Lost in Translation!

D

DAR si LAMU

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
2,940
1,500
Dar Si Lamu:

Maamuzi ya kupunguza matumizi kwanza yatahitaji kubadilisha mfumo mzima wa utawala kwa kupunguza idadi ya wilaya, majimbo ya ubunge, mikoa na nafasi nyingi za kazi. Sidhani kama kuna viongozi wa kisiasa watakaokubali kuchukua hatua hizo.
..i concur !
 
Rev. Kishoka

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,536
2,000
..jibu la swali hili liko wazi. atasema "hivi sasa tunajitahidi kuongeza mapato yetu ili kupunguza utegemezi,kwani si vizuri kutegemea sana wafadhili. wakati mwingine hawatimizi ahadi zao. kwahiyo,suala hilo tayari linafanyiwa kazi"

..kama namwona vile,akitoa hilo jibu. infact,naisikia sauti yake masikioni!
Wakirudi majimboni, Wananchi wawaulize Wabunge ni lini wilaya na majimbo yao yataanza kujiendesha kwa fesha zao wenyewe an si kutegemea saidia Serikali kuu na Wafadhili?

Waulize kwa nini hakuna mipango ya kuhakikisha kuwa 70% ya pato kutoka Wialaya linarudi wilayani kwa shughuli za maendeleo kama elimu,afya, maji, ajira na menginewe?
 
D

DAR si LAMU

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
2,940
1,500
Wakirudi majimboni, Wananchi wawaulize Wabunge ni lini wilaya na majimbo yao yataanza kujiendesha kwa fesha zao wenyewe an si kutegemea saidia Serikali kuu na Wafadhili?
..hili litakuwa gumu kwao! si unajua implication yake? more taxes and wananchi will have to work harder than before!

Waulize kwa nini hakuna mipango ya kuhakikisha kuwa 70% ya pato kutoka Wialaya linarudi wilayani kwa shughuli za maendeleo kama elimu,afya, maji, ajira na menginewe?
..hapa unaweza toa impression ya u-majimbo! on this i'm not taking positions!
 
Bin Maryam

Bin Maryam

JF-Expert Member
Oct 22, 2007
685
0
..hili litakuwa gumu kwao! si unajua implication yake? more taxes and wananchi will have to work harder than before!..hapa unaweza toa impression ya u-majimbo! on this i'm not taking positions!
Naomba ufafanue hapa kuhusu u-majimbo. Maana wakati mwingine sisi ni specialists wa kuwa na wasiwasi na vitu ambavyo havijawahi kujaribiwa. Kwa mfano kwa kuondoa umajimbo zikajengwa shule za sekondari za mabweni zenye kusomesha watu wachache sana. Na kama pesa za shule hizo zingetumika kwenye shule za day, nchi ingeweza kusomesha watu wengi.
 
D

DAR si LAMU

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
2,940
1,500
Naomba ufafanue hapa kuhusu u-majimbo. Maana wakati mwingine sisi ni specialists wa kuwa na wasiwasi na vitu ambavyo havijawahi kujaribiwa.
..wilaya ya kilindi na arumeru zinalingana kimapato?

..the argument is that,kutakuwa na maendeleo yaliyokuwa skewed kwa wale wenye mapato makubwa zaidi. hii inanikumbusha geita na kahama!


Kwa mfano kwa kuondoa umajimbo zikajengwa shule za sekondari za mabweni zenye kusomesha watu wachache sana. Na kama pesa za shule hizo zingetumika kwenye shule za day, nchi ingeweza kusomesha watu wengi.
..honestly,i'm lost here!
 
Rev. Kishoka

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,536
2,000
Dar si Lamu,

Unajua ukisukuma responsibility kwa wilaya au majimbo kutatokea competition ya hali ya juu? We are past enzi za kuoneana aibu. It is sad kuwa wengine are not pulling their weight kwa kuwa wanategemea handouts kutka Serikali.

Mfano mzuri ikiwa Dodoma na Singida wakiona mikoa jirani Arusha, Tabora na Morogoro wanapeta kutokana na uwekezaji wa jasho la wananchi wao kurudi katika wilaya zao kwa manufaa yao, basi ujue kuwa nao Wagogo, Warangi, Wanyiramba na Wanyaturu wataamka.

Si tumesema tumeingia katika mfumo huria? basi fungu la maato kutoka kila wilaya ligawiwe kutokana na uzalishaji mali wake. Ikiwa Bariadi na Sengerema wataendelea zaidi kutokana na maeneo yao kuwa na uchumi mzuri kutokana na uchimbwaji madini, kwa nini wasineemeke wao zaidi na si ununuzi wa ma-VX ya mawaziri na safari uchwara za kila siku za viongozi wa Serikali?
 
J

Jamco_Za

JF-Expert Member
Jul 14, 2007
1,333
1,225
You are right Rev. Kishoka kwani mashindano yataleta maendeleo zaidi, angalia huu utaratibu wa kutoa ruzuku kwa vigezo furani atleast kuna mabadiliko kidogo kwenye local government kulingana na report ya CAG
 
Rev. Kishoka

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,536
2,000
Jamco,

At one point tunalalamika kuwa tumechoka ujamaa. Lakini hatutaki kubadilikwa kuachana na ujamaa.

Ukisukuma chini nguvu za maendeleo ya watu kurudishwa mikononi mwao wenyewe, trust me kutatokea mashindano kama Simba na Yanga na utaona wale wenye kujivutavuta wakitafuta mbinu za kuongezeka kwa vipato wao.

Tulete mashindano ya mkoa na hata wilaya kama mwashowasho kusisimua shuhuli za maendeleo na hata kutoa ruzuku nishani kwa maeneo yanayotumia vizuri mapato yake na kupunguza matumizi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom