Wakati tuko shule ya Tulifundishwa historia ya vitu mbali mbali hasa kuhusu sisi waafrika na mambo yetu, mojawapo ya hoja au misingi ya somo hili ni kuelezea ugunduzi wa vitu mbali mbali na wazungu vilivyomo uku kwetu barani Afrika
Msingi huu ulipelekea somo hili kutuelezea mambo meengi ya ugunduzi wa wazungu kutambua maliasili na rasilimali zetu, lakini swali ni Je hayo yote yalikuwa kweli???
Tuanze kwa kuangalia mzungu wa kwanza kuuona mlima Kilmanjaro kulingana na msingi wa somo alikuwa John Rebman lakini je ni nani alieweza kujua kuwa huyu ni John Rebman?? na ni kweli hakukuwa na mwingine aliewahi kuuona kabla yake?? na nn kilitumika kupeleka huyu kutamkwa wa kwanza?
Si hayo tu ni mengi sana yanahitaji LOGICAL REASONING KUAMINI WANACHOSEMA.
Mi mzungu ninayemuamini ni huyu aliyekitengeneza kitu na kinatumika(mfano Facebook,forums,whatsaap,taa,umeme,gari,ndege n.k) lkn hao sijui wa kwanza kuliona ziwa Victoria,ml Kilimanjaro nawaona wanatuzingua tu
Nalog off
Logic ( mantiki) ya ugunduzi huo ni kwamba kabla ya hao, wanaotajwa hakukuwa na mtu mwingine mwenye ngozi nyeupe aliyefanikiwa kufika mahali hapo na kuona kwa macho matupu na hata kunusa harufu ya pale panapotajwa, kisha akawapasha habari wenzake, wa huko kwao au ugenini. Kumbuka, watu hao walisaidiwa na wapagazi na walughalugha ambao ndiyo walikuwa wenyeji wa maeneo hayo.
Kuna haja ya kuandaa mitaala iendane na sisi,hata simulizi zetu zingine hazitufai kwa kipindi hiki mfn kiuchumi inatusaidia nini kukaririshana kwamba walitutesa wakati huuhuu tunashirikiana nao?tunazitesa fikra na hisia za watoto hivi vitabu vyingine viwekwe maktaba tu kama hadithi au vya ziada visiwe kiada