Lol yamenikuta

Fundi mahiri wa Ujenzi

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2012
Posts
5,048
Reaction score
4,449
Salaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaam..................

Yamenikuta jamani.

Nikweli nampenda kwa dhati hata yeye ananipenda kwa dhati kiufupi ni kwamba tumeshibana
I mean we are in deep love. Hivi karibuni tumekuwa tukifanya mipango ya kufunga pingu za maisha
Kinachonitesa ndugu zangu ni hiki.....Juzi nimegundua kwamba mpenzi wangu alikuwa na mahusiano na mjomba wangu.

Nimelijua hili baada ya uncle kurudi toka masomoni huko china. Ilikuwa hivi:...nilikuwa niko maeneo tulivu na mpenzi wangu, simu ya mpenzi wangu iliita, kwakweli hakusita kuipokea katika mazungumzo yao aligundua kuwa ni huyo ex-wake ambae ni uncle wangu. Mpaka tukio hili linatokea sweet wangu alikuwa hajui kama mm na huyo jamaa ni ndugu.

Bila hiana nilimuuliza huyo nani alinijibu kwa kutaja jina la huyo uncle wangu. Niliendelea kumuuliza anaishi wapi? akataja sehemu ile ile anayoishi uncle. Kusikia hivyo nikashtuka lakini sikumuonyeshea hiyo hali. Nikamuuliza ni nani yako? Alichonijibu sikuamini kabisa.

Alinijibu hivi:-
Kipindi kile nakutana na wewe ( mimi ) nilikuwa niko kwenye frustration za kuachana na huyu kaka kwasababu niligundua ananicheat baada ya hapo alisafiri kwenda china kimasomo. Sasa nashangaa leo ananipigia simu sijui kasahau nini.

Hayo yalikuwa ni maneno ya mpenzi wangu

Ndugu zangu kwa kweli niliishiwa nguvu

Maswali yangu ni haya:-

Je niendele na plani za kumuoa? Kiukwele nampenda sana
Vipi kuhusu hatima yake na uncle? kwasababu uncle anaonyesha bado anampenda huyu binti
 
dah pole kijana ukajua umepata kumbe umepatikana!! but kaa nae ujaribu kumueleza ukweli na ana msimamamo gani kwako maana unaweza ukasema anakupenda kumbe anaempenda zaidi ni uncle
 
Seem uncle ni mzee wa totoz...Ninachojua wazee wa totoz wengi huwa hawaoni maumivu kuacha au kuachwa ila huwa wanapenda sana kukumbushia enzi zile...

I think ni kukaa na uncle na kumueleza ukweli vinginevyo ujiandae kuwa RISK TAKER....
 
Anakupenda ndiyo maana kakuambia ukweli.kama unampenda continue with your plans.Jiamini.wewe mwanaume.Je angekuficha ingekuwaje?
 
Duh, nitarudi ngoja nitafakari kwanza ila pole
 
dah pole kijana ukajua umepata kumbe umepatikana!! but kaa nae ujaribu kumueleza ukweli na ana msimamamo gani kwako maana unaweza ukasema anakupenda kumbe anaempenda zaidi ni uncle

Nimemuambia ukweli hata yeye alishangaa sana. Nilijaribu kumuambia tuachane baada ya kufahamu hiki kisa but alikataa na analia sana. bado anasisitiza tuoane
 
muachie uncle maana amekutanguia
 
Seem uncle ni mzee wa totoz...Ninachojua wazee wa totoz wengi huwa hawaoni maumivu kuacha au kuachwa ila huwa wanapenda sana kukumbushia enzi zile...

I think ni kukaa na uncle na kumueleza ukweli vinginevyo ujiandae kuwa RISK TAKER....

najiandaa kumueleza uncle ukweli ila inauma sana
 
Kwa mtazamo wangu huyu binti ni mkweli sana!! Naomba mpelekee hongera zangu. Deep down ongea naye na mkubaliane pia weka wazi kuwa huyoa ex wake ni uncle wako. Sasa hapo pima tena reaction yake.
 
Katoka masomoni China!!!! Kwa wadada zetu hawa wa kibongo tunavyo wajua. Kuwa makini sana. Angekuwa ametoka mikere kule kwetu kurio kwamtoro angeikata hiyo simu. Kitendo cha kuipokea tu, swadakta
 
Kwa mtazamo wangu huyu binti ni mkweli sana!! Naomba mpelekee hongera zangu. Deep down ongea naye na mkubaliane pia weka wazi kuwa huyoa ex wake ni uncle wako. Sasa hapo pima tena reaction yake.

Nimesha muambia. Alijisikia vibaya baada ya kumueleza na akasisitiza hawezi kuachana na mm na ananiomba nisimuache
 
Doh..tueleze tabia za uncle wako...!😛layball:
 
Huyo ndiyo mke na mjulishe uncle wako akae mbali naye.
Umemuoa alafu siku Anko wako kaja kukutembelea mjomba wake. Kwa bahati mbaya wewe unakuwa umetoka kisha unarudi unawakata wako sitting room wanaongea. Utajisikiaje?
Kiufupi huyo demu akufai kumuoa. Na mbaya zaidi issue ikilink kwa ndugu jamaa na marafiki
 
Nimemuambia ukweli hata yeye alishangaa sana. Nilijaribu kumuambia tuachane baada ya kufahamu hiki kisa but alikataa na analia sana. bado anasisitiza tuoane

kwa mswahili mimi huyu kwetu hatufai maana hata ukimuoa bado kutakuwa kuna uadui kati yako na uncle,kati ya demu wako na uncle,iko siku kitalipuka na mambo yenu vijana ya wivu wa mapenzi kuliko wivu pesa mmmmmh.mapenzi huwa hayafi ila yanasinyaa udungu huwa haufi sasa hapo akili ku mkichwa ..............................
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…