Love is a drug abuse

hancy Abdon

Member
Joined
May 24, 2026
Posts
87
Reaction score
58








SEHEMU YA KWANZA

AGE.............................18+

THE STORY MASTER

AUTHOR...................... Hancy A abdons



"Kuna mwanafunzi mgeni!".

Nikazungumza na kumtizama mtu aliyeniletea hiyo taarifa alikuwa ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza.

"Ndiyo mkuu".

akazungumza kwa uwoga baada ya mimi kusimama

juu ya meza niliyokalia huku mkononi nikiwa na kitabu cha mabara mbalimbali ambacho kilihusu mabara ya duniani siyo mabara the farmer akaanza kurudi nyuma huku midomo ikimtetemeka.

"Nishakukataza kuniita mkuu!".

Nikazungumza na kumshika shati yake shingoni nikamkamata vizuri shingo yake.

"Mwalimu anakuja."

sauti ikasikika nyuma yangu nikageuka na kumtazama Ray

"Kwahiyo"?.

Nikamjibu kisha nikamwachia yule kijana mdogo wa mwaka wa kwanza chuoni hapo akapepesuka kutaka kuanguka, mwili wake ulikuwa mdogo kama mnyoo.

"Mlete kule chini."

Nikazungumza na kuondoka ndani ya darasa hilo ambalo tulikuwa humo watu wanne pekee, Wenzangu watatu wakanifuata nyuma, na yule kijana akabaki amesimama huku ametupa mgongo; alikuwa bado anaogopa."Tabia yako bado hujaacha!" Sauti ya mwalimu ikanifanya nimtazame kwa dharau kwani nilikutana naye kwenye mlango. Alikuwa ni madam mwenye umbo kubwa; hips zake zilikuwa nene zilizoshiba mithili ya shape ya Kajala, yaani makalio ya Kajala halafu hips ya Mobetto, sura Mungu hakumjalia kivile. Nikanyanyua lips zangu huku nikimtazama kwa matamanio."Dominick unanitazamaje? Hili jambo naliripoti kwa mkuu wa chuo!" Madam akazungumza na kisha akasogea dirishani na kumwita yule kijana wa mwaka wa kwanza."Una roho mbaya, unatesa wenzako kisa kwenu mna hela, kisa baba yako ni Rais!" Akazungumza kwa uchungu ila sikujali nikapiga hatua kwenda napo kwenda.

"Na nyie mnaomfuata mwandike barua ya utovu wa nidhamu!".

Akazungumza na akaondoka na yule kijana mdogo kuelekea ofisini huku maumbo yake ya nyuma yakitingishika kama mfuko wa rambo wenye maji.

"Huyu madam mshenzi sana,"

Ray akazungumza. Nikatingisha kichwa na kuelekea darasani kwenye kipindi ambacho kilikuwa kinaanza muda mchache ujao, lilikuwa somo linalohusu mambo ya biashara na uchumi."Sitaki kelele!" Nikazungumza baada ya kuingia darasani na kukuta watu wakipiga kelele. Waliposikia sauti yangu wote wakatulia tuli, hata walioniona kabla sijazungumza walirudi kwenye siti zao. Nikaenda kwenye kiti changu kwa ajili ya kuketi, nikakunja ndita..

Baada ya kuona kalamu yangu ikiwa chini,

"Wewe ndiye uliyeangusha hii kalamu?". Nikamuuliza swali jirani yangu ambaye akanitazama kwa woga.

"Ni upepo," akanijibu.

"Na ukaiacha? Baadaye uje kule chini,". Nikazungumza na kuiokota."

"Husikii kupulizia marashi yako hayo?." Nikamuuliza swali msichana aliyekuwa pembeni yangu upande wa kulia. Marashi yake sikuyapenda toka siku ya kwanza nilipoyasikia.

"Mama hajanunua mengine," .Akanijibu na kuendelea kuandika kwenye kitabu chake kidogo mithili ya diary.Nikatazama katikati ya darasa na kumwona kijana niliyempiga juzi kipigo cha mbwa koko akiwa amelalia dawati. Nikatabasamu kwa furaha kwani napenda toka moyoni mwangu kuona mtu akiteseka, napenda kuona mtu akiwa na damu puani, mdomoni au popote pale.

Napenda kuona mtu akilia kwa maumivu makali huku akiniomba msamaha. Sipendi kuona mtu akifurahi au kutabasamu.Mwalimu wa somo la biashara akaingia darasani. Tukampatia heshima ambayo kila mwanafunzi anatoa kwa walimu au wakufunzi wake toka vidudu mpaka chuo kikuu. Alikuwa ni madam mwembamba mwenye umbo la Kisomali; alivutia kama twiga mbugani. Nikaacha kumkagua mwili wake baada ya kuanza kuzungumza."Jana sikumaliza kipindi, kwa hiyo nitafanya double!" Akazungumza na kufanya nitabasamu kwani huwa napenda kumwona kila muda.Ghafla darasa zima likalipuka kwa shangwe na furaha zilizoambatana na miluzi ya vijana wa kiume. Nikamtazama Ray na wenzake wawili ambao nao wakawa wananitazama, mimi.

Hatukujua kwa nini watu wale wanapiga kelele za kufurahi bila uwoga. Nikatazama mlangoni ambako watu wanatazama, nikamwona kijana wa kiume anaingia, mrefu mwenye umbo la misuli (mazoezi). Nikatabasamu baada ya macho yetu kugongana na yeye akatabasamu.

"Alex, Alex, Alex!" Watu wakaanza kutaja jina lake kama shujaa waliyemmiss kwa muda mrefu. Nikamtazama mkono wake nilioutegua (vunja) miezi mitatu iliyopita ulikuwa mzima, ulikuwa hujafungwa na P.O.P pia hata shingo yake ilikuwa nzima.

"Nitakuua, Dominick,"

Akazungumza kwa sauti nzito iliyofanya wanafunzi wote kutulia.

"Alex, maneno gani hayo?"

Madam akazungumza,Na kumtizama alex aliyenikazia macho, Nikasimama na kuelekea kule mbale ya darasa,alipo Alex, nikamtazama juu mpaka chini, mguu wake wa kulia niliouvunja miezi 2 iliyopita ulikuwa mzima.

Akatabasamu baada ya kuona namkagua.

"Baba yako amekupeleka India?" Nikazungumza na akatabasamu kwa kejeli.

"Nitahakikisha nakulaza miezi 6 kitandani!" .Akazungumza na kufanya watu wote kushangilia kwani hakunaaliyenipenda hata mmoja kutokana na tabia zangu mbaya za uonevu nilizokuwa nazo chuoni hapo. Kila mtu alionekana kumpenda Alex ambaye alikuwa ni head boy chuoni hapo na alikuwa mkarimu machoni mwa watu, alikuwa na roho safi na ndiyo mpinzani wangu mkubwa chuoni hapo yeye alikuwa mtoto wa Rais mstaafu, hakupenda tabia zangu ijapo kuwa mimi niliona niko sahihi.

"Demu wako nitambusu tena ili uje upambane na mimi!" Nikazungumza na kugeuka kumtazama Clara ambaye ni demu wa Alex, Clara akamtazama...

Alex huku machozi yakimlengalenga kwani nilimdhalilisha mbele za watu, nikaona hasira za Alex kifuani mwake zikipanda na kushuka kama mtu mwenye presha."Ukimshika tena Clara..." Alex akashindwa kumaliza kuongea, sauti ya mkuu wa chuo ikasikika."Njooni ofisini wazazi wenu wamekuja." Tukatazama dirishani na kumwona mkuu wa chuo akitutazama kwa macho makali, Alex akageuka na kuondoka nami nikafuata kwa nyuma na kundi la watu wachache wakaanza kunizomea, nikarudi kwa haraka darasani na wakatulia tuli.

"Ray, wakabili wote watakaonizomea.

""Sawa Domy," Ray akanijibu na nikaondoka bila ya kusikia sauti yoyote ile, nikaona msafara mkubwa wa magari ukiwa pembezoni mwa geti kuu, ofisi ilitazamana na geti kuu la chuo, ofisi ya mkuu wa chuo.

"Huyu mzee vipi?" Nikawaza na kuingia kwenye ofisi ya mkuu wa shule. Nikamwona baba akiwa amekaa upande wa kushoto huku Rais aliyepita madarakani mwaka uliopita naye akiwa ameketi upande huo huo wa kushoto na wanaume wawili waliovaa suti wakiwa nyuma ya mgongo wa baba. Nikamwona Alex akiwa katikati ya duara kubwa lililochorwa kwenye sakafu ambalo chuoni hapo tunaliita kikaango cha watukutu. Nikapiga hatua nami nikaingia kwenye lile duara, mkuu wa shule tukawa tunatazamana naye pamoja na wazazi wetu.

"Mnataka kuwa mabondia tumlete Tyson nchini?". Baba akazungumza huku akinitazama kwa macho makali ambayo kama angemtazama mtoto mdogo angelia na kulala usingizi fofofo. Nikatingisha kichwa kukataa alichozungumza.

"Mnataka kila siku mtuone hapa chuoni, hivi mnaleta picha gani nchini? Nashindwa kutatua changamoto za wananchi, tunashindwa kupanga mipango jinsi ya kuinua taifa letu toka uchumi wa kati mpaka wa juu, tena tuwaze na watu kama nyie wenye mapumbu!" Baba akazungumza kwa ukali zaidi huku akinikazia macho. Nikatizama pembeni.

"Alex, nitakuhamisha chuo." Rais aliyepita madarakani akazungumza.

"Baba haiwezekani, sitakubali!" Alex akazungumza kwa upole.

"Kwahiyo unataka ugomvi uendelee? Unataka mpaka wakuue au uue na wewe? Umelala hospitali miezi 3 hujitambui, mifupa imeteguliwa bado unataka nini?!" Baba Alex akafoka.

"Tupeni nafasi ya mwisho," nikazungumza na kuwatazama wote wawili.

Wakanitizama."Sababu ya kuonewa wenzako nini?" Baba akaniuliza, nikabaki nimetumbua macho.

"Mkuu hebu wachape viboko, inaonekana hamuwafundishi adabu."

Baba akazungumza na mkuu wa shule akasimama na kutoa heshima.

"Samahani mheshimiwa Rais na mstaafu, hawa tunawaonya sana na kuwaadhibu kwa kuwapa adhabu. Chuo chetu akiruhusu kuwatia fimbo wanafunzi wetu." Akazungumza.

"Nitamteua mtu mwengine." Baba akazungumza na kufanya mkuu wa shule ashtuke, akapiga simu hapo hapo.

"Nenda Form Six niletee fimbo za kutosha!"

"Zilete ofisini kwangu sasa hivi." Akazungumza na akakata simu.

"Hatuwezi lea ujinga kisa wazazi wenu wakubwa, mnafanya upuuzi chuoni!" Baba Alex akazungumza.

"Hawa wanatugombanisha, mitoto mjinga sana hii, mzee mwenzangu." Baba akakazia.Madam akaingia ofisini akiwa na mwanafunzi wa Form Six ambaye alikuwa kabeba fimbo za kutosha, mwanafunzi yule alipowaona wazazi wetu akashtuka sana, hakutegemea kama angeweza kuona watu kama hao.

"Shikamooni wakubwa," akazungumza kwa uchangamfu kuficha mshangao wake na uwoga, wakamuitikia wote kwa pamoja.

"Form Six?" Baba akamuuliza.

"Ndiyo kiongozi!" Akajibu.

"Sawa, sawa, kazana!" Baba akazungumza.

"Asante sana." Akaondoka huku uso wake na macho yake yalionyesha mshangao wa wazi kabisa.



ITAENDELEA.....
 
SEHEMU YA PILI

Yule madam akatoa heshima na yeye kisha mkuu wa chuo akachukua fimbo.
"Chukua hiyo kubwa!" Baba akazungumza na kusontesha kidole kwenye fimbo nyingine ambayo kweli ilikuwa kubwa. Nikameza mate huku kijasho chembamba kikaanza kunitoka.
"Malaya mkubwa wewe! Leo nakuua, unatembea na kaka yangu!" Sauti hiyo ikapita kwenye masikio yangu, lilikuwa ni tukio la zamani lililopita likanijia kichwani mwangu.
"Domy siyo mwanangu, yaani umezaa na kaka yangu!"
Sauti ya baba ikafanya nizidi kupata, maumivu kwenye kumbukumbu yangu. Nilimwona mama akipigwa na baba kipigo cha mbwa mwizi wakati huo nikiwa na miaka 7.
Fimbo ya makalio ikafanya nishtuke toka kwenye dimbwi la mawazo ya miaka mingi iliyopita. Nilikuwa naogopa fimbo kwani nimeshuhudia fimbo ikimchapa mama yangu mzazi, tena toka kwa baba yangu aliyeketi hapo ofisini.
"Shuka chini!" Mkuu wa chuo akazungumza kwa sauti kali ambayo sikumbuki mara ya mwisho kuisikia ilikuwa lini.
"Mkuu!" Nikazungumza ila nikajikuta tayari nipo chini. Fimbo ikashuka juu ya makalio yangu na ikapenya vizuri kwenye ngozi yangu. Nikapigwa fimbo za haraka haraka na za nguvu toka kwa mkuu wa chuo; zilikuwa fimbo 7 za moto. Nilisikia maumivu yake mpaka kwenye ubongo. Akafuatwa na Alex ambaye yeye alikuwa tayari amekwisha shuka chini; mwenzangu alikaza akupepesuka kama mimi.
"Head boy unakuwa mjinga kiasi hiki!" Baba yake akazungumza.
"Nikisikia tena nakuhamisha chuo." Baba akazungumza na kunyanyuka.
."Niwaongeze mheshimiwa?"
Mkuu wa chuo akazungumza na nikamkazia macho hasa jicho la kushoto, mpaka akajishtukia Baba akatoka kwenye siti yake na kupiga hatua kuja nilipo.
"Dada yako kamaliza kusoma Marekani hii wiki anakuja, jiandae kwenda kumpokea." Akazungumza na kunishika bega.
"Sawa Baba."
"Masomo mema!" Akazungumza na kumshika Alex mkono kisha akatoka na mlinzi mmoja akatoka naye huku aliyebaki akasimama mlangoni."Sitasikia fujo tena, Domy." Baba Alex akazungumza na akaondoka na yeye, tukabaki na mkuu wa chuo
."Ona Mambo yenu sasa," na yeye akatoka na kuwafata wale wageni wake, tukabaki ndani watatu, mimi, Alex na yule madam ambaye alikuwa amesimama mbali kidogo.
"Yote yameisha," akazungumza na kutusogelea."Sawa madam!" Alex akazungumza.
"Kumbatiani!". Akazungumza na sote tukamtazama kwa mshangao kwani hakuna aliyekuwa tayari.
"Haiwezekani," nikazungumza.
"Hivi kwnini una mdomo sana domy " Akazungumza na kuinua fimbo.
"Mkumbatie mwenzako," akazungumza na kunisontesha fimbo, ncha ya ile fimbo ikawa inatazamana na jicho langu la kulia.
"Huyu mtoto siyo wangu najua!"
“"Lakini kumbuka wewe mwenyewe ulisema nitafute mwanamume wa kuzaa naye ufiche aibu yako mume wangu". Sauti ya mama ikasikika vyema masikioni mwangu kipindi hicho nikiwa mtoto mdogo miaka 6.
“ Ndiyo, uzae na kaka yangu!" Baba akazungumza na akavua mkanda wa ngozi wa suruali yake, akaukunja na kushika kule kwenye kitasa. Akawa anatutazama mimi na mama tukiwa chini, huku mama akiwa amenikumbatia kwa nguvu. Baba akaanza kushusha mikanda ya nguvu ambayo mingine ilinipata na kufanya nianze kulia kwa sauti, na mama akanikinga na kunikumbatia kwa nguvu na mikanda yote ikatua kwenye mwili wake.
"Hata kama sina nguvu za kiume, ndiyo uzae na pacha wangu? Kwa hiyo ulitaka damu isitoke mbali?!"
Akafoka na kuzidi kushusha mikanda ya nguvu
“ Nisamehe mume wangu, nimezaa na kaka yako ili damu isitoke nje ya kabila letu,maana mila zetu hazirujusu kuzaa nje , pia huenda mwanaume wa nje angekusumbua sana!" Mama akazungumza kwa uchungu.
"Wewe mpuuzi!"
Sauti kali ikasikika na kunitoa kwenye dimbwi zito la mawazo na mchanganyiko wa maluelue niliyokuwa nayo, nikamwona mwalimu mkuu akikusanya faili zake huku Alex akiwa anaelekea mlangoni na yule madam akiwa na fimbo zake."Toka humu, husikii tu!" Akafoka.
"Samahani!". Nikazungumza na kushika kichwa changu kisha nikaondoka kuelekea darasani na kujifanya kuwa hakuna kilichotokea ofisini. Nikamwona Alex akiwa na mpenzi wake Clara wakionekana kufurahi, nikakunja ngumi baada ya kuona tabasamu lao tena toka ndani, kitu ambacho sipendi nikuona mtu au watu wakiwa katika furaha uwa nahisi wananicheka.
ITAENDELEA….
 
LOVE IS A DRUG ABUSE
SEHEMU YA TATU



Nikashika rungu na kuanza kulirusha rusha huku nikimsogelea kijana aliyekuwa mbele yangu, huku akiwa amepiga magoti chini na damu kutoka kwenye tundu moja la pua yake, nikamshika kidevu na kukibinua juu.

"Kwanini kalamu yangu hukuichukua?". Nikazungumza na kutizama rungu langu ambalo ndilo lililomraza alex miezi mitatu hospitali, ndiyo silaha yangu kubwa chuoni hapo.

"Sitarudia domy!!" Akazungumza na kulia kwa uchungu, moyo wangu ukafarijika baada ya kuona machozi yake

."Nenda ole wako useme chochote." Nikazungumza na nikamfuta damu yake ya pua kwa kutumia kitambaa chake na nikamkabidhi na kwa haraka akakimbia na tukaanza kumcheka mimi na jopo langu.

“ Kuna msichana mzuri kaletwa ni kisu hatari!!"

"Siyo vitu vyangu hivyo" Nikazungumza.

"Ah domy yaani unasema hivyo ujamuona huyo binti yani mweusi fulani hivi kama mwarabu wa kisomali nywele zake ndefu tena asilia siyo ma wigi kama ya jamila halafu sasa anakaa mbele yako"

."Mbele yangu?"

"Ndiyo leo si ukuingia darasani kaletwa huyo binti yaani Mwarabu yule mtoto amekamilika".

"Poa siyo kitu cha ajabu hicho." Nikazungumza na kumkazia macho.

"Sawa basi samahani." Akazungumza kwa upole.

“Ray yuko wapi leo?"

"Alitoka kidogo kuna mambo anafuatilia".

"Sawa" ghafla kishindo kama cha kuanguka kitu kilisikika "puuh" kwa haraka tukatoka nje na kutizama huku na kule, tukafanikiwa kuona mwili wa mtu ukiwa chini unavuja damu...

Tukamsogelea na kwa taharuki nikashtuka baada ya kumuona yule msichana ambaye kila siku nagombana naye kuhusu manukato yake mabaya yenye harufu kali. Tukatizama juu na kuona mgongo wa mtu ukiishia juu ya ghorofa lile la darasa letu.

"Ameanguka toka juu" .Raja akazungumza na tukatizama ghorofa lile ambalo ni darasa letu ulikuwa umbali mrefu zaidi ya ghorofa kama 3 hivi na ameanguka kwenye sakafu ya vigae vya mawe ambavyo vimejaa chuo kizima kwa ajili ya kuzuia vumbi na pia uchafu na kuvutia chuo chetu tofauti na vyengine.

"Anapumua". Nikazungumza na kwenda kumshika msichana yule, alikuwa ameshika tumbo lake damu zilikuwa zikimtoka puani na mdomoni kwa wingi pia kichwa chake kilikuwa kinavuja damu ya kutosha, na nyengine zikichuruzika toka sehemu za siri maana alivaa sketi fupi ambazo ndiyo sare zao.

"Nenda katoe taarifa" .Nikazungumza

."Tukimbie Domy hii kesi!" Rajah akazungumza.

" Kwani jengo si lina kamera inapiga upande wetu". Nikazungumza na kutizama kamera kisha nikashuka chini na kuanza kubeba mwili wake.

"Hazifanyi kazi domy". Rajah akazungumza na kunisisitiza kuwa hiyo ni kesi.

" Hapa chuo hakuna anayekuhamini kuwa wewe ujafanya chochote kama ukikutwa eneo hili".

" huyu kapatwa na tatizo". Nikazungumza na kubeba mwili wake vizuri na kuanza kumkimbiza hospitali ya chuo ambayo ni mita chache tu toka nilipo, watu wakabaki wamenikodolea macho kwani kila mtu alishangaa nini kinaendelea,jopo kubwa la madaktari likaja na kitanda cha kusukuma kwa haraka wakamlaza yule binti na kuanza kukisukuma kwa haraka kwenda ndani ya vyumba vya matibabu.

" Kawaje huyu". Dokta akaniuliza huku uso wake ukionyesha kunikazia kama nahusika katika hilo kwani hata siku moja sijawahi msaidia mtu.

" Amesukumwa". Rojah akazungumza na kufanya daktari kumtizama.

" Na nani?".

" Tuliona tu mgongo wa mtu".Nikazungumza na daktari akatingisha kichwa chake na kuelekea kwenye majukumu yake.

"Nimefanya nini sas?". Nikazungumza huku nafsi ikinisunta kwa kumsaidia au kumpeleka binti yule hospitali, hali yake ilikuwa mbaya mno na anaonekana alikuwa mjamzito.

"Umetaka tuwe mashahidi we ungesema tumemkuta chini". Nikazungumza na kumtizama rajah

" Nimesema hivyo kukulinda mkuu ili uchunguzi ufanyike ibainike ni nani aliyefanya hilo tukio". Rajah akazungumza na kufanya hasira kidogo zipungue.

" Umesema kamera za pale hazifanyai kazi?"

" ndiyo sasa zingekuwa zinafanya kazi uhalifu wetu wa kule chini tungeonekana kila siku". Akazungumza na kutingisha kichwa chake huku akitabasamu juu ya matukio yetu maovu ya kupiga watu bila huruma.

" Ni Mjamzito". Nikazungumza na rajah akanishangaa.

" Umemtambuaje". Akaniuliza ila sikumjibu tuka toka hospitai na kukutana na jopo la uchunguzi likiwa nalo linafika.

Lilikuwa jopo la uchunguzi hapo hapo chuo, uchunguzi wake ni siku moja pekee halafu taarifa ndiyo inafika polisi, walifanya hivi ili matatizo ya chuo yasitoke nje pia jopo hilo lilipewa kibari na polisi kwa siku moja pekee na pia kulikuwa na polisi wawili katika jopo hilo hili kuhakikisha hakuna kitu kinachoharibika yani kilikuwa chuo ambacho kila idara ilikuwepo.

" Domy na wenzako tunawahitaji". Kiongozi wa hilo jopo akazungumza na kunitizama kwa hasira za wazi wazi, kwani kesi zake nyingi akinishtaki nilikuwa namshinda, akanisogelea,

" Hii kesi najua uchomoki hata kama baba yako ni rais ni ngumu sana kujinasua". Akazungumza na kutabasamu, nami nikatabasamu na kumnong'oneza sikioni kwa sauti ya chini sana.

" Najua wewe ndiye uliyefanya ilo tukio". Nikazungumza na kumuona jinsi alivyoshtuka na kutizama kulia na kushoto kama kuna mtu amesikia kauli yangu, nikamuona jinsi uso wake ulivyobadirika ukawa wa mshangao zaidi.

" Najua ni vita ya mapenzi". Nikazungumza na kumuona mkuu huyo wa jopo hilo la uchunguzi akizidi kuchanganyikiwa zaidi.

" Unasema kuhusu nini?". Akazungumza baada ya kumuona mkuu wa chuo anakuja kule tulipo.


ITAENDELEA
 
We jamaa huaminiki jinsi ulituacha solemba kule kwenye Ile sea m nilijiapiza sitasoma tena hzi ngonjela.. yaan duh
 
Owaaaah nipo wazeee lazim kielewek lazim ikate sema nini nilipata msiba sa tarh 26 ndio narudi home kwangu naachia mzigo
 
Nilipata msiba wanangu sijafanya kusudi wazee ila tarhe 26 ndio narudi kwangu wanangu af mzigo unaendelea namaliz zote mpaka see me
 
SEHEMU YA NNE…..




“Unazungumza kuhusu nini domy?”. Mkuu wa jopo hilo la uchunguzi akazungumza huku macho na sura yake vikiingiwa na hofu,nikatabasamu na kumuona jinsi alivyoingiwa na unyonge ghafla Mkuu wa chuo akafika pale tulipo na jamaa akamuwahi kumfata huku wakipeana mikono kama ishara ya salamu.

“ Nini kinaendelea?”. Akazungumza huku akinikazia macho

“ kuna uchunguzi unafanyika kuhusu kuanguka kwa Vaileth”. Akazungumza huku akinitizama, mkuu wa chuo akanisogelea

“ Domy ukiwa una husika katika hili tukio hatutokuacha ata kama baba yako ni rais lazima sheria ifate mkondo, maana katiba inamlinda yeye siyo wewe”. Mkuu wa chuo akazungumza na kunitizama juu mpaka chini na akawaita wenzangu kwa ishara ya mkono.

“ Nishawakataza sana kutembea na huyu kijana sasa hii kesi mtaibeba wote iwapo tukikuta chochote kwenye uchunguzi wetu”. Akazungumza

“ Hapana SIR sisi hatuusiki maana tulisikia kishindo cha mtu ndiyo kutizama tukamkuta Vai”. Rojah akazungumza huku uso wake ukionekana kuwa na hofu, alikuwa muoga kupindukia

“Mkuu kusaidia mtu ndiyo kosa”. Nikazungumza kwa sauti ya upole hakunijibu akageuka na kumtizama mkuu wa jopo la uchunguzi.

“ Hakikisha una chunguza hawa vijana kabla ya taarifa kufika kituoni moja kwa moja”. Akazungumza na akaondoka kuelekea hosptali kubwa ya chuo,

“ Hatujafanya chochote wakuu”.Rojah akazungumza huku uso wake ukionekana kushuka kama kizee cha miaka 90.

“Domy twende ofisini nyie wengine nendeni darasani tutawaita”. Mkuu huyo wa uchunguzi akazungumza na wenzangu wakaondoka kinyonge mpaka nikawaonea huruma

Nikaenda ofisini na yule mkuu wa uchunguzi akiwa na askari wawili ambao wao nyumba zao zilijengwa nje kidogo ya chuo icho kwa ajili ya usalama na kila mwaka walibadirishwa,kilikuwa chuo kikubwa gharama yake ya ada ilikuwa inatofautiana kwa kila darasa yani kuna madarasa ya kawaida mpaka VIP na VVIP na madaraja mengine makubwa ya wasomi toka nje ya Tanzania,nikaingia na kuketi kwenye kiti kisha wale askari wakabaki nje baada ya mkuu wao kuwaambia wasubiri,naye akaketi na kuvua koti lake la suti na kutundika juu ya msumari uliokuwa umegongwa kwenye mbao iliyokuwa ukutani, akabaki na tisheti ya kijivu ya mikono mirefu kisha akaketi kwenye kiti na tukawa tunatizaman.

“ Una maanisha nini kusema mimi ndiye muhusika,Unataka kuficha dhambi zako kwa uongo, vita ya mapenzi ipi mimi siwezi toka na mwanafunzi wa hapa”. Akazungumza na kunikazia macho,nikatabasamu kwa dharau na kutizama tizama ofisi yake.

“Nafahamu Vai alikuwa anashika ukuta hapa anainama afu unaweka mbo* yako unamsugua mpaka unaridhika”. Nikazungumza na kumuona akishtuka na kukunja ndita za paji lake la uso.

“ Domy acha kuongea upuuzi na kutaka kupoteza ushahidi siwezi fanya uchafu wa aina hiyo me ni mtu mzima nayejiheshimu kwa ujinga wako nitakufunga”. Akazungumza na mara hii alikuwa mkali zaidi, nikatabasamu na kulegeza tai yangu shingoni kisha nikapandisha mguu wangu juu ya meza, nikamuona uso wake ulivyozidi kujawa na hasira za wazi juu ya dharau nayo muonyesha.

“ Hahhaa Vai familia yake haina uwezo wa kulipa millioni 45 kila mwaka ndani ya hiki chuo,wewe ndiye unayemlipia au huenda anasoma bure kupitia wewe”. Nikazungumza na kumtizama na kumuona ndita zake zikitoweka taratibu kwenye paji lake la uso, akawa mpole na kutabasamu na kutingisha kichwa, hizo pesa zilikuwa zikitolewa kila mwaka na ukimaliza chuo, chuo chenyewe kinakutafutia ajira ndani ya miezi 6 tu unaajiliwa, haina haja ya wewe tena kusumbuka na mavyeti mtaani, bali ni wewe kukaa miezi 6 nakusubiri kuitwa kwenye kampuni au fani yeyote ile uliokuwa unafanya au taasisi yeyote ile ya serikali au mtu binafsi, na ndiyo maana ghalama yake ilikuwa kubwa maana ajira wao wanakutafutia ndani ya miezi sita pekee.

“ Ina maana unanifatilia”?. Akazungumza na kufungua kifungo cha shati lake juu ya shingo alihisi sasa kinambana

“ Hapana siwezi fanya icho”. Nikazungumza

“ Ooh huyu namsomesha kama mwanangu ila siwezi fanya uo ujinga kwa binti yangu”.Akazungumza

“ Nitakuweka ndani Domy iwapo ukiendelea kunambia mambo ya kijinga”.akakazia msumari

“Leo hasubuhi ulimuita chemba na kumuambia atoe mimba kwani chuo chetu,hakiruhusu kuwa na mimba, isipokuwa mahusiano pekee, na endapo ikibainika mtu ana mimba ya mwanafunzi mwenzake watapewa Suspended ya wiki kadhaa ila kama ni mwalimu, au mtumishi yeyote wa hapa basi atafukuzwa kazi na kufungwa miaka miwili gerezani, hukuwa tayari kufukuzwa kazi na kufungwa gerezani endapo Vai akipimwa na kukuta ana mimba na ikajulikana ni yako pale atakapokutaja au mtoto atakapozaliwa, ulimwambia atoe ila Vai alikataa hapo ndiyo mkaanza ugomvi wenu wa kila siku kuhusu yeye kutoa hiyo mimba,”. Nikaa kimya baada ya mlango kubishwa nikamuona mkuu wa uchunguzi akitumbua macho na kujiuliza mambo hayo nimejuaje.

“ Ingia”. Akazungumza huku akijitoa wasi wasi wake,mlango ukafunguliwa na akaingia makamu wa chuo, alikuwa ni mwanamke mwenye umbo kubwa na la kuvutia sema umri wake ulikuwa miaka kama 50, aliponiona akanikonyeza kisiri siri kwani alikuwa akinitaka kila siku ila nilikuwa simjibu text zake na sijuhi namba yangu alipatia wapi?.kwani nayotumia haijaunganishwa na chuo kama namba nyengine ambazo kila mwanachuo namba yake ipo makao makuu ya chuo kama ikitokea ana shida yeyote imemkumba yupo nje ya chuo ilitakiwa kuipiga namba hiyo,au kama chuo chenyewe kinamuhitaji.

Alikuwa na Pc ( laptop) ya kijivu mkononi mwake akainama karibu yangu na kumgeuzia yule mkuu wa uchunguzi ambaye jina lake ni MR DERICK

“ Kuna kitu kimenishinda hapa kutoa ilo faili”. Akazungumza na kufanya nitabasamu kwani ingembidi aende upande wa nyuma au mbele ya Mr derick ili kumuonyesha faili hilo, Zaidi ya alichokifanya ni kubinua makalio yake ili tu niyaone.

“ Naondoka”. Nikazungumza na kupiga makalio yale kofi na kufanya wote kushangaa.

ITAENDELEAAA…………..

( THE STORY MASTER)


LOVE IS A DRUG ABUSE******
 
SEHEMU YA TANO


Wakanishangaa kwa kitendo nilichokifanya kwa makamu wa chuo kwa kupiga makalio yake kofi na kufanya yatingishike,lilikuwa ni jambo kubwa la aibu na dharau nililolifanya kwenye mwili wake na ilinistahili kupewa suspended ya miezi au hata kufukuzwa chuo na kufunguliwa kesi ya udhalilishaji.

“Domy!!”. Mr derick akazungumza na kusimama kwani jambo ilo nimelifanya mbele yake yeye kama mtu aliyekatika upande wa kutatua changamoto kama hizo ndani ya chuo, Nikamtizama na nikasimama, nilikwisha toa mguu wangu juu ya meza pale baada ya mlango kubishwa na ndiyo akaingia makamu wa chuo ilo asigundue chochote,Makamu wa chuo akanipiga kofi la uso lililojaa vizuri mashavuni mwangu n ninahisi huenda liliweka mpaka na alama za vidole vyake, akanipiga na la pili huku kifua chake kikipanda na kushuka

“ Andika barua ya jambo ili ulilolifanya na kamati itakupa adhabu ambayo hujawahi kuipata”. Akazungumza na kuchukua laptop yake na kuanza kuelekea mlangoni nikageuka na kutizama makalio yake yanavyotingishika alikuwa na ushawishi mkubwa shida alikuwa na umri mkubwa ambao alikuwa ana uwezo wa kuniita mwanangu au mjukuu.

“ Sawa”. Nikazungumza na mimi naye nikafuata kutoka humo ndani huku nikijisemea hakuna barua yeyote takayosumbuka kuiandika, nikawa nasikia Mr derick akiniita kwani jambo langu na lake halijaisha liliishia njiani kwahiyo alitaka tuyamalize, sikumsikiliza kwani tayari nilikuwa nishapandwa na hasira ya kupigwa makofi japokuwa nilistahili hata kuchapwa viboko vya kutosha,sasa moyo wangu ulikuwa umevulugwa nilichohitaji ni kuona mtu akilia mbele yangu au akiumia mbele yangu ili nipate faraja kwani akili yangu ilikuwa imeathirika kisaikolojia toka nikiwa mdogo nilisuihudia mama yangu akipigwa kila siku, nilishuhudia mambo ya kikatili makubwa toka kwa baba yangu.

“ Ray ulikuwa wapi leo”. Nikazungumza baada ya kukutana na Ray amabaye alikuwa anaelekea darasani hakunijibu akanitizama shavuni na kutoa macho kwa mshangao

“ Duuh umekuwaje nani kafanya ivyo”. Akazungumza huku akionekana kunishangaa, nikajitizama kwenye kioo cha dirisha na kuona alama za vidole za makamu wa chuo,

“ Mlete mtu yeyote leo usiku nahitaji kupiga mtu”. Nikazungumza na kuondoka kuelekea kwenye bweni letu la kulala wakati nikielekea huko, macho yangu yakatua kwa msichana mrembo ambaye sikuwahi kumuona kabisa chuoni hapo, alikuwa mrefu wa kimo cha kawaida,nywele zake zilikuwa nzuri ndefu na nyeusi tii urembo wa sura yake hulikuwa hauelezeki alivutia kwa weusi wake unaong’aa alikuwa kama mtu wa bara la Asia, mwenye ngozi nyeusi huenda wazazi wake walichanganya rangi alivutia kila nilipomtizama, lakini akili yangu ilitoka huko kwani mambo kama hayo sikuyapendelea niligundua huyo ndo mwanafunzi mpya ambaye ray alikuwa akinieleza kuwa anakaa mbele ya kiti changu, kweli alikuwa mzuri. Nikampita na nikasikia harufu kali ya manukato toka kwake, nikasimama na kumgeukia alikuwa amekaa kwenye benchi huku akionekana kuandika kitu kwenye kijitabu kidogo, mwanzoni nilipomtizama alikuwa amesimama ila kwa sasa alikuwa amekaa kwenye benchi.

“ Ukitaka kukaa kwa Amani badili hayo manukato”. Nikazungumza,akaonekana kunishangaa akatizama nyuma na kushoto akama kuna mtu nasema naye.

“ Unazungumza na mimi?”. Akazungumza na kufanya nione meno yake yaliyopangika vyema pia alikuwa na mwanya juu

“ ndiyo wewe hapo”.

“ tiih We kama nani ?”. Akazungumza

“ Sihitaji kurudia badili manukato yako ni mabaya”. Nikazungumza huku nikikunja ndita kwani nina historia nzito kuhusu manukato hasa yale yenye harufu ambayo kwangu naona ni mbaya.

“ We kaka vipi kuwa na heshima”. Akazungumza na kunyanyuka sasa nikaona kifua chake chuchu zilisimama dede hazikuwa zimeshuka kama ndala, sikuona kama kuna dalili yeyote ile ya sindiria( sidiria)

“Naomba niondoke”. Nikazungumza

“ ishii kwani nimekushika we vipi kazi kuharibu mood za watu au umetumwa”. Akazungumza na kufanya nimgundue kuwa ana mdomo licha ya uzuri wake wote au huenda alichukia kumwambia manukato yake mabaya.

Sikimjibu zaido ya kuondoka na kumuacha akinifyonza fyonza nikajiapizia usiku wa leo lazima limkute jambo nikakumbuka mwaka uliopita baada ya kumdhalilisha mwanamke kwa kumrekodi kifua chake kikiwa wazi na kurusha video hiyo iliyosambaa ndani ya chuo chote na kuzua taharuki juu ya uzalilishaji huo, kitendo kilichoperekea msichana huyo kutaka kujiua ila wakamuwahi na kumuamisha chuo huku video hizo zikifutwa na kuzuiwa kabisa kuingia mitandaoni, kesi hiyo ilikuwa kubwa muhusika alitafutwa kama miezi miwili ambaye ndiye mimi na ndipo nikaanza kujuana na Mr derick na akanza kuniwinda kila kesi ila uwa nazishinda, ndani ya begi langu uwa na kinyago ambapo nikimchukua mwanamke video ili kumdhalilisha nahakikisha yeye anitambui wala wanachuo wote, ijapokuwa mr derick alishanitambua ila ushahidi wa kunikamata hana, sasa nilitaka leo nikivae itakapofika usiku muda wa chakula na kwenda eneo la jengo ambalo uwa nafanyia ukatili wangu, jengo ilo uwa linamwanga hafifu na pia ni kama limetelekezwa lipo pembezoni kidogo lilipojengo kubwa la darasa letu, jengo hili linasadikika ilikuwa maabara ila iliungua na moto, na wanataka kuja kulijenga upya. Nilitaka muda ukifika niende na kuku wangu ndani ya jengo hilo ili kutimiza matakwa yangu na kuku wangu nilikwisha mlenga binti huyo mgeni,”najua wapi pa kumpata..” Nikawaza na kupaka dawa ya kuchua shavuni mwangu huku nikishika shika kinyago changu.

“ Leo usiku kuna sherehe ya miaka 20 ya chuo ichi, kutakuwa na matukio mengi ya watu kuwafanya wawe bize”

Nikazungumza na kukirudisha kwenye begi langu kisha nikarudisha nilipolitoa, nikakumbuka askari walivyoangaika kutafuta kinyago kila bweni ila hawakukipata kwani nilikificha ndani ya jengo lile la maabara.

Nikajilaza kitandani huku nikijaribu kutafuta usingizi ili kupumzisha akili yangu.ghafla mlango ukagongwa wa chumba ambacho nimo ambapo kuna vitanda vitatu, kila room

“ Sitaki usumbufu”.

“ Fungua ni mimi”. Sauti ya rojah ikasikika

“ Unataka nini?”.

“Nilitaka tu kujua kama uko sawa”

“ Usijali”. Nikazungumza na nikamsikia akiondoka nikaanza kutafuta usingizi taratibu na mwisho nikapitiwa na usingizi.


***********

“ Mama wewe ndo msaliti umemsaliti baba”. Nikazungumza na kumtizama yangu, ambaye hakujiuliza mara mbili mbili akashusha kofi zito shavuni mwangu na kufanya nianguke chini, nikanyanyuka huku nikiwa na hasira na moyo ukaingiwa ukatili wa ajabu.

“ Domy unanitizamaje hivyo una roho kama ya baba yako eeh”.. Akazungumza na kuniongeza kofi jengine huku akinifinya mwilini mwangu, nikaanza tokwa na machozi ya uchungu wa kipigo toka kwake

“ umerithi roho mbaya ya baba yako ndiyo kwanza una miaka 10”. Akazungumza na akaanza kutafuta kitu cha kunipiga nacho, akaona kitanda kwenye dressing table yake ya kijilemba, akakishika na kuanza kunipiga nacho kila sehemu aliyotaka kunipiga nililia kwa maumivu makali nayoyapata alinipiga bila huruma,alichanganya hasira zake za kupigwa na baba kila siku na alitaka kuzimalizia kwangu sasa alinibamiza mpaka ukutani na akae endela kunitandika viboko vya nguvu hakikikuwa kitana kidogo kilikuwa kikubwa cha nywele tena kilijaa kama mwiko, akaangaza na kuona mikanda ya baba ikiwa imepangika vizuri sehemu maalumu ya kupangia mikanda, nikataka kutoka mbio ila akanikamata mkono kwa nguvu na kunivuta kisha kunipiga na mikanda yake, halishawahi nikingia hiyo mikanda nisipigwe na baba ila leo yeye ndiyo alinipiga nayo kauli yangu huenda ilimkela zaidi na kumfanya roho yake kuingiwa na unyama juu yangu kwani hakuwahi kunipiga,nikafanikiwa kuchoropoka huku nikitoka chumbani kwake na kukimbilia chumbani kwa dada wa kazi kisha nikajifungia na kuanza kulia kwa uchungu, mwili wangu ulijaa madonda mengi yalitokana na kuchapwa ni mikanda hiyo, mwili ulikuwa umechemka mwili ulikuwa wa moto kupita kiasi moyo wangu uliuma na kuona nimeonewa nililia mpaka nikanyamaza na nikapitiwa na usingizi,

Nikaamka baada ya mlango kugongwa na sauti ya mfanyakazi ikasikika,nikatizama madonda yangu na chuki juu ya mama yangu ikaniingia ghafla kwa akili yangu nikajua mama na baba hawanipendi wote,akili ya kitoto ikanituma kuwa hasira zake alizimalizia kwangu kwa kunipiga pasina huruma, nikanyanyuka na kutaka kufungua mlango ila nikasita baada ya kuona pafyumu ya dada wa kazi ikiwa imeandikwa FLAMMABLE huku umbile la moto kuwaka likiwa limechorwa, roho ya kishetani ikanivaa, nikakumbuka mwalimu wetu alisema tukae mbali na vitu vinavyosababisha moto au mripuko maana sisi bado wadogo na alitaja vitu hivyo ikiwemo pafyumu. Nikaenda na kuichukua kisha kuiweka mfukoni na nikafungua mlango na kukutana na mfanyakazi ambaye akanikumbatia na kufanya machungu yangu yaongezeke zaidi.

“ Mama kalala polee mtoto mzuri sikiliza sasa nenda sebelni nakuja kukuandalia chakula ule sawa domy nisubiri kidogo nioge”. Akazungumza na kunibusu kisha akaondoka yaana akanibusu paji la uso.

Nikaenda chumba cha mama na kufungua mlango taratibu nikamuona akiwa amelala fofofo hasira zikanipanda baada ya kuona picha ukutani ya dada yangu ambaye yupo marekani anasoma tena picha hiyo wakiwa wamemkumbatika wazazi wangu wote wawili hasira zikanipanda kwani mimi sikuwa na picha hata moja, wazo baya likanija nikafata kiberiti jikoni na kirudi chumbani kwa mama, nikamsogelea taratibu na kutizama shuka alilolalia, nikasogea upande wa miguu yake na kuwasha njiti ya kiberiti kwenye shuka moto ukawaka ila ukazima, ndipo nikatoa ile pafyumu na kuanza kupulizia shuka eneo lile na nikawasha moto na shuka likawaka nikaanza muona mama akijigeuza geuza, nikatoka na kufunga mlango kwa nje, ndani ya dakika 5 nikachungulia kupitia tundu la ufunguo nikaona moshi mwingi umejaa ndani na harufu mbaya ikaanza kusikika harufu ya pafyumu ile sasa ikawa mbaya,nikamuona mama akikohoa kwa tabu alifanikiwa kuzima moto ila moshi mwingi ulimfanya akoe na kutaka kutoka ndani akawa anashika shika kitasa bila mafanikio yeyote roho yangu nikahisi sasa inatulia.

“ Domy unafanya nini una muua mama, mama anaumwa PUMU”.(pumu tatizo la kutovuta hewa kwa muda kwahiyo utahitaji kifaa hili uvute afu uendelee kupumua lasivyo unakufa.). Dada wa kazi akanitoa kwa nguvu na kufungua mlango ule na funguo nilizokuwa nazo, mama alikuwa tayari ameshazima sijuhi yani kama mzima au amekufa, nikaanza kulia na kumuita jina, akili ikaanza kuchanganyikiwa nikaanza kujuta kwa tukio nililolifanya dada wa kazi akabinya alamu ukutani, na ikaanza kupiga kelele moshi mkubwa wenye harufu kali ulikuwa umejaa, nikaanza kumtingisha mama bila mafanikio yeyote, yule dada wa kazi akaleta kifaa na kumuwekea mdomon na puani akaanza kukibinya binya kama dakika 3 hivi mama akaanza kupumua na ghafla jopo kubwa la watu wa huduma ya kwanza wakaingia ndani na kumtoa huku mimi nikifata kwa nyuma nikiwa na kopo langu la pafyumu………


*********

MLANGO ukagongwa na kufanya nishtuke toka usingizini na kwenye ndoto ya tukio la miaka mingi iliyopita.

“ N..ani”. Nikauliza huku nikijinyanyua taratibu

“ Ni mimi Ray toka nje asee unalala sana”

“ saa ngapi?”

“ Inaenda saa moja “.

“ duuh watu washavaa sare zaoza sherehe”.

“ ndiyo oga chapu afu fungulia wenzako wanataka kuoga wajiandae”.

“Powah”. nikazungumza na kutabasamu kwani leo nilitaka kufanya ukatili kwa yule mwanamke mgeni na kinyago nilikwisha kiandaa cha kuficha sura yangu


ITAENDELEAAAAAA.

(THE STORY MASTER)



“ LOVE IS A DRUG ABUSE”........
 
Nahisi mimi ndo mtu addicted sana na story.
Leta vitu mkuu 🔥
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…