Loliondo in Pictures












... ... . Tiba ya Mchungaji Mstaafu wa KKKT, Ambilikile Masapile ‘Babu’ anayotoa huko Loliondo, Arusha inadaiwa kuingia hatua ya pili baada ya hivi karibuni kufanya maajabu zaidi. Kwa mujibu wa shuhuda wetu, maajabu ya tiba hiyo yaliwakuta wanawake wawili, mmoja ambaye jina lake halikupatikana mara moja, alitapika nyoka muda mfupi baada ya kunywa dawa ya Babu na kuibua hisia kali miongoni mwa watu waliokuwa kwenye foleni wakisubiri huduma. Shuhuda huyo alisema kuwa, mwanamke mwingine aliyejulikana kwa jina moja la Saumu, yeye alijikuta akijifungua ‘minyama’ (kama steki ya ng’ombe) baada ya kupata kikombe hicho cha Babu Masapile. Alisema kuwa, awali, mwanamke aliyetapika nyoka alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya tumbo yasiyo na mfano ambapo ameshakwenda hospitali mbalimbali, ikiwemo kwa waganga wa kienyeji bila mafanikio.


Aliendelea kudai kwamba, siku ya tukio, mwanamke huyo, baada ya kunywa dawa ya Babu, saa chache baadaye alianza kuhisi kichefuchefu kilichoambatana na kutema mate kwa wingi. “Alianza kusikia kichefuchefu, akawa anatema mate, mwisho ikaja hali ya kutapika, ndipo nyoka mweupe alipotoka kinywani mwake na kuangukia chini,” alisema shuhuda. Alisema, baada ya tukio hilo, mwanamke huyo alijisikia mzima wa afya na kuamini amepona tatizo la tumbo lililomtesa miaka nenda, rudi. Aliendelea kusimulia kuwa, kwa upande wake, Saumu, yeye alikuwa kwenye foleni akifukuzia kikombe cha Babu kutokana na matatizo ya kutopata ujauzito tangu ameolewa. Alidai kwamba, saa chache baada ya kunywa dawa ya Mchungaji Masapile, alianza kuhisi tumbo kuvimba na kuwa kubwa mfano wa mjamzito. Shuhuda huyo alisema kuwa, ilifika mahali alipoeleza anavyojisikia, baadhi ya wanawake walimwambia ni mimba jamko ambalo lilisumbua akili ya Saumu akiamini haiwezekani apate ujauzito baada ya kupata kikombe. Aliendelea kudadabua kwamba, baada ya tumbo kukua zaidi, alianza kuhisi maumivu makali ambapo alipoyasimulia, wanawake walimwambia ni dalili ya uchungu wa kuzaa. Alidai kuwa, kilifika kipindi kingine kwa mwanamke huyo ambapo alisaidiwa ili ajifungue lakini cha ajabu, lilitoka pande la nyama kama kilo moja ya steki ya ng’ombe na kuwafanya watu kubaki vinywa wazi.​



Baadhi ya watu walioshuhudia matukio hayo walisema kuwa, sasa wanaamini dawa ya Babu inaponya hata magonjwa ya kurogwa wakidai matukio yote mawili ya wanawake hao yametokana na nguvu za giza.


“Hawa matatizo yao si ya kidaktari, itakuwa nguvu za giza. Naamini dawa ya Babu inaponesha hata mtu aliyerogwa,” alisema mwanaume mmoja ambaye yuko kwa Mchungaji huyo kwa ajili ya mkewe anayesumbuliwa na presha mara kwa mara. Hivi karibuni, Babu alitamka kuwa, ili mtu apone kwa kutumia dawa yake anatakiwa kutanguliza imani ya kiroho huku akijifagilia kwamba, tiba yake ina mkono wa Mungu kwa asilimia mia moja.​



Maandiko Matakatifu ya Wakristo (Babu ni muumini wake) yanasema kwa Mungu hata nguvu za giza zinashindwa.​

 
<table style="TEXT-ALIGN: center; MARGIN-LEFT: auto; MARGIN-RIGHT: auto" class="tr-caption-container" align="center" cellpadding="0" cellspacing="0"><tbody><tr><td style="TEXT-ALIGN: center"> </td></tr><tr><td style="TEXT-ALIGN: center" class="tr-caption">BABU AKIADA DAWA KWA AJILI YA WATEJA WA KE</td></tr></tbody></table>

 
<table style="TEXT-ALIGN: center; MARGIN-LEFT: auto; MARGIN-RIGHT: auto" class="tr-caption-container" align="center" cellpadding="0" cellspacing="0"><tbody><tr><td style="TEXT-ALIGN: center"> </td></tr><tr><td style="TEXT-ALIGN: center" class="tr-caption">BABU AKIADA DAWA KWA AJILI YA WATEJA WA KE</td></tr></tbody></table>

Vikombe hivyo, lolz
 
<table style="TEXT-ALIGN: center; BACKGROUND-COLOR: #0c343d; FONT-FAMILY: Times, 'Times New Roman', serif; COLOR: white; MARGIN-LEFT: auto; MARGIN-RIGHT: auto" class="tr-caption-container" align="center" cellpadding="0" cellspacing="0"><tbody><tr><td style="TEXT-ALIGN: center"> </td></tr><tr><td style="TEXT-ALIGN: center" class="tr-caption">HUU NDIO MTI UNAO TOA UPONYAJI



</td></tr></tbody></table>

 
Wenye kuona kuwa inafaa bila kushinikizwa kufanya hivyo fanyeni isipokuwa msilazimishwe..
 
Back
Top Bottom