Lost in Translation! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lost in Translation!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rev. Kishoka, Apr 24, 2008.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Apr 24, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  I wrote this piece almost 2 years ago. It still holds its value the only thing I would have added was Ufisadi.

  Lakini I am sticking to the core theme, Taifa being Lost in Transition, hence Translation!

   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Apr 24, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Why don't you go run for political office so you can effectively effect the change you wish to happen..?
   
 3. M

  Mkandara Verified User

  #3
  Apr 24, 2008
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Nyani Ngabu,
  Time... time wil tell... Tik..tak.. tik..tak!
  Rev Kishoka,
  U know what, I think there might be a good chance for the re birth of Ujamaa Party!...following Mwalimu nyayo...I can sense winning election big time.
   
 4. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #4
  Apr 24, 2008
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  We seriously need such characters to run the political offices, today than ever!
   
 5. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #5
  Apr 24, 2008
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ..rev,

  ..niliposoma hii nikakumbuka article ya jenerali wiki hii.

  ..that got me thinking about ujamaa!

  ..its not like sipendi ubepari au la,nadhani uchumi wowote unaotaka kukua vizuri hii leo lazima uwe na some sort of free market dynamics. huku kwetu tumeuvamia huu mwelekeo bila kujua kwamba unahitaji kusimamiwa na kuangaliwa kwa karibu ili kusiwe na abuses of the system [free market economy].

  ..tukija kwenye upande mwingine,uchumi wa rural areas hauwezi endelea bila some principles za ujamaa. hawa watu wanahitaji kushirikiana na kushirikishwa pia.

  ..i believe,in some areas lazima serikali iwe na the upper hand na hapa naongelea big public investments ambazo mostly huwa na faida za kiuchumi zaidi kuliko kibiashara.
   
 6. Bin Maryam

  Bin Maryam JF-Expert Member

  #6
  Apr 24, 2008
  Joined: Oct 22, 2007
  Messages: 685
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mkandara:

  Kuna kitabu The Fate of Africa: A History of Fifty Years of independence by Martin Meredith.

  Nakuomba kajipatie kopi na usome kuhusu huo ujamaa. Katika kitabu mwandishi anaonyesha bayana kuwa baada ya kuanza Ujamaa, uzalishaji katika sekta zote muhimu ulikufa. Katika kipindi hicho-hicho Tanzania ilipokea misaada ya zaidi ya billioni 6 USD kutoka kwa wafahisani mbalimbali. Kwa mtaji huu mwandishi anasema mafanikio yaliotokana katika kipindi cha ujamaa hayakutokana na mafanikio ya siasa zenyewe bali ni matokeo ya misaada ya kutoka nje kitu ambacho nakubaliana naye kwa asilimia 110.
   
 7. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #7
  Apr 24, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Nyani,

  Jiandae kukomba kadi nambari 3 ya chama changu kipya cha Social Democrats (DP) ambacho kitaanza kazi rasmi Januari 1 2011.

  NIkirudi kwenye hii hoja on serious note, Viongozi wetu walituacha solemba walipofikia uamuzi wa kukimbilia mfumo wa soko huria au ubepari.

  Si kwamba kuingia kwenye mfumo huo kulikuwa na ubaya, bali makosa yale yale yaliyotumika wakati tulipoingia Ujamaa walitumika tulipodandia mfumo mpya.

  Jamii na Taifa yalipewa hotuba laini na kuambiwa sasa hivi kila mtu na lwake na viongozi wanaweza jipatia mali za ziada.

  Hapakuwa na kampeni maalum ya kushirikisha na kuwaanda wananchi ili wawe tayari kuingia katika huu mfumo mpya wa "changia mwenyewe"!

  Mtanzania bado anaimba nyimbo za kijamaa, anaishi maisha ya kijamaa, lakini Serikali yake inajiendesha na kufanya mambo kwa kutumia mfumo mpya. Migongano inayoanza jitokeza katika jamii kama huu wa sasa UDSM au kule Buzwagi, ni matokeo ya Serikali kujifanyia mambo kwa kigezo cha dhamana ya kuongoza na hivyo kuburuza kila mtu.

  Ikiwa tunakiri tulifanya kosa hili la kuburuza wananchi 1967, 1974-76 na hata katika utekelezaji wa mambo mengine ya muhimu kwa Taif na jamii, basi ni tofauti gani iliyopo iliyotokea 1992 mpaka leo?

  Tunakimbilia kuuza kila kitu, viongozi wetu wanakimbilia kujitajirisha kwa njia fupi na za haraka, lakini mwananchi wa kawaida anaambiwa "kaza misuli, gurudumu la maendeleo ni zito kupanda mlima"!

  Si kwamba natetea ujamaa au kusema ujamaa ni mfumo bora, bali ni kuwa wananchi wamepotezwa kwa makusudi ili waendelee kushangaa feri huku watawala ambao ni watendaji wa serikali na makuwadi wao kwenye mashirika wakiendelea kujijengea temi, koo na falme ndogo ndogo za kitajiri hivyo kumfanya huyu mwananchi aendelee kutegemea serikali milele na kuishia kuwa masikini wa kubuhu huku akitukanwa kuwa ni mvivu na mwenye wivu wa kike!

  Natamani siku mwananchi huyu ageuke na kuwa na wivu wa kiume na kumfuata mtesi wake!
   
 8. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #8
  Apr 24, 2008
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ..bin maryam,

  ..ujamaa kama ujamaa hauna tatizo. utekelezaji wake na interpretations ndo tatizo!

  ..kwa mfano,nini kilitufanya tuamini kwamba tunaweza taifisha mali za wazungu na kuziendesha vizuri wakati soko wanalijua wao na liko kwao!. mbaya zaidi mitambo na tekenolojia ni yao na wanaizalisha wao!that was poor planning and it's the one thing we keep on doing over and over!

  ..lakini,watu maskini wasio na mtaji mkubwa,wakijiunga kwa hiari na kufanya miradi ya maendeleo kwa msaada wa serikali,huo ni ujamaa! wanaunganisha nguvu kwa faida ya maendeleo yao!

  ..ujamaa hata huko ulaya upo! and don't get me wrong,i'm not talking about marx's socialism or communism.
   
 9. Bin Maryam

  Bin Maryam JF-Expert Member

  #9
  Apr 24, 2008
  Joined: Oct 22, 2007
  Messages: 685
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Dar Si Lamu:

  Wazungu hata wakifuata udikteta bado wataendelea tu. Jamii zao zimeshavuka viwango fulani vya maarifa na mitaji na kuwafanywa kuwa na luxury ya kuchagua siasa gani wafuate.

  Kwa upande wetu, tunajaribu kukopi vya wenzetu hili vikubalike katika mazingira yetu na bado tunachemsha na matokeo yake ni kuwa na serikali kubwa zenye watumishi wasiotoa mchango wowote kwa jamii na kuzidi kutegemea misaada kutoka nje.
   
 10. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #10
  Apr 24, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Kosa letu ni kukataa kukubali makosa yaliyopita, kujirekebisha na kuchanganua yale tuliyoshindwa kwa kuyarekebisha na kuyapa mtazamo mpya.

  Sisi tunakimbilia kuanzisha kitu kipya kabisa bila kurekebisha kasoro ya lile la awali!
   
 11. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #11
  Apr 24, 2008
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Wenye wajibu wa kuwaelimisha wananchi ili tuweze kufanya mabadiliko ni akina Prof. Mkandala, ambaye watoto wa milimani wamemshinda unafikiri ataweza kuwaelimisha wananchi mil.38, nafkiri we have a long way to go, kuakikisha watanzania wanaelewa tumefanya wapi makosa na kuyalekebisha. Tunatakiwa kuangalia tulijikwaa wapi na kuakikisha tunavyoanza upya hakuna kukanyaga hapo tena.
   
 12. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #12
  Apr 24, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Jamco,

  Hali ya sasa wajibu ni wa kila mtu, si Serikali pekee au "wanene" fulani ambao ni viongozi.

  Ndio maana Jambo Forum ni kinara katika kuelimishana na kubadilishana mawazo ingawa wengine wanachukulia kuwa JF ni mahali pa watu wenye hasira na Serikali.

  Tumechoka kusubiri na kukumbushwa na Nyani Ngabu kuwa ndivyo tulivyo, tunaanza wote kushiriki katika ujenzi wa Taifa kwa hali, mali na fikra.
   
 13. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #13
  Apr 24, 2008
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ..na hiyo yote yatokana na uvivu na kung'ang'ania mambo yasiyokuwa na faida dhahiri kwetu!

  ..jambo likiwa gumu tunalihepa na kukimbilia linaloonekana rahisi!kama hii misaada toka nje. wakati tulihitajika kufanya kazi ngumu ya kukuza mapato yetu wenyewe!na tena ya muhimu ni haya ya ndani!
   
 14. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #14
  Apr 24, 2008
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Umefika wakati wa kuwabana viongozi wetu wakati wanagombea watuambie kabisa wanategemea nini wakati wa uongozi wao katika namba nafikiri itakuwa vizuri kuwakamata wapotoka madarakani na kuwaambia kuwa hawakutimiza walichokisema, mfano JK tutamuuliza siku zake za mwisho atuambie hizo ajira mil. 1 ziko wapi atupe figure sio makisio.

  Kampeni za wenzetu unaona kabisa hata mwelekeo wa budget ya serikali husika kwa miaka watakayokuwa madarakani ikoje maana wanasema wataongeza nini na kupunguza nini kwa namba.
   
 15. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #15
  Apr 24, 2008
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ..huko ndiko tunakoelekea. hii "dhambi" ya bunge kufichua maovu inatapakaa taratibu kwa wananchi. watu hawana illusions tena!

  ..na tutakapoanza kuuliza hayo ndio tanzania itakuwa huru. wakati wa ukombozi ni sasa!
   
 16. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #16
  Apr 24, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Natamani sana siku Mkuu wa nchi anafanya mahojiano na Waandishi wa habari aulizwe ni lini Tanzania itaacha kutegemea 50% ya bajeti yake kutegemea fedha za wafadhili? NI lini Tanzania itaacha kuwa Matonya? NI lini Serikali itakaza mkanda na kupunga matumizi na kulenga mgao wa bajeti kuelekea katika maendeleo?
   
 17. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #17
  Apr 24, 2008
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Mkuu ili linawezekana kinachotakiwa ni nia ya kweli ya kushughulikia watu wasio waaminifu serikalini, resources ni nyingi sana ukianzia na mali asili, madini, na subortage kwenye tuviwanda twetu tulivyonavyo, Rushwa inasababisha serikali inakosa mapato mengi sana, kama juhudi zinafanywa na kuakikisha kuwa sehemu zote hizi zinachangia tunaweza kuendesha budget yetu wenyewe.
   
 18. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #18
  Apr 24, 2008
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ..jibu la swali hili liko wazi. atasema "hivi sasa tunajitahidi kuongeza mapato yetu ili kupunguza utegemezi,kwani si vizuri kutegemea sana wafadhili. wakati mwingine hawatimizi ahadi zao. kwahiyo,suala hilo tayari linafanyiwa kazi"

  ..kama namwona vile,akitoa hilo jibu. infact,naisikia sauti yake masikioni!
   
 19. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #19
  Apr 24, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Jamco,

  Tukianza kumbugudhi mkuu wa kaya kila siku na kumkera kuhoji ni lini tutaendela, labda ataamka na kufanya halaiki ya nguvu kwa askari miavuli wake na watu tutaanza kuona matokeo.

  Tusipombugudhi kila siku, yeye atakaa mkao wa kula na kuhisi kila kitu ni mswano na kuendelea kulonga Hamsindile Hamnoga!
   
 20. Bin Maryam

  Bin Maryam JF-Expert Member

  #20
  Apr 24, 2008
  Joined: Oct 22, 2007
  Messages: 685
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Dar Si Lamu:

  Maamuzi ya kupunguza matumizi kwanza yatahitaji kubadilisha mfumo mzima wa utawala kwa kupunguza idadi ya wilaya, majimbo ya ubunge, mikoa na nafasi nyingi za kazi. Sidhani kama kuna viongozi wa kisiasa watakaokubali kuchukua hatua hizo.
   
Loading...