria na bake kwa jua! Nimeoiga sun googles zangu kama kawaida yangu, na kajuice kadogo kamekaa hapo pembeni mara namwona mnyamwezi amesimama mbele yangu, nikamwangalia kwenye miwani akahisi nimelala! Kumbe namwona akaja akanisalimia sikumjibu
Hi;
Me: kimya
Mnyamwezi: naitwa Wonder!
Me: kimya
Akaenda akachukua kiti cha plastic akaja akajiongelesha weeee
Me: kimyaaa!
Akaongea wee me hata sikumsikiliza nawaza biashara zangu wenzake wakaja wakamchukua akaondoka, nikarudi zangu home baadae
J2 naenda church hapo st.peters nimekaa kwenye ibada naskiliza preachings mara namwona kasimama kwa pembeni ananiangalia, nikajikausha, saa ta kutoka akaja kunisalimia
Oh samahani nakufananisha!
Me: nikafungua gari nikaingia
Na yeye akaingia
Nikamkata jicho, kwa maana shuka you disgusting maniac!
Akaniuliza ivi wewe ni bubu?! Sikumjibu
Akaniambia, dada me nakupenda naomba unielewe, nataka hata dk 20 na wewe
Nikawasha gari vuuuum mpaka sea cliff, nikapaki pale spurs nikaingia kula akanifuata, nikaagiza na yeye akaagiza. Nikala nikakaribia kumaliza akaniambia dada me nakupenda, nataka kuwa mpenzi wako, sikumjibu!
Akaendelea kuongea weeeeee, nikalipia chakula nikainuka kwenda toilet kurudi namkuta, nikanyanyua kila kilicho changu nikaondoka akanifuata, nafungua mlango yupo nyuma yangu, nikaingia ndani ya gari akanishika kwa nguvu akanichum, chum chum chum na wewe me nimeukaza mdomo kama mamba, yeye anajaribu kuutoa ulimi auingize kwangu me nimebana mdomo
Akachoka akaacha business card yake kwenye gari yangu akaondoka me nikawasha gari huyoo wetu njia nzima najifuta mamate yake,
Ikabidi nipaki tu pembeni ninawe usi na mdomo nikafika nyumbani nikaogaaa bonge la bath, najisugua mwili mzima huku nalaani, shenzi kabisa hawa majambazi ana bahati sijamwitia polisi, nikaenda kwenye gari nkaichukua ile bness card akaitupa kwenye dustbin nikaendelea zangu na biashara zangu za online na blogs!
Baada ya wiki 1 akaja nyumbani mdogowake na maza, tukamkaribisha katoka huko kijijini, akapewa chumba akalala lakini ma mdogo huyu hakosi kung'ang'ania kukaa chumbani kwangu, sijui alikuwa na nini na mimi, roho yangu ilimkataa kabisaa, nikawa simpendi siku nyingine nikitoka sirudi, nalala hotelini hata wiki namwambia nimesafiri, nikirudi namkuta kahamia chumbani kwangu yani kero mtindo m1, jamani sitakaa nimsahau yule mama mdogo nikakuta amevurugua chumba changu, kapuliza perfume zooote, kachukua nguo yani so classless
Nikamsemea kwa dadake(mama yangu) akasema basi nitaongea nae and shit, akaenda ongea nae kesho akaaga anarudi kijijini, me nikaendelea na maisha yangu siku nimekaa napanga nguo naona nguo moja siioni, ni top yangu nilikuwa naipenda sana naivaaga usiku siku ya alhamisi, mh siioni, uliza maids hamna kitu, uliza kwa mama hamba nikajua tu moja kwa moja kuwa mamdogo kachukua nikaenda kumweleza mama (dadake)
Dadake kusikia akanikalisha chini kunieleza, kuwa yule mdogowake anapenda kwenda kwa mganga sanaaa, na hajui wala haelewi kwanini alumkaribisha
Mmiaka ya nyuma, alishawahi kumkaribisha akamkuta amelala na mumewe (baba yake) akapataga mimba, nikakasirika sana hata kabla wewe haujazaliwa (mama ananihadithia sasa)
Mtoto akazaliwa me nikadai talaka kwa mume nimenuna kweli kweli, baadae nikamweleza bibi yako alikuwa bado yupo hai akaweka kikao tukasuluhishana nikasamehe ndio kupata kazi kuwa balozi, tuka reconcile na babako hapaa pita pita za hapa na pale nikapata mimba yako
Sasa mama yako mdogo yule mtoto Mungu alivyo wa huruma siku unazaliwa ndio siku mwanae aligongwa na gari akafa, sikuweza kuhudhuria msiba kabisaa, kwasababu ya uzazi na wewe ulipofika mwaka 1, nikapata promotion kazini nikaondoka kwenda Canada. Sasa kama amechukua nguo yako basi kuna kitu, tukafunga safari mpaka kwa Pastor wa kilokole, yakapigwa maombi weeeee tukarudi home
Baafa ya siku 3 tunapigiwa simu kuwa mama mdogo anaumwa sana mahututi kalala kitandani hajiwezi
Mama na mie tukafunga safari mpaka mbeya
Tunatia mguu kwa bibi watu wanalia, Mama mdogo amekufa sasa hivi yani kama mnapishana nae mlangoni, mama akalia pale me hata sijui misiba ndo nini, tukakaa msiba ukaisha wakazika tukasubiri tanga likavunjwa mama akasema tukae mpaka 40 nimechukua likizo, tukamaliza 40 mbeya ni sawa na kumaliza 40 kuzimu, pabayaaa, basi natambulishwa pale kwa watu wajomba na nini, siku haziendi! No connection na Tz yenu no internet basi nikaona nacheleeewa kweli kweli! Siku 1 bibi akaniita akaniambia jinsi gani mama mdogo alivyoumwa nika connect na yale maombi niliofanyiwa ndio siku aliumwa nikajua mamdogo kuna kitu wakati naongea na bibi kuangalia pembeni naona ile nguo yangu kudadeki, nikamwuliza bibi hii top vepee akaniambia nilipewa zawadi na mamako mdogo, nikauchuna chunu! Siku ya kuondoka nikamwambia bibi hii nguo itupe tu usiivae, hakujua kwanini akamwita kijana wa ng'ombe akamwambia akaitupe. Kijana na tamaa zake akaenda kumpe girlfriend wake, beibe kuivaa akafa siku hio hio hawakuelewa! Wakajua labda kifo cha ghafla, nikajua ile nguo iliwekewa kitu kibaya sana, nikaondoka Mbeya nikiwa salama rohoni, bibi hakuivaa tena ile top na mimi sikuichukua, lakini njia nzima nikawa namuwaza Mr Wonder sikujua kwanini!
ITAENDELEA SAA 3 USIKU