LORl LACHINJA SABA TANGA.

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,850
155,786
WATU saba wamekufa papo hapo na wengine wanane kujeruhiwa katika ajali ya lori iliyotokea usiku wa kuamkia jana wilayani Handeni, Tanga.


Habari zilizolifikia gazeti hili jana zimeeleza kuwa lori hilo aina ya Fuso lililobeba abiria 15 kutoka Dar es Salaam kuelekea Moshi, mkoani Kilimanjaro, liliacha njia na kupinduka katika kijiji cha Kitumbi.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Liberatus Sabas alisema ajali hiyo ilitokea saa 5:00 usiku wa kuamkia jana.


Kamanda Sabas alifahamisha kuwa watu sita kati ya hao ni wanaume na mmoja ni mtoto wa kike mwenye umri wa miaka mitatu


Alisema miili ya waliokufa katika ajali hiyoimehifadhiwa katika Hospitali ya Magunga Korogwe.


"Majeruhi akiwemo utingo gari hilo pia wamelazwa katika hospitali hiyo, lakini dereva wa gari hilo ametorokana naakwamba, polisi wanaendedelea kumtafuta," alisema Kamanda Sabas.


Ajali hiyo imetokea siku chache baada ya watu wengine 15 kupoteza maisha na wengine 48 kujeruhiwa vibaya katika ajali iliyotokea wilayani Kondoa mkoani Dodoma.


Ajali hiyo ilitokea saa 1:00 asubuhi kwenye Kijiji cha Mnenia kilicho kilomita 30 kutoka Kondoa mjini mkoa wa Dodoma wakati lori moja lilipoacha njia na kupinduka.




Wakati huo huo, Mussa Mwangoka anaripoti kutokan Sumbawanga kwamba, watu watatu wamefariki dunia katika matukio matatu tofauti ya ajali za barabarani zilizotokea mkoani Rukwa.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Isuto Mantage ajali hizo zilitokea Julai 11. mwaka huu na kati ya hizo mbili zilizosababisha vifo vya watu hao zilihusisha pikipiki.

Alisema kuwa ajali ya kwanza iliyotokea katika kitongoji cha Mazwe kwenye makazi ya wakimbizi ya Mishamo wilayani Mpanda, abiria Adonikana Ezekiel (22) alifariki dunia baada ya pikipiki aliyokuwa ameipanda kuacha njia na kupinduka.
Alisema kuwa katika ajali hiyo mwendesha pikipiki alinusurika na kupata majeraha kidogo lakini anaendelea vizuri.


Katika ajali nyingine ya pikipiki iliyotokea Manispaa ya Sumbawanga kwenye kitongoji cha Mollo, Bwana mifugo wa kata ya Mollo James Mrema (35) alifariki dunia papo hapo baada ya pikipiki aliyokuwa akiendesha kuacha njia na kupinduka.

Kamanda Mantage aliongeza kuwa katika tukio lilitokea huko katika kijiji cha Mtimbwa Manispaa ya Sumbawanga, barabara ya Matai – Sumbawanga, lori aina ya Fuso liliacha njia na kupinduka na kusababisha kifo cha mtu mmoja ambaye hakuweza kufahamika mara moja.

Katika ajali hiyo watu watano walijeruhiwa na kupata matibabu katika Hospitali ya Mkoa ya Sumbawanga na kuruhusiwa baada ya hali zao kuendelea vizuri.

SOURCE: MWANANCHI
 
Ajali Ajali Ajali!
Mungu atupishie Mbali.
Poleni wafiwa!
Uponyaji wa haraka kwa wahanga
Mungu ibariki Tanzania.
 
kweli lori limetoka dar limepakia watu na kuruhusiwa na trafic wapite bila kuzuiliwa? labda kitu kidogo! ila atakuwa ametoa sana maana kuna viziuizi vingi sana barabarani, du poleni sana wafiwa
 
Back
Top Bottom