Local airline ikikukosea haki unadai wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Local airline ikikukosea haki unadai wapi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by robert_m, Nov 27, 2011.

 1. r

  robert_m Member

  #1
  Nov 27, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Inatokea mara kwa mara mtu unapata usumbufu hasa airport ya Mwanza kwa makosa ya airliner. Leo nimepata uzoefu ambao kwa kweli umeniudhi sana na nafikiri kunahaja ya kuchukua hatua wakati mwingine, kwa kuwa watumishi wanaona kuwa ni jambo la mazoea na wanaweza kufanya chochote.

  Nilikuwa na tiketi ya Precision Air ya kundoka saa mbili usiku (20:00hrs). Nimefika Airpot saa Kumi na mbili na nusu jioni (18:00hrs). Baada ya kuonyesha tiketi yangu nikakabidhiwa "Boarding Pass" inayonitaka nisafiri saa tano na nusu usiku (23:30hrs) inamaana unafika Dar Saa Nane usiku kwa wastani. Nilishangaa kwa maana hatukupewa taarifa yoyote ile, na kwa kiasi fulani nilifikiri ni afadhali ningesafiri kesho yake.

  Lakini cha kusangaza ni kwamba watumishi wa airline hawakuchukua hatua zozote hata kutupa nafasi ya kuchagua tufanye nini, zaidi tu ya kutulazimisha kwenda na ndege husika. Walichotoa ni soda moja na andazi tu kitu ambacho kulingana na mazingira hakikuwa kitu. Nilijaribu pia kuzingatia hatari za kufika Dar usiku kiasi hicho. Pia wafanyakazi hawakuchukua hatua za kutunza kwa ubaridi mizigo yetu ya samaki wabishi ambao nilikuwa nimetoka kununua tu. Nikaona hii ni hasara nyingine.

  Naomba waungwana wanisaidie nipate kuelewa, hivi tukiwa na matukio kama haya haki yetu tunaweza kuidai wapi kama wahusika wanatupuuza?
   
Loading...